figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 27,910
- 63,599
Kufuatia ajali ya meli ya MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Sep 2018, Rais Magufuli aivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ili kupisha uchunguzi wa kamati na vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza ajali hiyo.
====
Kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 katika ziwa Victoria, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri imevunjwa kuanzia tarehe 23 Septemba, 2018 wakati kamati ya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa ajali hiyo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Septemba, 2018