Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,685
- 6,689
Sifa moja ya comedians wazuri ni kutumia maisha na changamoto za maisha kama chanzo kikuu cha vichekesho vyao. Lakini kuwa comedian bora kabisa unahitaji uwe tayari kujiangalia mwenyewe na mapungufu yako kama source ya comedic material zako. Hili ni jambo gumu sana kwa wengi lakini ndiyo linatofautisha comedian wa kawaida na wale wa viwango vya juu.
Comedians wengi wanatumia maisha ya wengine kama source ya material zao. Wengi wa Tanzania weakness yao ni hiyo. Wanatumia maisha ya wengine tu wakati ili uwe the very best comedian, inabidi ujiangalie wewe mwenyewe na uwe tayari kujicheka. Nakumbuka kulikuwa na Award show moja alihost Mpoki wa Ze Comedy, alifanya vizuri sana na nadhani ni standup bora kuwahi kufanyika Tanzania ila ukiiangalia alikuwa anawachamba wengine tu. Sikumbuki hata kama alisema kitu kinachomuhusu yeye mwenyewe.
Sasa tuje kwa Magufuli (kwa nia ya uzi huu, nitamuita tu kwa jina moja kwa nia ya kufupisha tu lakini siyo kwa nia ya kumvunjia heshima). Kauli zake nyingi na hata matendo yake kadhaa yana element ya kicomedy ila zimeonekana ni za utata na hata wakati mwingine kukera na kuchukiza baadhi ya watu. Hata akiwa anatania anatumia sauti ya ukali kiasi kwamba utani unapotea katika tafsiri.
Kitendo cha leo cha viongozi 6 wa CHADEMA kushindwa kufika mahakamani kwa sababu eti ya ukosefu wa usafiri ni episode nyingine kwenye Magufuli Show. Sina shaka Kisanduku wakati anawataarifu ukosefu wa usafiri alitoa ushauri kama inawezekana labda watembee kutoka Segerea mpaka Kisutu. Namuona kabisa Magufuli akitoa maagizo hayo, hiyo ndiyo style ya vichekesho vyake. By the way, ni jana tu nimetoka kuongelea kuhusu utaratibu usiofaa wa gari lililo wazi kusafirisha mahabusu.
Tukio la leo ni muendelezo wa kauli zinazofanana na tukio hili. Kule Zanzibar, alimwambia Rais Shein, atakubalije kulipia matibabu ya Maalim Seif wakati hataki hata kumpa mkono. Aliwahi kuwaambia Wakurugenzi asione mmoja wao anataja wapinzani wameshinda uchaguzi halafu wategemee mshahara kutoka kwake. Juzi kati ametoa kauli kwamba wafungwa hawatapewa hela na serikali inabidi walime chakula chao. Tukio la leo inaonyesha ana mtazamo pia kwamba serikali haiwezi kulipia gharama za mafuta za kuleta mahabusu mahakamani, tena ukizingatia mahabusu wenyewe ni wapinzani wake.
Mmoja wa comedians maarufu kuwahi kutokea Charlie Chaplin aliwahi kusema ‘My pain may be the reason for somebody's laugh. But my laugh must never be the reason for somebody's pain.’ Huyu ni mtu aliyekuwa anajua maana hasa ya comedy ndiyo maana mafanikio yake yamebaki ni historia. Comedy ni therapy nzuri sana kwa comedian mwenyewe na watazamaji/wasikilizaji ila ni budi mchekeshaji ajiangalie yeye badala ya kutumia matatizo ya wengine kama source ya vichekesho vyake. Usipofanya hivyo, hauwi tena comedian unakuwa sadist.