Rais Magufuli anasema hivi kuhusu misaada

Rais Magufuli anasema hivi kuhusu misaada

bora kuwa maskin jeuri kulikokujinyenyekeza kumba misaada mwishowe tutakubali USHOGA!!
viva maguuuu
 
Ni wakati wako sasa kufufua fikira ulizoua za kujitegemea. Fikiria namna ya kuifanya Tanzania nchi inayojitegemea kiasi cha kufikia kutoa misaada kwa nchi nyingine. Kama unaona uwezi kukaa katika Tanzania inayojitegemea anza sasa utaratibu wa kuukana uraia wa Tanzania na kutafuta uraia wa nchi nyingine itakayokidhi matakwa yako. Kwa nini unataka kila kitu ufanyiwe, yaani hata kufikiri unahitaji msaada...!!? Mnaaza kunifanya niandike kwa ukali kwenye jukwaa hili. TUJITEGEMEE muda ndiyo huu.
Mkuu sio tatizo kujitegemea tulikuwa na misamiati mengi tu ujamaa na kujitegemea Siasa ni kilimo mtakula sijuwi nn hakuna mipango maalum ya kujitegemea sasa iliobaki ni siasa tu hamna chochote miaka 50 tulikuwa na ujamaa na kujitegemea matokeo yake tumekuwa masikini wa kutupwa tusubiri yaliowakuta wamalawi na wazimbabwe .tulikuwa tunasubiri dona na unga wa muhogo kwa foleni ndio hayooo
 
Tatizo la watanzania wengi tunawaza kitumwatumwa, watu wanadai tutaishije bila msaada, huo ni utumwa
Mkuu kuna mtoa mada ameomba uchanganuzi wa jinsi ya kupata pesa za kureplace hizo tulizokuwa tunapewa kama msaada. Only that.
 
KUONGEA NI RAHISI SANA KULIKO KUTENDA....na tena utendaji usio open ili tujue ni mchanganuo na mwelekeo upi utakaotufanya tuweze kujitegemea.

Mfano: Kujitegemea ni jambo zuri ila Je ni kwa vipi zitapatikana hizo pesa zote ambazo hatutazipata tena via misaada?
 
Tanzania hatukuwa na maandalizi ya kujitegemea tulilemazwa sana na misaada ya hawa Jamaa wa MCC, kujitegemea Ni processes hatuwezi kulala na kuamka tukiwa tumejitegemea kwa one night.Tukubali wanavyotaka kwanza ili tuanze hizi processes za kujitegemea bila kuathili Maisha ya kila cku kwa RAIA.Naamini ndani ya miaka 15 tutakuwa katika mazingira mazuri ya kujitegemea kama taifa.
Point....
 
Kwanza nianze na kukupa pole na majukumu uliyonayo ya kuongoza nchi! Wakati huu ni muafaka kukaa chini na familia yako yaani watanzania kwa makundi yao na kutafakari na kuomba kuungwa mkono katika hatua utakazozichukua ili kurejesha heshima ya uchumi wa nchi yetu! Tumia wasomi mbalimbali,kusanya maoni kwa wananchi kwa muda takribani mwezi hivi, tumia baraza lako la mawaziri kama washauri wako na ikiwezekana angalau international consultants wawili au watatu kwa ujumla wake wakushauri jinsi ya kuongeza mapato na kukidhi mapungufu ya bajeti yetu!

Usiogope! Wananchi wanakuelewa na ninaamini tutakuunga mkono! Msingi huu utakaoujenga ni kwa taifa letu na hautafutika kirahisi kama baba wa taifa alivofanya! Msingi wa kujitegemea katika kazi na utatuzi wa changamoto zetu! Nyumba bora haiendeshi maisha kwa kutegemea makombo ya jirani! Ukifanya hivi hao wanaokukimbia sasa watakutafuta wenyewe tu!
Ahsante
 
Inamaana watanzania wengine wanaona ni sawa demokrasia kupokwa?

Wahisani wameliona hilo. Watanzania wanaojitambua wameliona hilo. Wamebaki wagonjwa hospitali ya milembe ndo bado kuliona hilo.
 
Kwanza nianze na kukupa pole na majukumu uliyonayo ya kuongoza nchi! Wakati huu ni muafaka kukaa chini na familia yako yaani watanzania kwa makundi yao na kutafakari na kuomba kuungwa mkono katika hatua utakazozichukua ili kurejesha heshima ya uchumi wa nchi yetu! Tumia wasomi mbalimbali,kusanya maoni kwa wananchi kwa muda takribani mwezi hivi, tumia baraza lako la mawaziri kama washauri wako na ikiwezekana angalau international consultants wawili au watatu kwa ujumla wake wakushauri jinsi ya kuongeza mapato na kukidhi mapungufu ya bajeti yetu! Usiogope! Wananchi wanakuelewa na ninaamini tutakuunga mkono! Msingi huu utakaoujenga ni kwa taifa letu na hautafutika kirahisi kama baba wa taifa alivofanya! Msingi wa kujitegemea katika kazi na utatuzi wa changamoto zetu! Nyumba bora haiendeshi maisha kwa kutegemea makombo ya jirani! Ukifanya hivi hao wanaokukimbia sasa watakutafuta wenyewe tu!
Ahsante
Hana haja ya kutafuta consultancy wala nini... atekeleze wazo lake la kuwakusanya vijana wote wasio na kazi awapeleke JKT wakalime na kufuga, baada ya miezi sita tutakuwa tunalisha Afrika na Asia yote. Tatizo ni kuongea bila kutekeleza.
 
Inamaana watanzania wengine wanaona ni sawa demokrasia kupokwa?

Wahisani wameliona hilo. Watanzania wanaojitambua wameliona hilo. Wamebaki wagonjwa hospitali ya milembe ndo bado kuliona hilo.
Demokrasia bongo...?
 
Kaka democracy unayoisema, hao wanaoihubiri hawaitendi.
Angalia Saudi Arabia, Libya, Iraq waliambiwa kwao hakuna democracy.
Sasa wapo huru democracy inatawala.
Chezea mzungu wewe! Kwenye maslahi?
No enemy, no permanent friends.
Pesa kwanza.
 
Inamaana watanzania wengine wanaona ni sawa demokrasia kupokwa?

Wahisani wameliona hilo. Watanzania wanaojitambua wameliona hilo. Wamebaki wagonjwa hospitali ya milembe ndo bado kuliona hilo.
Demokrasia au domokrasia! Demokrasia lini ilimshibisha mwanakijiji, demokrasia inaliwa?! Tulishaaswa wahisani sio wajomba zetu! Mhisani mzungu akusaidie wewe ngozi nyeusi bila kunufaika yeye kweli? Kwanza tunakosea sana kuwaita wahisani. Wanatuhisani wakati tangu enzi wao ndio tunawafanyia hisani ya kuwapa madini na rasilimali zetu zinginezo bureee!
 
Mwaka we
Demokrasia au domokrasia! Demokrasia lini ilimshibisha mwanakijiji, demokrasia inaliwa?! Tulishaaswa wahisani sio wajomba zetu! Mhisani mzungu akusaidie wewe ngozi nyeusi bila kunufaika yeye kweli? Kwanza tunakosea sana kuwaita wahisani. Wanatuhisani wakati tangu enzi wao ndio tunawafanyia hisani ya kuwapa madini na rasilimali zetu zinginezo bureee!
mwaka wetu huuu wabongo chezea Jecha wewe na ccm Zanzibar tuombe mungu wasije kutunyima mafuta hivi sasa tunasaidiwa na mpaka panadol tunanunua madukani dah mungu wangu wanyonge tutaumia wala sio viongozi wao watakwenda Haidrabad au Apolo Cheinai
 
watanzani hebu tuache kudanganyana kwa kudhani rais wetu atafanya miujiza ili hali zetu za maisha ziboreke.tusijipe matumaini yasiyowezekana kuwa eti tutaweza kujitegemea bila misaada ya wafadhili. tizameni pato la taifa letu pamoja na deni kubwa tunalodaiwa na hao hao wafadhili.kwa sasa hata tujitahidi kukusanya kila senti ya kodi hatuna uzalishaji mkubwa wa viwanda ambao utatuwezesha kukusanya kodi na pesa za kigeni za kutosha.

Juu ya hayo ifahamike kuwa wafadhili mabepari hawataki nchi inayoonyesha dalili ya ujamaa.kwao mjamaa ni adui namba moja.angalia urusi pamoja na ubabe wao walivyolazimika kudanya mageuzi kwa mbinyo wa mabepari. huku kutunyima misaada ni baada ya kuona mwelekeo wa JPM wa kutaka kuleta usawa kwa watu wote.kwenye mfumo wa ubepari lazima pawe na tajiri sana na masikini sana.

na sisi jeuri ya kiuchumi ya kupambana nao kwa sasa hatuna.kuna msemo wa kiingereza unaotafsirika kuwa: "kama huwezi kupambana nao,jiunge nao".wenzetu kenya walijiunga nao zamani.wametuacha kwa mbaali!
 
Ukiangalia mzizi wa tatizo JPM sio chanzo cha mgogoro yamemfika tu! Walioyapika haya ni mfumo sasa tutatue tatizo lililopo kwanza! Kwenda kujipendekeza kwao tena kuanza kulia njaa haiwezekani! Tanzania mpya inayojengwa sio lzm wore tuliopo tufaidi itachukua muda lkn watoto wetu watanifaika!
 
Mh. Rais akisoma maoni ya wananchi yalikusanywa na Tume ya Jaji Warioba nafikiri hatahitaji wataalam toka nje kwa ushauri! Wananchi tulisha shauri karibu yote kupitia Rasimu ya Warioba.
 
Back
Top Bottom