Rais Magufuli ashuhudia makabidhiano ya Dhahabu Kg 35 iliyokamatwa nchini Kenya

Unaweza kuta UK alikuwa tungi halafu Monica ni side chick wake, awe amemwaga mchele kwenye kuku wengi.
 
Hebu weka picha ya huyo Monica

huyo hapo
a-32-1024x683.jpg
 
Sitasema mengi, iliyopo hapa mbele yetu ni kilo 35.34 ya dhahabu na pia baada ya kumrejesha Patrick Ngowi mwezi Januari 2019 ..

Nimejaribu kuvuta kumbukumbu huu ya hili jina PATRICK NGOWI, I stand to be corrected.

Miaka kama sikosei 3-5 nyuma, jarida maarufu la Forbes liliwahi kutoa majina ya vijana wenye mafanikio makubwa with 30's age. Katika list alikuwepo mtanzania mwenye jina Patrick Ngowi ambaye alikuwa na kampuni inaitwa Helvetic located in Arusha City.

Nimesikitika sana if he's the one, what happened to him!? According to Forbes, alikuwa akitengeneza almost US $1mil per year as profit.

Kuna anayejua what happened to this fella
 
Kwan
Rais Magufuli atashuhudia makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya itakayowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais wa Kenya Mhe. Kenyatta leo Julai 24, 2019.

Hafla ya makabidhiano hayo itafanyika Ikulu Jijini DSM kuanzia saa 4:00 asubuhi.

DPP, Biswalo Mganga:

Nakushukuru Rais na Serikali unayoongoza kwa sababu ulivyokuwa Chato mapumzikoni uliongea na Rais kuhusu kuweza kurudishwa kwa dhahabu iliyokamatwa.

Tarehe 15 Februari, 2018, dhahabu kilo 35.34 ilikamatwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta wakati Baraka Chaulo akisafiri na Precision Air. Ilitua Mwanza halafu ikaenda Nairobi ikakamatwa. Wakurugenzi wa upelelezi Kenya na Tanzania walianza upelelezi Hii inaonesha ushirikiano mzuri tulio nao sisi kama wana Afrika Mashariki

Mimi na DPP Haji tuna msimamo mmoja kuwa hatuwezi kuacha mhalifu akajificha. Nchi zetu haziwezi kuwa vichaka vya wahalifu. Na msimamo huo nanyi mnao na ndio maana Rais Kenyatta alipokuja mliweza kukubaliana kuwa dhahabu irejeshwe

Leo sio tunashuhudia kukabidhiwa kwa dhahabu iliyokamatwa Kenya bali tunashuhudia kurejeshewa fedha ambazo zilikamatwa Kenya baada ya kuibiwa Tanzania mwaka 2004. Hili ni tukio ambalo lilitokea Mei 21, 2004 wakati benki ya NBC tawi la Moshi lilipovamiwa

Kati ya Wahalifu, mmoja alikamatwa nchini Kenya na taratibu za kumrejesha nchini zilishindikana kwa kipindi chote. Lakini kwa ushirikiano tulionao hasa na ndugu yangu DPP Haji naomba kusema Mshtakiwa huyo naye amerejeshwa Tanzania na sasa kesi ipo Moshi

Tulikuwa tunasubiri ushahidi wa vielezo alivyokamatwa navyo ambavyo ni Tsh. Milioni 170 Dola za Kimarekani 77,500 na Ksh. Milioni 171 na mia 600. Vyote naamini wameturudishia ili kesi iendelea. Sisi tunaamini ushirikiano wetu ambao ni sehemu ya ofisi yetu

Naendelea kukushukuru Rais kwa kuwa umekuwa unatoa msaada mkubwa kwangu na ofisi ya mashtaka kuhakikisha dira ya haki, amani na usalama kwa maendeleo inapatikana. Niwashukuru tena viongozi wa ngazi zote, vyombo vya upelelezi, ulinzi na Mahakama

DPP Noordin Haji (Kenya):

Kwanza Rais utaniwia radhi kwa maana Kiswahili kidogo sisi Kenya kinatupiga chenga. Nikichanganya na kizungu, utanisamehe. Sisi tumekuja kwa moyo mkunjufu kama ndugu, nchi jirani. Kama alivyosema Biswalo tumefanya mengi kuimarisha uhusiano bora

