Rais Magufuli anasema hivi kuhusu misaada

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,262
"Wale wanaojitokeza kutupa misaada, nataka niwahakikishie ile misaada ni ya masharti. Unaweza ukapewa masharti kwamba usikohoe na kikohozi kinakujaga tu. Kwa hiyo ni lazima watanzania tujisimamie sisi wenyewe. Na tukisimama sisi wenyewe, Tanzania hii tutavuka. Tanzania hii tuna kila kitu, Tanzania ni matajiri lakini utajiri tumeukalia"
 
Safi sana, lakini tungependa atupe mchanganuo wapi tutazipata hizi fedha tofauti na kodi pekee,
Ni wakati wako sasa kufufua fikira ulizoua za kujitegemea. Fikiria namna ya kuifanya Tanzania nchi inayojitegemea kiasi cha kufikia kutoa misaada kwa nchi nyingine. Kama unaona uwezi kukaa katika Tanzania inayojitegemea anza sasa utaratibu wa kuukana uraia wa Tanzania na kutafuta uraia wa nchi nyingine itakayokidhi matakwa yako. Kwa nini unataka kila kitu ufanyiwe, yaani hata kufikiri unahitaji msaada...!!? Mnaaza kunifanya niandike kwa ukali kwenye jukwaa hili. TUJITEGEMEE muda ndiyo huu.
 
Jamani tumuhurumie raisi wetu, hapo alipo ana mawazo, MCC wamekata mirija, Nchi 10 kati ya 14 zinazochangia budget wamesepa,Bandarini kumezorota, Wafanyabiashara hawaagizi kama kawaida, mapato ya ndani yanaendelea kupungua, kila kinachokusanya kinatumika, Mataifa rafiki hayamuelewi! walimu 50,000 wanatakiwa kuajiriwa, bado pesa za elimu bure ni janga jengine, hata za Mock hamna! nadhani anafikiria kuirudisha kodi ya kichwa sasa
 
Yupo sawasawa Rais
Lakini hawa walio ishiwa hoja yakupatia Kick wanadhani MCC imewatoa kimasomaso
Poleni sana
Halafu mtu anakuja anasema na bado, wengine wazuie misaada yao kwa TZ hivi ana akili huyu? Kumbe mafanikio ya nchi ni ya Magufuli tu? Hovyo kabisa....sikuamini kumuangalia akiongea....
 
"Wale wanaojitokeza kutupa misaada, nataka niwahakikishie ile misaada ni ya masharti. Unaweza ukapewa masharti kwamba usikohoe na kikohozi kinakujaga tu. Kwa hiyo ni lazima watanzania tujisimamie sisi wenyewe. Na tukisimama sisi wenyewe, Tanzania hii tutavuka. Tanzania hii tuna kila kitu, Tanzania ni matajiri lakini utajiri tumeukalia"
Sawa Mheshiwa RAIS, lakini hilo suala ni la long term plan, sio la muda mfupi kiivyo, just take it slow this is process , we cant win overnight, mheshimiwa
 
Jamani tumuhurumie raisi wetu, hapo alipo ana mawazo, MCC wamekata mirija, Nchi 10 kati ya 14 zinazochangia budget wamesepa,Bandarini kumezorota, Wafanyabiashara hawaagizi kama kawaida, mapato ya ndani yanaendelea kupungua, kila kinachokusanya kinatumika, Mataifa rafiki hayamuelewi! walimu 50,000 wanatakiwa kuajiriwa, bado pesa za elimu bure ni janga jengine, hata za Mock hamna! nadhani anafikiria kuirudisha kodi ya kichwa sasa
Hivi unafikiri toka tupate uhuru mwaka 1961, tulikuwa tunategemea misaada ya MCC? Sasa hamna muda wa kubet, eti MCC watakuletea pesa. Kilichobaki ni kufanya kazi na kujitegemea!
 
Haya,tunajitegemea!cha msingi mishahara iendelee kufika kwa wakati,walimu waliomaliza toka mwaka jana wapatiwe ajira,maness pia toka mwaka jana post hazijatoka,bei ya bidhaa kama sukari ishuke,hapa kazi tu.
 
tusubirie mapato ya mwezi huu tuona kama tutabaki na hela ya maendeleo,kama haitobaki inabidi tuwarudie hawa wazungu tu haina budi.
 
Hapo najua anawaza tu kichwani mwake ningejuaga nisichukue form ya uraisi leo ningekuwa waziri tu maisha yanaendelea, uongozi ni mzigo tena kama hujajipanga ni tabu tupu miezi sita tu mzee kaomba likizo kaenda Chato magu komaa babaaaa
 
Nakubaliana na mantiki ya Rais kuhusu umuhimu wa nchi yetu kujitegemea. Ila suala hili lilitakiwa kupangiwa mkakati wa muda mrefu kidogo siyo hii ya kushtukizwa na wafadhili wanaokatwa misaada yao halafu tunaanza kuongelea kujitegemea bila kueleza tunafidia vipi mapengo yanayoachwa na fedha za wafadhili zinazoondoka.
 
"Wale wanaojitokeza kutupa misaada, nataka niwahakikishie ile misaada ni ya masharti. Unaweza ukapewa masharti kwamba usikohoe na kikohozi kinakujaga tu. Kwa hiyo ni lazima watanzania tujisimamie sisi wenyewe. Na tukisimama sisi wenyewe, Tanzania hii tutavuka. Tanzania hii tuna kila kitu, Tanzania ni matajiri lakini utajiri tumeukalia"

Tunajisimamamia katika dhuluma. Hapo hakuna masharti.
Tunajidanganya hatuvuki
Nakumbuka maneno aliyowaambia viongozi wenzeke kuhusu unyanyasaji wa demokrasia
 
Tatizo la watanzania wengi tunawaza kitumwatumwa, watu wanadai tutaishije bila msaada, huo ni utumwa
 
Back
Top Bottom