Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza uwanja ndege wa JNIA, Dar. Akuta mashine mbovu...

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Leo tarehe 13.05.2016 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya kushtukiza katika uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) na kuiagiza wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kuondoa dosari iliyopo kwenye kitengo cha ukaguzi wa mizigo ya abiria.

CiWPOW5WsAAlYPZ.jpg

Ifuatayo ni taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania kuhusu ziara ya kushtukiza ya Rais Magufuli uwanja wa ndege wa JNIA.

===========================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulia meiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminol One) Jijini Dares salaam.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazo tofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli kuamua kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.

'Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili. Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege.

'Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu akiamua kuja na madawa yake ya kulevya, nikija na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya Tembo kwa kutumia ndege ndogondogo napita tu' Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam Mei 13,2016

CiWCJ69XIAE1ZOO.jpg
 
Ajenda Kuu ni Sukari.Sasa mtu anarudi Safari anapita hapo uwanjani anaamua kukagua inakuwa kwamba alifunga safari kutoka Uganda kushtukiza hapo JNA?

Tulishasema ndani ya miezi 6 alipaswa awe angalao ametengeneza chain of accountability hapaswi kuwa kila mahali .Hiyo kazi ya kukagua machine sio yake .

Mbona hajatumbua tena ?Inaelekea somo letu la utawala wa sheria limemuingia au pia alipokutana na Uhuru Kenyatta amejifunza kitu.Good for him.

Sawa sasa hebu basi kwa haraka turudi kwenye ajenda kuu ya Sukari na Lugumi sasa

Maana hiyo watoto wa mjini wanasema ni janja ya "Nirudi Vipi" maana mtu mzima ukikumbwa na aibu lazima ufanye matukio mengi ya kupotezea ili mradi uonekane unafanya vitu vingi

Kama ile ya kutoka pia Dodoma na kujifanya amesimamishwa huko Manyara na wananchi wakati ulikua ni mkutano ulioandaliwa uwanjani apate platform ya kujisafisha na kuvurumisha Lawama kwa wafanyabiashara kuwa wanamhujumu

Haya turudi kwenye ajenda kuu ya Sukari,hilo la JNA tayari Wizara itashughulikia.
 
Sasa ameanz kuelewa utawala wa sheria! Mbona hajamtimua Mkurugenzi wa Viwanja ndege na wakubwa wa ujenzi? Ina maana Waziri na Katibu Mkuu hawajui kuwa machine zile mbovu? Report wanapeleka wapi? Wamefanyaje hadi sasa miezi 2 machine mbovu?? Baada siku 3 zitakuwa nzima!!
 
Mm naona Magufuli asipunguze kasi ya kutumbua Majipu, hadi watu walalamike vipi, Oohoo afuati sheria. Hii nchi ilifikia kubaya sana. Itafikia wakati watakuelewa tu!! Sasa kama mtu hadi amefikia kiwango cha kumdanganya Rais wa nchi, hii ni dharau kweli kweli!!

Prof. Makame Mbarawa mtumbue huyo alie mdanganya Rais. Hapo wamekalia wizi wa mizigo ya abiria tu.
 
Ajenda Kuu ni Sukari.Sasa mtu anarudi Safari anapita hapo uwanjani anaamua kukagua inakuwa kwamba alifunga safari kutoka Uganda kushtukiza hapo JNA?

Tulishasema ndani ya miezi 6 alipaswa awe angalao ametengeneza chain of accountability hapaswi kuwa kila mahali .Hiyo kazi ya kukagua machine sio yake .

Mbona hajatumbua tena ?Inaelekea somo letu la utawala wa sheria limemuingia au pia alipokutana na Uhuru Kenyatta amejifunza kitu.Good for him.

Sawa sasa hebu basi kwa haraka turudi kwenye ajenda kuu ya Sukari sasa

Maana hiyo watoto wa mjini wanasema ni janja ya "Nirudi Vipi" maana mtu mzima ukikumbwa na aibu lazima ufanye matukio mengi ya kupotezea ili mradi uonekane unafanya vitu vingi

Kama ile ya kutoka pia Dodoma na kujifanya amesimamishwa huko Manyara na wananchi wakati ulikua ni mkutano ulioandaliwa uwanjani apate platform ya kujisafisha na kuvurumisha Lawama kwa wafanyabiashara kuwa wanamhujumu

Haya turudi kwenye ajenda kuu ya Sukari,hilo la JNA tayari Wizara itashughulikia.
Leo hujanishawishi kwa hoja wala kwa hisia. Kwahiyo kama angenda ni sukari basi Rais asifanya jambo lingine tu kwasababu agenda ya kwanza haijaisha? Kwahiyo wewe hutazungumzia jambo lingine lolote mpaka agenda ya sukari iishe?
 
Nilipita hapo mwaka juzi nikielekea Dodoma, mashine hizo zilikuwa mbovu! Ukaguzi ulikuwa unafanywa kwa kumwangalia mtu usoni!
 
Ajenda Kuu ni Sukari.Sasa mtu anarudi Safari anapita hapo uwanjani anaamua kukagua inakuwa kwamba alifunga safari kutoka Uganda kushtukiza hapo JNA?

Tulishasema ndani ya miezi 6 alipaswa awe angalao ametengeneza chain of accountability hapaswi kuwa kila mahali .Hiyo kazi ya kukagua machine sio yake .

Mbona hajatumbua tena ?Inaelekea somo letu la utawala wa sheria limemuingia au pia alipokutana na Uhuru Kenyatta amejifunza kitu.Good for him.

Sawa sasa hebu basi kwa haraka turudi kwenye ajenda kuu ya Sukari na Lugumi sasa

Maana hiyo watoto wa mjini wanasema ni janja ya "Nirudi Vipi" maana mtu mzima ukikumbwa na aibu lazima ufanye matukio mengi ya kupotezea ili mradi uonekane unafanya vitu vingi

Kama ile ya kutoka pia Dodoma na kujifanya amesimamishwa huko Manyara na wananchi wakati ulikua ni mkutano ulioandaliwa uwanjani apate platform ya kujisafisha na kuvurumisha Lawama kwa wafanyabiashara kuwa wanamhujumu

Haya turudi kwenye ajenda kuu ya Sukari,hilo la JNA tayari Wizara itashughulikia.
Mimi ni ukawa damu na naamini na wewe ni ukawa lakini sio kila kitu upinge. Yaani unataka Pombe asifanye chochote kwa sasa isipokuwa akae na issue ya sukari tu!!? Si sawa kabisa. Nchi sio sukari tu.
 
Back
Top Bottom