Sitasema mengi, iliyopo hapa mbele yetu ni kilo 35.34 ya dhahabu na pia baada ya kumrejesha Patrick Ngowi mwezi Januari 2019 napenda kukabidhi Tsh. milioni 170, USD 76,500 na USD 1,000 kwa ajili ya 'denomination' na pia Ksh. Milioni 171 na 600

Rais kama alivyosema ndugu yangu Biswalo, sisi tunashirikiana kuhakikisha kuwa hakuna wahalifu katika nchi zetu. Mimi nataka kukuhakikishia Rais kuwa Watanzania tumewaweka moyoni kama ndugu zetu na tutawahudumia kama Wakenya wenzetu. Nakushukuru sana

Waziri wa Mambo ya Nje Kenya, Monica Juma:

Leo tuna furaha sana, nilikuwa kwa muda mrefu nikitamani kufika Dar. Tumefika hapa leo kuleta ujumbe kutoka kwa ndugu yako Rais Kenyatta. Amenituma kukuletea wewe ujumbe na pia dada na kaka zetu wa Tanzania kupitia wewe

Tunashukuru kwa kumpokea Rais wetu kule Chato. Nakumbuka tulipokutana Entebbe mlituamrisha kuwa tusipofanya haraka ninyi mtajipangia kukutana. Tulipopata simu, nikamuuliza Rais nitakuja Chato? Akaniambia huwezi, nitakwenda mwenyewe kwa kuwa nyie hamkupanga

Tunashukuru sana, Wakenya wote walikuwa wanaangalia wakitamani kuja Chato. Tunaomba na sisi utualike Rais. Picha zilikuwa za kufana sana. Tumefika hapa kutimiza maamuzi baina yako na Rais Kenyetta. Tukifanya kazi pamoja tutafanikiwa kama walivyosema ma-DPP

Tumefika kukukabidhi vyote alivyovisema DPP Haji hapa ili tuweze kuimarisha uhusiano na Tanzania. Umoja ni nguvu kama tusemavyo. Tunashukuru tumekaribishwa vizuri na maafisa wote waliokuwa uwanjani. Tumefurahi sana

Waziri Kabudi

Leo ni siku maalumu, ya kipekee na kihistoria. Zaburi ya mwisho ktk vitabu vya Zaburi inasema "Ni vema ndugu wanapokutana, wakakaa pamoja wakazungumza na kufurahi". Leo yametimia ya kile kitabu cha mwisho kabisa cha Zaburi kwa kuwataka ndugu wakae pamoja

Sisi na Kenya ni zaidi ya Majirani, ni ndugu wa damu. Na mipaka hii ilipochorwa na kuwekwa katika mkataba palikuwa na ubishani mkubwa sana. Na ubishani haukuhusisha Mlima bali Ziwa Victoria kuwa nani atawahi kupata chanzo cha mto Nile

Professa Boga (Waziri Kilimo, Kenya) Mdigo huyu ana ndugu zake Wadigo wa Maramba. na mimi namfahamu tumesoma wote Ujerumani. Ni mtaalamu Mahiri sana wa Sayansi ya Kilimo na utafiti, na amekuwa kwa miaka mingi sana 'external examiner' Chuo Kikuu DSM

Kubwa leo hii ni shukrani nyingi kwa Rais Kenyatta, amefanya maamuzi makubwa. Asingeweka mkono mali hizi zirudi zilipotoka, isingewezekana. Ni kweli mambo haya yanawekwa kwa sheria lakini sheria haina uhai hadi ipuliziwe na binadamu ambao ni Marais wetu

Baada ya Wadigo wanafuata Wakamba Kenya na Tanzania. Mkamba wa Kenya ni Monica Juma ambaye yeye tulishirikiana sana kuanzisha 'Center for Forced Migration' ya UDSM - Yeye alifanya PhD yake Oxford katika mambo ya Forced Migration na refugees na yeye ni Mkamba

Nitaomba Rais baada ya vikao vya SADC niende Kenya kumsalimu ndugu yangu Waziri Monica na mimi nitatafuta shughuli ya kukualika (Waziri Monica) Mwanza. Mwanza ndio lango la Afrika Mashariki, ukifika Mwanza tutafika tu Chato ili ndoto yako iweze kutimia

Hotuba ya Rais Magufuli

Nijaribu kwanza kumpigia simu rafiki yangu nimwambie mzigo umefika (Anampigia Rais Kenyatta inaita bila kupokelewa). Bado hajapokea sasa akipokea sawa nitaongea, naiacha hapa hapa jamani

Siku ya leo kwanza naiona ni 'very special'. Nianze kumshukuru Mungu na napenda pia kumshukuru Kenyatta kwa uaminifu na upendo alionao. Kama ulivyosikia kwa Mjumbe dada yangu Monica. Dada yangu wa damu naye ni Monica, sitafanya vibaya kumuita dada yangu

Kwanza napenda kushukuru vyombo vya ulinzi vya Kenya kwa kazi kubwa viliyofanya. Dhahabu ilikamatwa katika Uwanja wa Jomo Kenyatta kwa Mtanzania aliyekuwa akiisafirisha kwenda Dubai

Nakumbuka Rais Kenyatta alipokuja Chato tulizungumza mambo mengi na nikawa nimemuomba kuwa kuna pesa na dhahabu zetu zimekaa huko. Akaniambia nataka nikuhakikishie Rais kuwa mwezi wa saba hautapita, dhahabu na pesa hizo zitakuwa zimerudi Tanzania

Namshukuru sana kwa uaminifu wake, hivi vitu vya fedha na dhahabu vinahitaji moyo wa jiwe. Na Uhuru na serikali yake wana upendo wa pekee. Dhahabu hizi zingepigwa tu juu huko na hizi fedha kuendelea kuwepo kwa zaidi ya miaka 15 ni uaminifu mkubwa

Lakini na mimi mnipongeze basi kidogo. Kwa sababu inawezekana wangekuwa wengine tungepiga dili na Mzee Kenyatta. Wala msingejua wala Kenyatta asingehangaika kuchukua ndege zake kutuma mzigo huu na mimi ningemwambia hii bwana ifikishe tu sehemu

Nchi za Afrika zimebarikiwa utajiri mkubwa ikiwemo madini lakini zimekuwa hazinufaiki sana. Madini mengi yanaibwa ama kwa kutoroshwa ama kwa mikataba mibovu na ya kinyonyaji na wengine wanaohusika ni wenzetu

Tumechukua hatua mbalimbali za kudhibiti utoroshwaji wa madini yetu na mapato yamekuwa yakiongezeka. Mathalani kwa mwaka 2017/18, tulipanga kukusanya Tsh. Bilioni 191 lakini tukakusanya Tsh. Bilioni 301. Mwaka 2018/19 tukakusanya Tsh. Bilioni 335

Kwa upande wa kukamata wahalifu, kwa miaka mitatu iliyopita jumla ya matukio 102 yameripotiwa ambapo yalihusisha madini yenye uzito wa gramu milioni 163,576,416.45 na karati 6,826.38. Thamani ya madini yote haya inakadiriwa kuwa zaidi ya Tsh. Bilioni 45

Napenda kulipongeza Bunge kwa kupitisha marekebisho ya sheria kwa mwaka 2017. Nampongeza DPP na wanasheria wote. Naipongeza Wizara ya Madini kwa kuimarisha usimamizi na pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kuzidisha udhibiti dhidi ya wizi

Dhahabu hii imetoroshwa kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza ikapandishwa ikaenda hadi KIA na kufika Kenya. Wa kupongezwa hapa ni vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya. Najua wakuu wa vyombo vya ulinzi mpo hapa lazima niwatandike hapa hapa mbele

Lazima ujiulize je, ilipokuwa inatoka Mwanza au KIA vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania vilikuwa vinafanya nini? Je, vilishirikiana na mhalifu au kumuachia? Je, dhahabu ngapi zimesafirishwa bila watuhumiwa kushikwa? Hii nawaachia ninyi

Mnafanya kazi nzuri ila kuna sehemu hamfanyi vizuri. Hii inadhihirisha aibu kwetu kwa vyombo vyetu kwamba tunaachia mali mpaka zinaenda kushikwa kule. Nitaandika barua rasmi ya kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa niaba ya Watanzania

Niviombe vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania, shirikianeni sio kila mmoja afanye kivyake ili mali ya Watanzania isiendelee kuibiwa. Hii ni kwa bahati tu mwizi alichagua njia kwenda Kenya. Inawezekana angepita baharini tusingemuona

Ndio maana Kenya wanahitaji heshima kubwa kwa hili. Maaskari walioshika mali hii tutapanga tuone kwa namna gani tutawazawadia. Ndugu zangu ngoja nimpigie tena Kenyatta au ninawachelewesha? Hakuna matata. (Rais Kenyatta bado hajapokea simu)

Kwenye suala la fedha hili nalo ni la kupongeza. Ni fedha nyingi tangu 2004 zimetunzwa. Nashukuru sana. Kama walivyosema Mawaziri Kabudi na Monica na Ma-DPP, tutashirikiana zaidi. Mkosaji wa Kenya ni mkosaji wa Tanzania na ukikosa Tanzania umekosa Kenya

Niwakaribishe wawekezaji hususani ndugu zangu wa Kenya kuja kuwekeza katika kununua madini yetu. Pia kuwekeza katika viwanda vya uchenjuaji na uongezaji thamani. Mnakaribishwa sana. Sisi ni ndugu na hakuna atakayevunja undugu huu milele

Rais Kenyatta alisema atawatuma viongozi wa Wizara ya Kilimo na amemtuma Profesa hapa. Wanataka kununua mahindi na hawatanunua mahindi yaende kusagwa kule bali watanunua unga ili viwanda vya hapa watengeneze na kuongeza thamani

Nimeshazungumza na Mkuu wa Majeshi, wao wana viwanda vya mahindi. Hivyo Profesa na CDF kaeni muelewane namna nzuri ya kusafirisha unga. Jeshi linunue kwa wakulima mahindi na kisha wawauzie. Si lazima mfanye biashara na Jeshi tu hata Wafanyabiashara wengine

Pia Rais Kenyatta aliniambia makusudio yake ya kutaka kununua gesi kutoka Tanzania. Tuna ethane nyingi. Wanataka wakaitumie na amemtuma Katibu Mkuu wake anayehusika na gesi hivyo Wizara ya Madini mkae nae. Msumbiji imetutangulia sana wakati tulianza pamoja

Sisi tukabaki kufukuzana tu kwasababu hata yule mtaalamu aliyekuwa anahusika na gesi aliyefanya kazi nzuri kule Marekani alisimamishwa tangu mwaka 2016. Alisimamishwa kwasababu alikataa kuchukua rushwa ya kampuni fulani iliyokuwa inataka vitalu 2 baharini

Alisimamishwa kwa miaka miwili, mitatu na juzi nilimrudisha. Sifahamu kama Wizara imemrudishia Ukurugenzi wake wa TPDC. Wizara inayohusika ikae na hawa wanaohitaji gesi ili gesi ianze kuingiza fedha. Najua wanahitaji na makaa ya mawe, nayo tunaweza kuuza

Ni jukumu letu sasa Watanzania tuliopewa nafasi kusimamia maeneo hayo. Wenzenu wamekuja na nitashangaa mkae tu hivi hivi. Unajua sisi tunachelewa kuchangamka, wenzetu wa Kenya wamechangamka haraka. Sasa Wizara husika mchangamke, wamekuja kwa upendo mkubwa

Rais Magufuli (Akiongea na Kenyatta): Asante sana, dada yangu Monica ameshashusha mzigo hapa

Kenyatta: Pole niliweka simu kando nilikuwa na Mkutano ila asante sana tulisema mali ya Wananchi lazima irudi kwa Wananchi

Rais Magufuli: Sawa kabisa

Rais Kenyatta: Sisi tunataka tuhakikishe kwamba pale ambapo wananchi wametupatia imani yao kutupatia uongozi, tumetenda haki na kulinda mali yao. Na mali hiyo iende kujenga hospitali, shule barabara na kuunganisha watu wetu. Walaghai hawana nafasi

Tuendelee kushirikiana namna hiyo. Kenya na Tanzania tulisema hatuna mpaka, sisi ni kitu kimoja na tuendelee kuwa hivyo. Tushirikiane mpaka tufute umaskini kwenye nchi zetu. Kwa hayo machache nasema Mungu abariki Watanzania wote tuendelee na ujirani

Rais Magufuli: Nilikuwa nawaambia hapa tungekuwa sisi watu wabaya hii dhahabu wewe ungeikata huko moja kwa moja wala hela zisingekuja. Nikawaambia ningekuwa mbaya tungezungumza kwa siri wasingeona hizi hela, tungegawana. Wangebaki kuandika kwa magazeti ila hela imeliwa

Nashukuru sana Rais Kenyatta kwa kumtuma Waziri Monica. Mbali ya kuwa ni mzuri lakini anachapa kazi na anawakilisha vizuri sana Kenya

Rais Kenyatta: We wachana na huyo arudi nyumbani hapa. Nitakutumia wale ambao...

