Rais Magufuli afanya ziara Ikulu, aonesha umahiri katika kushona

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,230
116,853
Nilikua natazama taarifa ya habari Azam Two nikaona taarifa yenye headline 'ziara ya Rais Magufuli Ikulu' nikamuona Rais ametembelea wanaoshona nguo hapo na yeye mwenyewe akishona kidogo....

But najaribu sana kuelewa 'Rais kufanya ziara ''Ikulu'' '

Nashindwa kabisa kuelewa....naomba kuelimishwa...

Rais si anaishi Ikulu?

Ziara Ikulu ni sahihi au Azam two wamekosea namna ya kuripoti, au kuna kitu sijaelewa?

=======

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016

1453315191165.jpg


1453315223157.jpg

 
Rais ana mambo mengi, na pale Ikulu ni Taasisi kuna kazi nyingi sana zinaendelea mle ndani, hivyo kutembelea ni sawa hasa ukizingatia Rais hapendi sana kwenda nje ya nchi bila mpango, mimi nawashauri huyu bwana tumuombee atasaidia sana hii nchi...
 
Ngoja waje,labda kwa vile ikulu ni taasisi kubwa. Kuna ikulu hata mikoani,huenda ametembelea moja ya ikulu za nje ya magogoni. Au picha zilikuwa za magogoni????
 
Hizo nguo wanashonewa watu gani?

Ni biashara ya nguo inafanywa na ikulu au.

Maana mimi nadhani nguo za wale wa ikulu wanaagiza toka nje.
 
Na kama amekuta mapungufu tunataraji atamsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Ikulu ....ambaye bila shaka ni Rais

Kulitafakari vizuri hili tujue Ikulu ina vitengo vingapi na wafanyakazi wangapi.

Mwenye taarifa hizo atujuze.
 
Hilo ni jambo la kawaida na ni sahihi kabisa! Hata ukiwa mkuu wa idara kuna wakati unaamua kutembelea vitengo mbalimbali vilivyo chini yako na kusikiliza kero zao!
 
Back
Top Bottom