Rais Magufuli amtembelea Maalim Seif, Serena Hotel

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
12794580_10204530586825011_2746383943787031723_n.jpg
12801415_10204530587865037_2019982198199698893_n.jpg




===========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, amemtembelea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika holeti ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif yupo hotelini hapo kwa mapumziko baada ya kutolewa hospitali ya Hindu Mandal jana jioni alipokuwa amelazwa.

Maalim Seif amewahakikishia Watanzania kuwa afya yake inaendelea vizuri na kwamba anaendelea na shughuli zake na siku chache zijazo ana matumaini ya kurejea katika hali yake ya kawaida.
 
Wazanzibar na watanzania wa kawaida wakipewa ED wakitoka hospitali wanaenda kupumzika na kuugulia nyumbani huyu anapumzika na kuugulia na kunywa panadol hotel ya kitalii.

Halafu mnasema Seif Shariff HAMAD akishika ataboresha maisha ya wazanzibari.

Hapo SEif muungano anaupenda hata kama swala la mahoteli si jambo la muungano
 
JPM , sijakupa kura lakini sasa nakukubali.

Kiongozi mzuri daima huwa anaonesha njia. Moses aliwaongoza wana waisrael kutoka utumwani na kuwa peleka kwenye " promised land" sio kwa fimbo ya chuma lakinikwa maneno matamu na vitendo vya utu na uungwana.

Kwa hili na kupa tano. Kama kuna uchaguzi wa marudio kura yangu unayo!
 
Wazanzibar na watanzania wa kawaida wakipewa ED wakitoka hospitali wanaenda kupumzika na kuugulia nyumbani huyu anapumzika na kuugulia na kunywa panadol hotel ya kitalii.Halafu mnasema Seif Shariff HAMAD akishika ataboresha maisha ya wazanzibari.

Hapo SEif muungano anaupenda hata kama swala la mahoteli si jambo la muungano
Umeni furahisha sana. Hivi wewe ukuija Zanzibar hata kikazi na ukapata maradhi na kulazwa hospitali ukitoka utakwenda wapi kama si hoteli, au utakwenda kuishi kwa hawara yako mpaka upate nafuu?
 
Huyu Maalim Seif kazoea kuishi hotelini. Hajiamini. Hata Zanzibar hakai/kuishi. Kigeu geu sana, angalia yuko serikalini na huku nje anaiponda.
 
Umeni furahisha sana. Hivi wewe ukuija Zanzibar hata kikazi na ukapata maradhi na kulazwa hospitali ukitoka utakwenda wapi kama si hoteli, au utakwenda kuishi kwa hawara yako mpaka upate nafuu?

Kwa ndege kwenda zanzibar ni dakika 25.Baada ya kulazwa, alipopewa discharge alitakiwa kurudi kwao.Wangemtumia nauli hata ya boti SAA MOJA TU ANGEKUWA KAFIKA KWAO KWENYE NCHI YAKE.
 
JPM , sijakupa kura lakini sasa nakukubali. Kiongozi mzuri daima huwa anaonesha njia. Moses aliwaongoza wana waisrael kutoka utumwani na kuwa peleka kwenye " promised land" sio kwa fimbo ya chuma lakinikwa maneno matamu na vitendo vya utu na uungwana. Kwa hili na kupa tano. Kama kuna uchaguzi wa marudio kura yangu unayo!
Hata kama uchaguzi utasimamiwa na jecha?, mkuu acha utani bhana
 
Huyu babu anatutia hasara tu kwanza na yeye ana nafasi kubwa tu ya kuvuruga uchaguzi wa Zanzibar,
 
Back
Top Bottom