Rais Magufuli: Asante sana ndugu yangu

Dotto Biteko, Waziri Madini

Kuna watu wanazungumza mambo utadhani hawapo Tanzania. Wanazungumza kuwa tumekimbiza Wawekezaji na vitu kama hivyo. Nikuhakikishie Rais, kwenye historia ya nchi kwenye sekta ya madini hatujawahi kutoa leseni ya uchimbaji yenye gharama kubwa

Tangu mwaka 2010, Kwa mara ya kwanza kwenye kipindi chako leseni yenye uwekezaji wa USD Milioni 100 itatolewa. Tunazo leseni mbili tutazitoa kwa ajili ya uchimbaji mkubwa huo. Kwa uchimbaji mdogo tumetoa leseni 2,673. Leseni uchimbaji wa kati 32

Leseni za utafiti tumetoa 105. Ulisema lazima tuongeze thamani ya madini ndani ya nchi, sasa sisi tulipata wawekezaji 37 katika eneo la 'refinery na smelter'. Tuliwachambua na tumetoa leseni mbili za 'refinery' kwa dhahabu na moja kwa ajili ya 'smelter'

Nataka nieleze Wizara ya Madini hatustahili sifa yoyote ila wewe kwa sababu kwa wakati wote ulikuwa ukitoa maelekezo. Wanaostahili sifa hizi wengine ni Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kusimamia madini hayo

Kwahili nipo pamoja na wewe Raisi wa Nchi yangu
 
Tangia nizaliwe miaka 30 iliyopita na hata nilipozaliwa Mara ya pili miaka 15 iliyopita, sijawahi kusikia Nchi yoyote Duniani imekamata na Kurejesha Fedha na Dhahabu katika nchi zilipoibwa. Hapa Mheshimiwa Mkuu wa Nchi nategemea wazee wastaafu, Zitto Kabwe na Mtandao wa Jamii Forum, na Dada yetu wa Kambo kule Marekani tuungane Kukupongeza. Unastahili Tuzo ya Diplomasia ya Uchumi. Nadhani vyuo vyetu vikuu vitakutunuku PhD (PhD in Economic Diplomacy). Natarajia Asasi za Kiraia pia zitatoa tuzo mbalimbali. Kuishawishi Nchi nyingine kurejesha fedha na Dhahabu ilizokamata????, That's a big success. Wengi wamepatwa Butwaa, wanatafuta wakosoe nini. Ushindi wako ni Ushindi wetu na Ushindi kwa Taifa. Nakupongeza sana kwa Ushindi Huo, Tu nakupenda, tunakuombea na Kukuunga Mkono. Tupo Pamoja nawe Baba. Naishukuru pia serikali ya Kenya kwa huo uungwana.
 
Halaf yeye alivo na roho mbaya ya kunyima wengine haki ya kuishi alichoma vifaranga kutoka Kenya vikiwa hai hadi vikateketea kwa moto, kila nikifikiria tukio lile machozi hunitiririka😢😢😢😢

It shows the kind of a person he is...evil in soul, evil in deeds!
 
Tangia nizaliwe miaka 30 iliyopita na hata nilipozaliwa Mara ya pili miaka 15 iliyopita, sijawahi kusikia Nchi yoyote Duniani imekamata na Kurejesha Fedha na Dhahabu katika nchi zilipoibwa. Hapa Mheshimiwa Mkuu wa Nchi nategemea wazee wastaafu, Zitto Kabwe na Mtandao wa Jamii Forum, na Dada yetu wa Kambo kule Marekani tuungane Kukupongeza. Unastahili Tuzo ya Diplomasia ya Uchumi. Nadhani vyuo vyetu vikuu vitakutunuku PhD (PhD in Economic Diplomacy). Natarajia Asasi za Kiraia pia zitatoa tuzo mbalimbali. Kuishawishi Nchi nyingine kurejesha fedha na Dhahabu ilizokamata????, That's a big success. Wengi wamepatwa Butwaa, wanatafuta wakosoe nini. Ushindi wako ni Ushindi wetu na Ushindi kwa Taifa. Nakupongeza sana kwa Ushindi Huo, Tu nakupenda, tunakuombea na Kukuunga Mkono. Tupo Pamoja nawe Baba. Naishukuru pia serikali ya Kenya kwa huo uungwana.

