Rais Magufuli amdhalilisha Meya wa UKAWA Manispaa ya Ilala

Rais Magufuli amdhalilisha Meya wa UKAWA Manispaa ya Ilala

Baadae alimkaribisha Raisi aliyekuja na kituko cha mwaka. Aliendelea kutambulisha mabalozi na wawekezaji, mkewe, mbunge Zungu (Ilala), mbunge Kessy (Nkasi Kaskazini) akamruka Anatropia wa CDM, akamwita mbele mbunge Bona na kumsifia sana akisema kwamba wananchi wa Segerea walifanya vizuri kuchagua mbunge wa ccm kama na yeye alivyo wa ccm na kwamba kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwa sababu ati hawezi kumpa mtoto wa jirani chakula wakati wakwake yupo!
Kimsingi kwenye uchaguzi wa mbunge wa ccm katika jimbo la Segerea ni busara tu inaweza kutumika katika kuwasaidia wanaobeza upinzani kunyamaza. Wananchi ndio waliopiga kura na kura za upinzani (Mtatiro na Antropia) zilikuwa nyingi kuzidi za huyu mbunge. Kumbuka karibia madiwani wote jimboni kwake ni wa upinzani pia kitu kinachoonyesha wazi kuwa chaguo la wananchi lilizidiwa na 'technical fouls'. Kwa mkuu wa nchi kutolielewa hili ni kupotoka!
 
Haya ni mambo ya ajabu mno. Kwanini umdhalilishe kiongozi ambaye ameweka na wananchi kama wewe ulivyowekwa? Hii ni dhahiri sasa kuwa upinzani unapaswa kuwa na msimamo mkali dhidi ya udiktator huu vinginevyo wananchi watakata tamaa.

Alivyokuwa anaomba kura alisema kuwa ni rais wa watu wote lakini ni dhahiri sasa ni wa ccm
 
umeonaeeeeee yanni phd zakuungaunga amejaa visasi na unafiki et mniombeeee nyooooooooooo naubaguzi huo uliomjaaa
Unafiki mtupu sisi tumuombee vipi wakati ana ulinzi tunataka actions na maendeleo. Sasa tukisali ndo maisha yatapungua ugumu.unafiki wa viongozi wa kisiasa tu wanazungumza wasiyo ya tenda
 
Kwa Hali hii ya Kiongozi kuweka itikadi za chama chake mbele Na sio taifa ni mbaya sana jua watanzania wanakupima kwa kila unachokifanya Na sifa ya Kiongozi ubomolewa Na kitu kidogo sana usichokizania kulewa madaraka ni kitu kibaya sana katika uongozi jua upinzani ndio utakaopima uongozi wako kwa wananchi ukitaka kujua baya lako mpaka atakapopata atakaye kukosowa
mulivyokuwa munaimba maalim saif pale bungeni ilikuwa poa?
 
Akili yako inakutuma dawa ya moto ni moto siyo!
Je hapo meya kosa lake lilikuwa nini?
Je kauli za Magufuli za kuwatumikia watanzania wote amezifuta lini?

Je kiongozi mzuri ni yule anayefanya malipizi?

Hopeless moving figure
ttz rafiki hua hatutafakari kiuhalisia au tunakua wabinafsi au tunafikiri kuwa makosa yetu wengine watatuelewa as if raisi ni malaika. ni binaadamu kama sisi nae anapenda kusifiwa,kutambuliwa alichofanya then ndio kumkosoa. kosa la meya na chama chake ni kutoyafanya hayo ikiwemo pia kutomtambua rasmi,kumbuka wao wanasema waliibiwa nk nk na wana/waliyafanya hayo kwa umoja wa kichama.
 
Donald Trump.yupo.sahihi.sana kumbe kuhusu viongozi wa africa?
 
Kama rais kafanya hivyo basi ameonyesha udhaifu,matusi na dharau kubwa kwa demokrasia nchini,tena ni ushamba na ulevi wa madaraka.Mimi nashangaa kwa mtu aneyoneka kupewa support kubwa na umma kuwa na inferiority complex na kuubenza upinzani ni jambo la kushangaza sana.Unadharau wapinzani wakati hayo majipu anayotumbua yamejulikana kupitia kelele za wapinzani kila kona ya nchi
 
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA ALIVYODHALILISHWA NA SERIKALI YA MAGUFULI

Makamanda pipozzzzz! Jana nilipokea mwaliko wa maneno kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kupitia kwa Mkurugenzi wangu Manispaa ya Ilala wakinitaka niungane nao leo (jana) kwenye ziara ya Raisi Kinýerezi kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo kipya cha kufua umeme wa gesi na mvuke 240 MW (Kinyerezi II), mradi unaotarajiwa kukamilika 2018.

Nilipofika nilipokelewa na kiongozi mmoja wa protocal ambaye ananifahamu kwa kuwa tulikuwa tunasali pamoja zamani akanikabidhi kwa public relation manager wa Tanesco ambaye pia ananifahamu tangu akiwa mwandishi wa habari na mimi nikiwa mwanaharakati wa kupinga wawekezaji wa TTCL.

Kama Meya nilipangiwa kukaa jukwaa kuu la Raisi kati ya matatu ambayo mengine yalikaliwa na waheshimiwa wabunge na wawekezaji, lingine likikaliwa na wakurugenzi na viongozi wengine.

Sasa kituko kikaanza, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco akaanza kutambulisha watu walio ktk jukwaa kuu akataja karibu wote pamoja na mbunge Bona aliyekaa pamoja na mimi kwa heshima ya mbunge mwenyeji akaniruka mimi japokuwa alikwishaambiwa uwepo wangu!

