Rais Magufuli afuta sherehe za maazimisho ya siku ya UKIMWI, fedha zinunue dawa...

Acha uongo wako hapa! leo nilikuwa singida,maadhimisho hayo yamefanyika viwanja vya peoples.Labda ungesema Magufuli ameshindwa kuhudhuria.Ila chakushangaza walijaza tu wanafunzi wa sekondari.

zimefutwa, huelewi nini? Ufunguzi ndo ulifanyika, ile kilele chake Dec. mosi hakitaadhimishwa.
 
Acha uongo wako hapa! leo nilikuwa singida,maadhimisho hayo yamefanyika viwanja vya peoples.Labda ungesema Magufuli ameshindwa kuhudhuria.Ila chakushangaza walijaza tu wanafunzi wa sekondari.

Maadhimisho rasmi ni tarehe 1, Dec. ila maandalizi yalianza mapema kwa maonesho ya wiki moja
 
Siku ya ukimwi ni kwa ajili ya kutoa ushauri kuhusu ukimwi, haihusiani na sherehe,,kuifuta ni uzuzu wa hali ya juu

Hata mimi nashangaa. Hivi siku ya ukimwi duniani ni sherehe za ukimwi? Nadhani huyo mkulu anapaswa aelimishwe.
 
Huyu mtu anatakiwa atiwe governor na bunge au washauri wake (.. ila sidhan hata kama anashaurika). Hayo ni maadhimisho ya dunia/UN kwa ajili ya awareness, siyo SHEREHE.

Mkuu,

Kuongeza uelewa juu ya UKIMWI ni kazi endelevu ambayo inapaswa kufanywa na vyombo husika ikiwemo media. Kama hawafanyi hivyo, basi wawajibishwe- hasa taasisi husika za serikali. Hii pia inaweza kuhusu siku zingine ambazo huadhimishwa kila mwaka kwa gharama kubwa -badala ya kazi hiyo kufanyika kila siku na idara /wizara husika- mathalan wiki ya maji. Ila kuna masuala ambayo Jamii yetu inahitaji uhamasishaji zaidi -viwango vya uelewa bado viko chini sana na hivyo kuhitaji siku maalum-mathalan magonjwa ambayo hayajulikani vizuri nchini(Hepatitis A na B, magonjwa yatokanayo na ulaji mbaya na mtindo wa maisha nk)
 
Rais wa JMT Dkt. John Magufuli amefuta tukio la Maadjimisho ya UKIMWI siku ya tarehe 01.12.2015 ambayo kutaifa yalikuws yafanyike Mkoa wa Singida.

Je, nini maoni yako juu ya hili?
 
Rais alielewa tofauti ya 'maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani'
na 'sherehe za siku ya UKIMWI'?

Halafu kama bajeti ni miloni 20 ambayo ni kama mshahara na posho ya mbunge mmoja
ni kweli ttume save?

Jee hakuna umuhimu wa kuadhimisha siku hii?

je wahamasishaji wa kupiga vita ukimwi watumie siku ipi ?

Je kununua dawa ndio the best way ya kupiga vita UKIMWI?

Je maoni ya mashirika ya Afya ya kimataifa yanaendana na uamuzi wa Rais?

Je hatuwezi kubana matumizi bila ku interrupt maadhimisho?
 
Hata mimi nashangaa. Hivi siku ya ukimwi duniani ni sherehe za ukimwi? Nadhani huyo mkulu anapaswa aelimishwe.

Somo la Ukimwi limeingizwa hadi kwenye mitaala ya shule za msingi... hiyo elimu ya siku moja ya wapi?

All in all, vyama mbadala tuko miguu juu maana wanaCCM walokuwa na utitiri wa vibiashara uchwara wako hatarini. Walionzisha biashara za tshirt, kanga, vitenge, na kujikuta wanachezea fedha sasa WANAISOMA NAMBA!!
 
...siku ya ukimwi duniani ni tarehe 01 december kila mwaka, huko singida ni sayari gani?!
mbojo amejichanganya.
By the way mbojo kwa kikwetu ni fisimtu,eti zamani walikuwepo wataalamu huko singapore wanageuza watu kuwa fisi
 
ccm walituundia taifa la ajabu mno. yaani gonjwa baya lililoacha yatima bila msaada eti lina sherehe, inayotumia millions of money?
 
Kinachofutwa sio maadhimisho...Ni sherehe ambazo zinaambatana na matumizi makubwa sana ya fedha...Bajeti zake zinatisha...Watu wamekuwa wakizitumia sherehe hizi kuvuna mapesa kwenye zabuni za fulana...Kofia...Matangazo...Maandalizi n.k

Kipi bora...Kufanya sherehe za gharama kubwa ama kutumia fedha hizo kununua dawa...

Tunaweza kiadhimisha hata kwa Rais kuhutubia kupitia TV na Radio

Kwahiyo Mkuu hizo zabuni ulizozitaja hapo juu zilikua bado hazijafanyiwa kazi?
Sherehe zimesitishwa jana, siku 5 kabla je hizo Kofia, Khanga, T-shirt na Vipeperushi vilikua bado havijaandaliwa?
 
Nijuavyo ni kwamba, siku ya UKIMWI ni tarehe 1 December ila siku hiyo huwa inatanguliwa na maadhimisho ya wiki nzima ambapo huduma mbalimbali ikiwemo upimaji wa virusi hutolewa. Nimesoma magazeti ya leo, maadhimisho yamezinduliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Singida. Sasa kama, yameshazinduliwa, ninaamini kwamba kama watu wa tender za kupamba, mabanda, fulana, matangazo watakuwa ama wameshaingia mikataba au wamelipwa kiasi cha fedha. Pia, kuna watu wamesafiri toka maeneo mbalimbali kwenda Singida kwenye maadhimisho hayo. Hivyo, nafikikiri kwamba hii haitasaidia sana kubana matumizi ya fedha zilizopangwa kutumika kwenye maadhimisho hayo.
 
Kwahiyo Mkuu hizo zabuni ulizozitaja hapo juu zilikua bado hazijafanyiwa kazi?
Sherehe zimesitishwa jana, siku 5 kabla je hizo Kofia, Khanga, T-shirt na Vipeperushi vilikua bado havijaandaliwa?

Nimewaza pia hivi, inawezekana nusu au robo tatu ya bajeti imeshatumika.

Tofauti na hapo naona mh Rais anatoa ujumbe kwamba taifa lipo kwenye hali ambayo hatustahili kusherehekea kitu chochote hadi baadhi ya mambo ya msingi yakae sawa.
 
Labda wiki moja kabla nayo itafutwa na hela ambazo watu wangetumia kunywea bia na kangala zitatumika kuwanunulia nguo na kuwapikia pilau watoto yatima.

Nimeona tangazo la Katibu Mkuu Kiongozi amezuia uchapishaji wa kadi za Christmas kwa gharama za serikali.

Hapo lazima kuna watu wamepoteza 10%,

Probably serikali haina hela kugharamia hizo kitu,

Ingawa kwa kipindi cha jamaa yetu yule tungekopa ili tugharamie hizi kitu.
 
Back
Top Bottom