Rais Magufuli afanya Mazungumzo na Mjumbe Maalum kutoka Burundi, Ikulu Dar es Salaam

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Rais Dkt.Magufuli afanya mazungumzo na Ndugu Reverien Ndikuriyo Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Ikulu Jijini Dar.

=====================
2VVCV.JPG
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Ndugu Reverien Ndikuriyo Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 22.
,2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mheshimiwa Reverien Ndikuriyo Ikulu jijini Dar Es Salaam hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi na jitihada zinazochukuliwa na Tanzania ikiwa ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika Mashariki

Akiwasilisha ujumbe wa Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi kuhusu hali ya Burundi, Spika Ndikuriyo amesema Serikali ya Burundi ipo tayari kufanya mazungumzo na wadau wote wa siasa kuhusu hali ya Burundi na jitihada za kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo

Akitoa maelezo ya kikao hicho kwa niaba ya Rais Magufuli, Balozi Maiga amesema serikali ya Burundi imekubali usuluhishi unaofanywa na Rais wa Uganda Mh. Yoweri Kaguta Museveni kwa niaba ya Marais wa Jumuia ya Afrika Mashariki kutokana na kikao kilichofanyika Jijini Dar es salaam mwezi Julai mwaka huu na kwamba serikali ya Burundi iko tayari kushiriki katika mazungumzo hayo ya amani.

"Mheshimiwa Rais Magufuli amefanya mazungumzo na rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi mwishoni mwa wiki iliyopita ambaye amemuhakikishia Rais Magufuli utayari wake wa kushiriki katika mazungumzo hayo ya usuluhishi" Alisema Balozi Maiga .

Balozi Maiga ameongeza kuwa "nimeagizwa nilipeleke taarifa kwa mawaziri wa nchi za nje wa nchi jirani juu ya maandalizi ya mazungumzo hayo ambayo yataanza kule Uganda tarehe 28 mwezi Desemba na Waziri wa Ulinzi wa Uganda amekabidhiwa jukumu la kuratibu mazungumzo hayo"

Ameongeza kuwa suala jingine lililojitokeza katika mazungumzo hayo ni juu ya uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa Afrika kutaka kupeleka majeshi yake nchini Burundi baada ya siku tano jambo ambalo Bunge la Burundi limepinga.

Balozi Mahiga amesema Burundi imepinga maamuzi hayo kwa kuwa inaamini kuwa hakuna hali ama dalili za kutokea kwa mauaji ya kimbari kama ya Rwanda, na kwamba kwa sasa kuna utulivu nchini humo tofauti na wasiwasi wa Umoja wa Afrika, Jumuia za kimataifa hasa Umoja wa Ulaya, na kwa kiwango fulani Umoja wa Mataifa unaotoa msukumo wa kutaka kuyapeleka majeshi ya kulinda amani nchini Burundi.

"Wao kama Burundi wakiwa ni washirika wakubwa wa kulinda amani katika bara la Afrika wana wanajeshi 6000 nchini Somalia,wanajeshi 1000 Jamhuri ya Afrika ya Kati na dhamira yao katika kushiriki kuleta amani, wao watakuwa ni watu wa mwisho kuleta hali itakayosababisha hatari ya kutokea kwa mauaji yanayofanana na mauaji ya kimbari" amesisitiza Balozi Mahiga

Dkt. Maiga amesema kutokana na maelezo hayo, Rais Magufuli amependekeza kuwa serikali ya Burundi ifungue milango ya mazungumzo na kuwakaribisha Umoja wa nchi za Kiafrika kupeleka ujumbe wa aina yeyote ili kwa pamoja waweze kutathmini hali usalama ilivyo nchini Burundi badala ya kukataa pendekezo hilo moja kwa moja.

Aidha, Balozi Mahiga amesema, Rais Magufuli amemuagiza kwenda nchini Burundi kutazama, kujiridhisha na kutathmini hali halisi ilivyo hususani katika suala la amani hasa ulinzi na usalama wa raia katika jiji la Bujumbura na maeneo mengine ya nchi hiyo ili kufahamu sababu zinazowafanya warundi kukimbia nchi yao na kukimbilia nchi majirani ikiwemo Tanzania kama wakimbizi.

Ameongeza kuwa safari yake ya kwenda Burundi kwa kiasi kikubwa itasaidia katika kuendeleza mazungumzo yanayotarajia kufanyika huko Uganda.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es Salaam.

22 Desemba, 2015
 
Siku zote Tz ni champion wa usuluhishi,

Heko Magufuli - Nipe kazi hiyo kwa niaba ya Tanzania ili hawa jamaa zetu niwaweke pamoja
 
Rais wa JMT ni mkuu wa nchi mwenye nguvu kuliko marais wote wa EAC ni vyema na haki viongozi wenzake ambao ni wadogo kwa maana ya ukubwa wa nchi ni lazima wamfuate tena wanatakiwa kumpigia magoti na kumfuta viatu.

Chikwete aliporomosha hadhi ya Rais wa Tanzania katika kasi ya ajabu.We fikiria Rais anakwenda Jamaika kubembea.

Mbona Rais Wetu Yeye Hatoki Kwenda NJE?
 
Tz wanaweza kusuluhisha ya wenzao ya kwetu mbona magumu
Zanzibar vikao name hata mrejesho kwamba wamefanikiwa kipi na kukwama wapi hakuna.
 
Mwambie akamfikishie ujumbe bosi wake kuwa
JPM kasema haache kuzengua wananchi wake .
 
Atatoka muda wake ukifika

Kufanya nini na huku hajamaliza kazi ya kutumbua majipu, mwacheni ashughulikie matatizo ya wananchi bana, kwani hujui rais anatumia mabilioni kwa safari moja tu, si bora amtume waziri
 
Nilikuwa sijui kama Burundi imo katika JMT. Kumbe ni sawa na Zanzibar, katoka Seif wameingia wao! Kwa wale wanaokereketwa kumuona maalim Seif kaonana na Dr Magufuli, wanaombeza maalim kutaka Zanzibar huru.
 
Tumejionea kwenye mtandao burundi kunamwagika damu na kunawakimbizi kuja tanzania .viongozi wa burundi wanaona damu kama mafuta !
 
Kwnn wameshindwa kuzuia watu waliouwawa au hawakuwa binadamu? Hatua gani zitachukuliwa dhidi ya wauaji? Je Burundi haiwezi ishi bila huyo dikteta?
 
Back
Top Bottom