Baadae alimkaribisha Raisi aliyekuja na kituko cha mwaka. Aliendelea kutambulisha mabalozi na wawekezaji, mkewe, mbunge Zungu (Ilala), mbunge Kessy (Nkasi Kaskazini) akamruka Anatropia wa CDM, akamwita mbele mbunge Bona na kumsifia sana akisema kwamba wananchi wa Segerea walifanya vizuri kuchagua mbunge wa ccm kama na yeye alivyo wa ccm na kwamba kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwa sababu ati hawezi kumpa mtoto wa jirani chakula wakati wakwake yupo!

Kama hiyo haikutosha akampa nafasi ya kusalimia wananchi! Haikuishia hapo akasema amemchagua mkuu wa mkoa Makonda kwa vile ni mchapakazi na kwamba wengine walikuwa wakigombana naye na kujidai kukataa fedha za maendeleo sasa yeye kampa ukuu wa mkoa awe bosi wao sasa aone kitakachoendelea!

Kauli hii iliniacha hoi. Kama vile haitoshi akasema tena kwamba amemteua mchapakazi mwingine ambaye wasiopenda maendeleo wanampinga Mh. Muhongo. Ati naye atawakomesha wale waliokuwa wanapenda kukodishakodisha mitambo ya kufua umeme. Ati anampongeza kwa kuvunja bodi iliyokuwa inamshauri kukodishakodisha mitambo ya ajabuajabu.

Yote hiyo ni mipasho kwa wapinzani ambayo haikutakiwa kutoka kwenye kinywa cha Raisi. Ile ilikuwa ziara ya kiserikali siyo ya chama chake. Na madongo mengine mengi kawarushia wapinzani utafikiri akina mama wanaocharurana kwa mafumbo.

Nimejuta kwenda huko na sitakaa niende tena kwenye ziara zake kwani huko ni kufuata maudhi badala ya kufurahia maendeleo ambayo ndiyo lengo la UKAWA.
Ujinga muliuanzisha wenyewe kwa kumzomea bungeni, sasa maalim anakula bata serena hotel nyie munaanza kuzodoana, nayule mama muliyemkwida blauzi pale karimjee muliona poa tu. Badala ya kwenda pemba kuhakikisha maalim anakuwa rais munaenda kwenye minuso isiyowahusu.
 
Mwita wewe ni ndugu yangu lakini ni pumbavu uliyetukuka. Jana nilikuwepo hapo kinyerezi katika msafara wa Rais. Kwa nini unapotosha umma hivi!!!!!????? Mbona sisi watu wa mara hatuna tabia hizi za kishenzi Mwita!!!!!! Huyo Meya wa Ilala ulitaka Mh Rais ampakate ili kutambua uwepo wake!? Mbona ITIFAKI ilizingatiwa sana jana.
Mkuu kuna maneno tata katamka rais me nimeona kupitia itv so bado ninawalakini na Magufuli
 
Si huwa mnasema humu wana ccm wanaisoma namba kwa Magufuli.
 
Kwanza lugha aliyotumia Rais inaonyesha tabia chafu za uchoyo na zinamchora kwamba hana utu. Pia ni mzazi mbaya.Unatumiaje kauli kuwa siwezi kumpa chakula mtoto wa jirani wakati wangu yupo?Anajionyesha alivyo kuanzia background yake na tatizo kubwa katika social cohesion.

Halafu si alisema atakuwa Rais wa Wote?Si anasema ni msema kweli kwa hiyo ni mpenzi wa Mungu?

Mungu yupi wa wabaguzi na wachoyo?

Halafu anahitaji kusaidiwa sana katika suala la PR na Diplomasia

Uongozi wa aina hii ni Disaster !
 
Tatizo viongozi wengine wanapenda umaarufu mno sasa kukosa chance kama hiyo ya utambulisho hilo linamuuma mno, kama unataka umaarufu wenye heshima kashirikiane na wanachi wako waliokuweka katika hiyo nafasi kwa kuwaletea maendeleo. hata nyie mna katabia kakutokuheshimu viongozi wa serikali ambao wameteuliwa na Maraisi kwa sabab ya siasa zenu za chuki mpaka mnafikia kupelekana Mahakamani, Mbunge kumtolea maneno mbovu mbovu mkuu wa wilaya mbele ya wananchi hakuwa sawa, sasa nyie mnadharau viongozi wakuu au watu walioteuliwa na viongozi wakuu halaf nyinyi mnataka muheshimiwe, HALAFU NYINYI MLITOKA BUNGENI KUSEMA HAMUMTAMBUI RAIS NI LOWASA, NA YULE NI RAIS WA CCM?
no matter what asmaa, hekima ya rais inatakiwa ionekane popote pale.
upinzani hata wafanye kosa gani itakuwa ni too low for him to sink into their level. as for Mr president he should not sink into that level.

hata kama ukawa walitoka nje kwamba hawamtambui yeye kama rais, leo hii he cant just go in front of citizen and confess that "chakula cha mbwa siwez kutupia mbwa",
hii inamaanisha nini? je does it mean wapinzani ndio mbwa?
hivi tukikaa na kuchunguza kwa umakin among majimbo ya upinzani hakuna kura alizopata yeye kama yeye? hata kama ni moja tu? je atamjuaje huyo mmoja aliyempigia kura? kwann asiwe fair tu?

nadhan asingesema lolote lenye kubeba taswira mbaya kama hili kusingekuwa na kumlaumu hapa, ila ninachokiona moyoni mwake amebeba chuki, na vinyongo kwa wale ambao hawajampa kura.

jana nilisema na hata leo narudia tena wale wanaotoka kule uso wa dunia unapoinukia wanaisoma namba this time.
 
Back
Top Bottom