figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za taasisi 5 za Serikali baada ya wenyeviti waliokuwa wakiongoza bodi hizo kumaliza muda wao na wengine kuteuliwa katika nyadhifa nyingine.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
22 Oktoba, 2018
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Charles Anael Mkonyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mifupa (MOI). Prof. Mkonyi ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS).
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Mwamini Juma Malemi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Sophia Simba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Mwanza Kamata kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE). Dkt. Kamata amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Christopher Chiza ambaye amechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu.
- Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Maria Mashingo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo (TIB). Dkt. Mashingo amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Palamagamba Kabudi ambaye aliteuliwa kuwa Mbunge na baadaye kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
22 Oktoba, 2018