Rais Magufuli afuta sherehe za maazimisho ya siku ya UKIMWI, fedha zinunue dawa...

Daaah! Dkt Magufuli unatupa raha huku mitaani. Jina lako linatajwa kila sekunde. Wananchi wanazidi kukupenda mhe rais. Hakika tumeokota dodo kwenye mbuyu kukupata wewe kama rais wetu.

Kumbukumbu zangu zinaniambia kwaka jana kiasi cha Bilioni 3 kilitumika kuazimisha siku ya UKIMWI. Sasa sijui mwaka huu walipanga kutupiga kiasi gani? Pesa ya mlipa kodi ilikuwa inafanyia mambo ya kipuuzi tu.

Pia nakumbuka wakati wa kampeni uliahidi kufuta maazimisho yote ikiwemo ya maji? mbio za mwenge nk Futa mhe rais...wananchi tupo nyuma yako.
Mkuu hivi vitu vilitakiwa kufanywa zaidi ya miaka 20 ilopita pro ccm mlipinga sana selekali kupunguza matumizi yasiyo ya Lazima na yale ya anasa. Kwakweli mnatuchelewesha kupiga hatua.
 
Tusishangilie kila kitu,
Tujiulize siku hiyo inatumika kushereheka??
Ninavyojua siku kama hizo zinakua maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanachi na kupeana lipot peupe achana na ripot za maofcn!!

Ningedhan angangazia gharama zinazotumika kama ni kubwa zipunguzwe!! Kwan sherehe ya wabunge ilifutwa?
Ilikuwepo ila wakanywa maji kula kila mtu kwake!!!!
 
Rais anaendelea kuchukua maamuzi ya busara mosi, ya Value for Money.Pili naamini ni kutaka serikali ijitegemee na huo ndiyo mwanzo tu. Angekuwa kiongozi mzembe anapoambiwa serikali haina hela halafu akalengeshewa "matajiri" na kuambiwa "ndiyo wanaoisaidia serikali kuishi" ndiyo mwisho atakuwa hana sauti tena. lakini huyu anataka watu wajifunze na kujizoeza kujitegemea na hapo ndipo uadilifu unapomea vizuri. Hizi sherehe zinazokula pesa nyingi kwa manufaa kidogo hazitufai maana ni kuendekeza ujinga kusema eti ndiyo siku ya kuelimisha watu kuhusu ukimwi!.
 
ni sawa kabisa! nchi hii ilijaa uswahiliswahili mwingi!, watu walikuwa kama wakongo kwa starehe. Pia hizi nyingine hazikuwa ni sherehe wala maadhimisho, zilikuwa deal za watu. Tufanye kazi. tuache vya bure bure!
 
Acha uongo wako hapa! leo nilikuwa singida,maadhimisho hayo yamefanyika viwanja vya peoples.Labda ungesema Magufuli ameshindwa kuhudhuria.Ila chakushangaza walijaza tu wanafunzi wa sekondari.
Disemba moja imeshafikq huko SINGIDA
 
But,hizo hela labda ziwe ni za serikal pekee,endapo wafadhili like Global Fund wana mkono wao italeta shida kidogo,any way ni maamuz murua kwangu
 
Ni bonge ya Raisi kuwahi kutokea Afrika miaka ya karibini.Hakuna kiongozi kama yeye Afrika mashariki na kati.Watatypenda nchi za Afrika,chezea MWALIMU lazima awe mkali.
 
Hii siku ni muhimu kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu ukimwi... ukitoa elimu utakuwa umeokoa maisha ya watu wengi kuliko kuwapelekea dawa!

Asasi za kijamii na Taasisi binafsi zinaweza kufanya hizo sherehe kama zinavyofanya miaka yote. Serikali inaweza Toa elimu Yenye kufikia watu wengi zaidi kwa Tv na Radio Nchi nzima.
 
Rungu nimecheka hadi mbavu zinauma, MaCCM wanaisoma namba!!
Jamaa anapiga makufuli kila kona, bado mwenge, utapelekwa makumbusho!!
Mhs anafanya kazi!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom