Rais Magufuli anza mwaka mpya 2017 na kusamehe

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,896
2,000
Mh. Rais Magufuli ninakupongeza kwa hotuba yako fupi jana Singida katika kanisa la Parokia ya Moyo mtakatifu wa Yesu.
Katika hotuba yako uliwaagiza watanzania KUPENDANA na KUSAMEHEANA.

Nami nakuunga mko kabisa kauli yako maana MSINGI wa UKRISTO wa kweli umejengwa katika UPENDO. ndiyo maana Biblia inasema
"MSILIPIZE kisasi ndugu zangu "Rom 12:17-20 Adui yako akiwa na KIU mpe MAJI na akiwa na NJAA mpe chakula maana ni kama kumwekea MAKAA ya moto kichwani"

Najua mwaka wa 2016 kuna
WENGI wamekuudhi na hata
KUKUSEMA vibaya na wengineVIBAYA sana
Kuna WENGI pia HAWAKUKUTAKIA MEMA mengine haya siwezi kuyaandika hata mimi yalinisumbua. Lakini naomba famya jambo moja la maana ambayo hiyo ndo TABIA ya Yesu Kristo. WASAMEHE wote(.......)
Hii itakusaidia KIROHO ma hata KIUTAWALA maana UTALISHUSHA joto la kisiasa na CHUKI zinazotokana na WAKUCHUKIAO!

Yesu akasema katika Mathayo 6:14 Kwa maana MKIWASAMEHE wale WALIOWAKOSEA baba yenu wa mbinguni naye ATAWASAMEHE ninyi Na MSIPOWASAMEHE baba yenu naye HATAWASAMEHE ninyi"

Anza mwaka 2017 bila MIZIGO yeyote. Neno linasema njia za MTU zikimpendeza Mungu, HUWAFANYA ADUI zake kuwa RAFIKI naye. Naomba tena regardless WALIVYOKUMIZA. Mwachie Mungu. ANZA kwa KUWASAMEHE.
Siwezi KUWATAJA majina yao hapa maana nitakuwa kama nakulazimisha.
Ila Mungu mwenyewe AKUAMBIE huyu na huyu."MSAMEHE".
Unielewe sizungumzii MAFISADI waliopora mali ya Watanzania na kuwaacha MASKINI. Bali ni wale
waliokuwa WAKIKUOMBEA MABAYA ama kukutakia MABAYA!
Uwe na mwaka mpya wa BARAKA tele!
 

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,306
2,000
Kusema sameheana siyo kusamehe!!
Labda yeye ndiye anaomba huruma tumsamehe..
 

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,125
2,000
Rais hana shida na watu wema isipokuwa wachochezi, wezi wa Mali za uma, mafisadi, wasiowajibika kazini, wala rushwa, wapiga dili, wakwepa kodi..wakisamehewa mtasema rais mzembe, dhaifu, tulijua tu nguvu ya soda, kaogopa..mtamalizia kuwa mnataka mabadiliko
 

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,896
2,000
Rais hana shida na watu wema isipokuwa wachochezi, wezi wa Mali za uma, mafisadi, wasiowajibika kazini, wala rushwa, wapiga dili, wakwepa kodi..wakisamehewa mtasema rais mzembe, dhaifu, tulijua tu nguvu ya soda, kaogopa..mtamalizia kuwa mnataka mabadiliko
Mkuu umesema kweli. Mimi sizungumzii watu kama wale uliowataja.
Nazungumzia hasa wale WALIOMUUMIZA Magufuli personaly/Yeye mwenyewe na familia yake.

Mambo ya WIZI kama rushwa ni kuwa WAKIRUDISHA ile MALI iwe ni NUSU ama yote WASAMEHEWE!
 

kalimbwane

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
710
1,000
Nasisi aliyetukosea tumfanyeje ili hali tungali kwenye joto ya maumivu yaletwayo na yeye mwenyewe?
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,217
2,000
Ana UTU ataelewa!
Sidhani, kwa sababu sio mara ya kwanza kuongea kama alivyoongea jana. Ni kawaida yake kuwa mnyenyekevu na mwenye maneno ya upendo na busara akiwa kanisani, lakini akitoka tu, anayaacha humo humo kanisani. Chuki au upendo hauko mdomoni mwa mtu bali moyoni mwake. Ndio maana wengi husema tu, lakini kuyatenda wanayosema inakuwa vigumu kwa kuwa hawayasemi kutoka ndani ya mioyo yao. Tusubiri tuone binadamu sio jiwe huenda akabadilika.
 

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
Aendelee hivyo hivyo,ni vizuri kila mtanzania akamjua alivyo ili 2020 tuwe na mteremko
Wanafunzi,wanasiasa,wafanyabiashara,watumishi aendelee kuwafanyia hivyo hivyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom