Rais Magufuli amenishangaza mara mbili juma hili

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Kwanza, amenishangaza kuteuwa Wabunge sita wanaume kati ya Wabunge kumi anaopaswa kuwateuwa kikatiba. Ilivyompasa ni kuteuwa angalau Wabunge wanaume watano na wanawake watano. Rais amenishangaza. Kuna hoja ya kuifanyia kazi hapa.

Pili, Rais Magufuli amenishangaza kwa kumuapisha Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania. Imekuwa ni mara yangu ya kwanza kushuhudia Kaimu akiapishwa-tena kwa kiapo kile kile cha 'mwenye-kiti' chake. Kaimu alipaswa kukaimu tu. Kiapo hakikutakiwa.

Washauri wa Rais wa mambo ya kisheria na ya kisiasa mko wapi? Tafadhali, tendeni kazi zenu kwa weledi, uhodari, umakini, bila awoga na bila ushawishi. Maamuzi ya Rais hayapaswi kuwa mjadala usio na tija. Washauri wajibikeni.

Mtangulizi wake ilikuwa hivi:Kikwete amenitukana....

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
 
Kuna walakini mkubwa kwa timu yetu ya utendaji pale Magogoni, why kila atendacho, akisemacho na anachoshauri bwana mkubwa kina kuwa na kasoro za kimaadili, kanuni au kisheria siku zote? Tunaona hata mfumo wa hotuba zake nao ni wa kuligawa taifa badala ya kuliunganisha.

Moja ya vipengele vigumu na vizito ndani ya katiba ni kile cha kumng'oa Rais katika wadhifa wake kama anavunja katiba aliyoapa kwa Mungu kuilinda na kuitetea.

Huu mtindo wa kuvunja katiba wakati wapo wataalamu wengi na wakila nyanja tunaowalipa vizuri wapo pale na yanatokea haya tueleweje? Jee ni kuwa hawafanyi kazi yao ipasavyo? Na kwa ni kwa bahati mbaya au makusudi? Na kama ni makusudi nia yao ni nini. Au hawana uwezo waondoke?

Au pengine kila washauricho hakifuatwi? Kwa nini sasa hawajiondoi ili kulinda weledi wao? Tumechoka ofisi yetu kuu kuonekana inafanya kazi kwa makosa kila uchao utazani ni ya mtendaji wa Kata
 
Kwanza, amenishangaza kuteuwa Wabunge sita wanaume kati ya Wabunge kumi anaopaswa kuwateuwa kikatiba. Ilivyompasa ni kuteua angalau Wabunge wanaume watano na wanawake watano. Rais amenishangaza. Kuna hoja ya kuifanyia kazi hapa.

Pili, Rais Magufuli amenishangaza kwa kumuapisha Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania. Imekuwa ni mara yangu ya kwanza kushuhudia Kaimu akiapishwa-tena kwa kiapo kile kile cha 'mwenye-kiti' chake. Kaimu alipaswa kukaimu tu. Kiapo hakikutakiwa.

Washauri wa Rais wa mambo ya kisheria na ya kisiasa mko wapi? Tafadhali, tendeni kazi zenu kwa weledi, uhodari, umakini, bila awoga na bila ushawishi. Maamuzi ya Rais hayapaswi kuwa mjadala usio na tija. Washauri wajibikeni.

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Ni kurahisisha kazi ya kumtumbua, Jaji mkuu ana security of tenure kikatiba, akishateuliwa akaapishwa hatenguliki mpk amalize muda wake astaafu, kwa mwendo huu dhana ya checks and balances (mihimili 3 ya serikali) iko matatani!
 
Kwanza, amenishangaza kuteuwa Wabunge sita wanaume kati ya Wabunge kumi anaopaswa kuwateuwa kikatiba. Ilivyompasa ni kuteua angalau Wabunge wanaume watano na wanawake watano. Rais amenishangaza. Kuna hoja ya kuifanyia kazi hapa.

Pili, Rais Magufuli amenishangaza kwa kumuapisha Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania. Imekuwa ni mara yangu ya kwanza kushuhudia Kaimu akiapishwa-tena kwa kiapo kile kile cha 'mwenye-kiti' chake. Kaimu alipaswa kukaimu tu. Kiapo hakikutakiwa.

Washauri wa Rais wa mambo ya kisheria na ya kisiasa mko wapi? Tafadhali, tendeni kazi zenu kwa weledi, uhodari, umakini, bila awoga na bila ushawishi. Maamuzi ya Rais hayapaswi kuwa mjadala usio na tija. Washauri wajibikeni.

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)

Katiba inasema angalau wanawake watano. Wakiwa zaidi ni sawa lakini wanaume hawawezi kuwa zaidi ya watano
 
Back
Top Bottom