Kweli wajinga ndio waliwao, dhahabu kilo 35 mubashara mbele ya rais kila mtu aone, lakini dhahabu kilo 300+ zilizokamatwa hazijaonyweshwa na kama hiyo haitoshi polisi walioshiriki igizo lile wamerejeshwa kazini! Hivi bado mnadhani kuna wajinga wa hivyo?
 
Ulijiuliza kwanini huyo mtu wako alikosa uungwana na kuamua kupiga kiberiti vifaranga vya Kenya na kupora mifugo yao badala ya kuwarudishia kama wao walivyofanya kwenye dhahabu ? kwa taarifa yako tukio hili la wakenya kurudisha dhahabu kwenye nchi iliyochoma vifaranga vyao limeivua nguo Tanzania
 
Kweli wajinga ndio waliwao, dhahabu kilo 35 mubashara mbele ya rais kila mtu aone, lakini dhahabu kilo 300+ zilizokamatwa hazijaonyweshwa na kama hiyo haitoshi polisi walioshiriki igizo lile wamerejeshwa kazini! Hivi bado mnadhani kuna wajinga wa hivyo?
Iko shida mahali hili liko wazi
 
Naunga mkono hoja, sasa tunachosubiri sio kusubiria ni dhahabu ya nani, bali walioipitisha toka Mwanza hadi Kia undected halafu kuja kukamatiwa Nairobi!.
Ingekuwa ni enzi za Nyerere, saa hizi saa nyingi barua za Mawaziri wawili zingeishatua Meza kuu!. Sijui hawa watu wanasubiri nini au mpaka kitokee nini ndipo wawajibike?!.
P.
 
JPM atawashangaza sana, kwa ubunifu, Kenya na Tanzania baada ya yule mbaguzi kuchafua hali ya hewa mambo yametulizwa, JPM na Uhuru (Uhu Magu) wako poa, rafiki yake Odinga anaendesha maisha yenye furaha na amani Kenya.

Jamaa ni mbunifu na akili zake ziko on kila sekunde. Hafanyi kazi kwa mazoea, ingekuwa mazoea kumpigia simu Rais mwenza ya kikazi pengine kungeundwa kamati ya maandalizi na utaratibu yenye wajumbe wanadiplomasia wabobezi. Yeye kanyanyua mobile yake kapiga papo kwa papo. Ooh fantastic..
 
Tangia nizaliwe miaka 30 iliyopita na hata nilipozaliwa Mara ya pili miaka 15 iliyopita, sijawahi kusikia Nchi yoyote Duniani imekamata na Kurejesha Fedha na Dhahabu katika nchi zilipoibwa. Hapa Mheshimiwa Mkuu wa Nchi nategemea wazee wastaafu, Zitto Kabwe na Mtandao wa Jamii Forum, na Dada yetu wa Kambo kule Marekani tuungane Kukupongeza. Unastahili Tuzo ya Diplomasia ya Uchumi. Nadhani vyuo vyetu vikuu vitakutunuku PhD (PhD in Economic Diplomacy). Natarajia Asasi za Kiraia pia zitatoa tuzo mbalimbali. Kuishawishi Nchi nyingine kurejesha fedha na Dhahabu ilizokamata????, That's a big success. Wengi wamepatwa Butwaa, wanatafuta wakosoe nini. Ushindi wako ni Ushindi wetu na Ushindi kwa Taifa. Nakupongeza sana kwa Ushindi Huo, Tu nakupenda, tunakuombea na Kukuunga Mkono. Tupo Pamoja nawe Baba. Naishukuru pia serikali ya Kenya kwa huo uungwana.
improve your hand writing.
 
Naunga mkono hoja, sasa tunachosubiri sio kusubiria ni dhahabu ya nani, bali walioipitisha toka Mwanza hadi Kia undected halafu kuja kukamatiwa Nairobi!.
Ingekuwa ni enzi za Nyerere, saa hizi saa nyingi barua za Mawaziri wawili zingeishatua Meza kuu!. Sijui hawa watu wanasubiri nini au mpaka kitokee nini ndipo wawajibike?!.
P.

Usishangae ukifuatilia vizuri ukakuta ni igizo kama maigizo mengine. Hivi mawaziri wafukuzwe kwa kipi kama polisi waliosimamia wizi wa kilo 300+ wamesamehewa na kurudishwa kazini, badala ya kifungo na kupoteza kazi? Fuatilia vyema kama hutaona ni igizo.
 
Back
Top Bottom