figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, leo amempigia simu Msanii wa Muziki wa kufokafoka aka Hip Hop ndugu Hamis Mwinjuma aka MwanaFalsafa aka MwanaFA aka Binamu, na kusema yeye ni mpenzi wa kazi zake haswa Wimbo wake unaotamba anga za Miziki wa [HASHTAG]#DumeSuruali[/HASHTAG] ambao alimshirikisha Vanessa Mdee. Moja ya ya Msitari anaoupenda ni "Utoe hela kwani ina TV ndani?"
"Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais Magufuli kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa [HASHTAG]#DumeSuruali[/HASHTAG]" amesema MwanaFA kwenye Ukurasa wake wa Twitter
Hapa chini nimewawekea Wimbo huo aliousifia kwa wale wasioujua
Hapa chini ni Mashairi ya Wimbo Dume Suruali wa Mwana FA
Msanii: MwanaFA Featuring Vanessa Mdee
Wimbo: DUME SURUALI
Intro
Wewe ni dume suruali
Kaa mbali nami mbali nami
Kama dume suruali
Kaa mbali nami uendani nami
Falsafaaaa
Verse 1
Who dat who dat hii ni salamu
Na ufahamu kama unauza mapenzi si kwa binamu
Huna haja ya kusubiri hii ni hukumu
Hakuna kitu utapata utangoja kama
Askari wa zamu
Dume suruali dume kaptura
Shauri zako ilimradi sipati hasara
Usione utani mimi siongei hata kwa ishara
Utaniambia nini mpaka unigeuze Fala
Kwanza naskia hongo zinaleta mkosi
Senti tano yangu hugusi hata ukiongea kidosi
Yabaki mapenzi tusileteani ujambazi
Hata upige sarakasi utachonga viazi
(Bahiri kama nini)
Ndo mnavyosema na
Ukiniomba kesho hunisikii teyna
Kwani unauza nini dada hunitakii mema
Chorus
Wewe ni dume suruali
Kaa mbali nami mbali nami aaah
Kama dume suruali
Kaa mbali nami uendani nami
I want that Gucci Fendi
Spend all on a girl like me
My name is Vee Money money
Spend all on a girl like me
Verse 2
Nionge nanunua nini kwanini yani
Kuna kipi nisichokijua ina TV ndani
Usiulize ntakupa nini dada
Piga moyo konde
Viuno vingi kama mwari wa kimakonde
Usipende ela kama mfuko
Au fanya unavyofanya upate zako
Vishawishi vingi binti sema na moyo wako
Na ujifunze pesa zinauza utu wako
Tajiri mtata kama Sallah
Zipo ila sitoi
Sio Bahiri mimi balaa
Unapenda ela zangu nami nazipenda pia
Kila mtu abaki na zake
Bye babe tutaongea
(Mwanaume wa hivyo wa nini sasa?)
Ndo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii teyna
Kwani unauza nini dada hunitakii mema
Chorus
Wewe ni dume suruali
Kaa mbali nami mbali nami aaah
Kama dume suruali
Kaa mbali nami uendani nami
I want that Gucci Fendi
Spend all on a girl like me
Money is Vee Money money
Spend all on a girl like me
Bridge
Aje aje mi mtoto flani ghari
Yeaah Nionge gari
My sweet sweet babe
Wanna see u today unipeleke Paris
Aje aje njoo nikupe TBT
Yeaaah
verse 3
Siyo kwa enzi ya magufuli
Zari lilikuwa long
Siku hizi hakuna la mentali
Nikikuonga na ukaniacha ntakujia
Usingizini Naepusha shari
Matatizo yote ya nini?
Hakuna kipya chini ya jua
Hata nsiyoyafanya nshayasikia
Ningekuwa muongaji ningeshafulia wangu
Mademu wangu wa zamani
Wote wangekuwa maadui zangu
(Mwanaume hovyo wewe)
Ndo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii teyna
Kwani unauza nini dada hunitakii mema
(Baki na hamu zako)
Chorus
Wewe ni dume suruali
Kaa mbali nami mbali nami aaah
Kama dume suruali
Kaa mbali nami uendani nami
I want that Gucci Fendi
Spend all on a girl like me
Money is Vee Money money
Spend all on a girl like me
Baba bure huyu
Hata Panton linastaafu
Unamwambia nani sasa
Unamwambia nani sasa