Rais Magufuli aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri, Ikulu Dar es Salaam

Waziri Dr Shein alikuwepo??? Simuoni hapo!
View attachment 443605
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo tarehe 07 Desemba Ikulu jijini Dar es Salaam. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU
 
Kweli huyu nanihii yumo humu. Nimepiga kelele kuhusu kutokuwepo vikao vya baraza la Mawaziri na haukupita muda mrefu kikao cha baraza la Mawaziri kinafanyika. Natumai vikao hivi vitapunguza sana matamko uchwara na zile kauli za "Nimenukuliwa vibaya"
Kama ndiyo umeona baraza hili la mawaziri tangu rais Magufuli aapishwe basi una matatizo yako.
 
Weka ushahidi badala ya kukurupuka bila ushahidi wowote. Vikao vya baraza la Mawaziri havifanywi siri weka hata picha au link ya habari kuhusu vikao vilivyopita.

Kulikuwa na kikao kimoja tu cha maandalizi ya Bunge la bajeti sikusikia wa kusoma popote kuhusu kikao kingine cha baraza la Mawaziri.

Mwanzoni walisema Magufuli hawezi sababu tatizo ni mfumo.

Baada ya kuanza kuwatumbua mafisadi wenzao wakasema ni nguvu ya soda.

Baada ya mwaka mzima kuisha huku sindano zikiwaingia kwa kasi ile ile na soda haiishi nguvu, sasa wameanza kupongeza!

Safi sana Yericko, natamani ufipa yote ipokee ubatizo wa moto kama uliopokea wewe na hatimaye kuungana na rais bora kabisa duniani kulijenga upya taifa la Tanzania.
Ha ha ha ha
 
Kweli huyu nanihii yumo humu. Nimepiga kelele kuhusu kutokuwepo vikao vya baraza la Mawaziri na haukupita muda mrefu kikao cha baraza la Mawaziri kinafanyika. Natumai vikao hivi vitapunguza sana matamko uchwara na zile kauli za "Nimenukuliwa vibaya"
Kikao hakusaidii,sanasana atawapa oda tu,nini wakafanye,nini waache.atakaebisha amejiondoa mwenyewe.
Nimeona hapo mtoa mada kamtaja waziri mkuu,nilitegemea atamtaja mwanasheria mkuu kwa sababu angeweza kuwafafanulia baadhi ya sheria,ili kupunguza matamko.LAKINI NAAMINI MKUU WA KIKAO HATA SHERIA ANAZIJUA VIZURI TU.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sheria ya vyombo vya habari inakataza kutoa habari zinazo husu baraza la mawaziri...angalia hii post yako.
 
Mbona mezani naona maji tu ............au juice na wine zimeisha huko mjini
 
Sheria ya vyombo vya habari inakataza kutoa habari zinazo husu baraza la mawaziri...angalia hii post yako.
Tumsubirie Greson Msigwa aje atupe feedback,huenda michongo yetu ya ajira inaandaliwa
 
Weka ushahidi badala ya kukurupuka bila ushahidi wowote. Vikao vya baraza la Mawaziri havifanywi siri weka hata picha au link ya habari kuhusu vikao vilivyopita.

Kulikuwa na kikao kimoja tu cha maandalizi ya Bunge la bajeti sikusikia wa kusoma popote kuhusu kikao kingine cha baraza la Mawaziri.
Hiki kikao cha cha baraza la mawaziri ilikuwa Sep 29, je ilikuwa ni maandalizi ya bunge la bajeti?

Weka ushahidi badala ya kukurupuka bila ushahidi wowote. Vikao vya baraza la Mawaziri havifanywi siri weka hata picha au link ya habari kuhusu vikao vilivyopita.

Kulikuwa na kikao kimoja tu cha maandalizi ya Bunge la bajeti sikusikia wa kusoma popote kuhusu kikao kingine cha baraza la Mawaziri.
Rais Magufuli aongoza Baraza la Mawaziri Ikulu Jijini Dar es Salaam leo
Hilo baraza la mawaziri lilikawa Sep 29, 2016, je, ndiyo maandalizi ya bajeti?
 
Mwanzoni walisema Magufuli hawezi sababu tatizo ni mfumo.

Baada ya kuanza kuwatumbua mafisadi wenzao wakasema ni nguvu ya soda.

Baada ya mwaka mzima kuisha huku sindano zikiwaingia kwa kasi ile ile na soda haiishi nguvu, sasa wameanza kupongeza!

Safi sana Yericko, natamani ufipa yote ipokee ubatizo wa moto kama uliopokea wewe na hatimaye kuungana na rais bora kabisa duniani kulijenga upya taifa la Tanzania.
Kwani ameweza nini? Ujinga ni kuandika kama kasuku!
 
Back
Top Bottom