Alwatan Mabruki
Senior Member
- Sep 20, 2020
- 132
- 118
Mara baada ya nchi yetu kupata uhuru iliamua kufuatia mfumo wa siasa ya ujamaa na kujitegemea na ilipofika mwaka 1967 lilitangazwa Azimio la Arusha ambapo njia kuu zote za uchumi zilikuwa zinamilikiwa na kusimamiwa na dola ikiwemo mifumo rasmi ya masoko ya mazao. Mashirika mbali mbali yaliundwa ili kusimamia biashara ya mazao, kwa mfano, GAPEX ilihusika na uuzaji mazao nje ya nchi na biashara ya mazao ya ndani sehemu kubwa ilisimamiwa na kuendeshwa na vyama vya ushirika. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 mfumo wa uchumi duniani ulianza kubadilika. Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ulitekelezwa ili kuendana na dhana mpya ya soko huria. Hali hii kwa namna moja au nyingine iliathiri mfumo mzima wa masoko kwa bidhaa mbalimbali.
Kutokana na mabadiliko mengi katika nyanja za biashara yanayotokea duniani kote ikiwemo Tanzania, Serikali imekuwa ikifanya mapitio ya Sera na Sheria ili kuboresha mazingira ya biashara nchini. Serikali kwa kushirikiana na washirika wa Maendeleo kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania (MKUMBITA) imefanya maboresho kadhaa kwa kuangalia changamoto zilizokuwa kikwazo kwa kufanya biashara kwa ushindani na wakati huo huo kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutambua kuwa biashara ni kichocheo cha maendeleo ya viwanda na sekta nyingine za kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015 - 2020), Chama tawala kimeendelea kuisimamia Serikali na kuhakikisha sekta ya biashara inaendelea kuimarika na kutoa fursa za masoko kwa mazao na bidhaa na kuwaunganisha wananchi na masoko yenye upendeleo wa ushuru wa forodha kikanda na kimataifa.
Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ni kuboreshwa kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa katika masoko ya kikanda na kimataifa.
Mafanikio mengine yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa na huduma kwenye masoko ya kikanda yanayotoa fursa za upendeleo maalum (preferential market access) ambapo kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018 Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Pesa za Kitanzania milioni 662,492,000, bidhaa zilizouzwa zaidi ni pamoja na madini ya Tanzanite, Chai, Kahawa, Sigara, Dawa na Vifaa Tiba.
Pamoja na Kuimarisha mahusiano ya kibiashara na nchi za nje ikiwemo nchi za Ulaya mfano Uswisi ambapo mauzo ya Tanzania yaliongezeka kutoka Pesa za Kitanzania milioni 334,311,331.2 mwaka 2015 hadi milioni 591,491,000 mwaka 2018 na nchi za Asia kwa mfano India ambapo mauzo yameongezeka kutoka Pesa za Kitanzania milioni 44,631,312 mwaka 2015 hadi milioni 97,566,000 mwaka 2018.
Mbali na mafanikio hayo, kumekuwepo na changamoto kadhaa katika biashara, ikiwemo upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji na biashara, uzalishaji wa mazao na bidhaa usiokidhi mahitaji ya ubora unaotoa ushindani katika soko la ndani na nje, Ufahamu mdogo wa matumizi ya TEKNOHAMA, kukosekana kwa Nishati ya umeme ya uhakika na ya kutosheleza kuendesha mifumo, na uelewa mdogo wa wadau kuhusu sheria na kanuni zinazosimamia biashara.
Aidha, serikali inapaswa kutatua changamoto hizo kupitia Wizara pamoja na Taasisi zilizochini yake kwa kuendelea kubuni mikakati na mipango ya kutekeleza majukumu yake ili kuongeza mchango wa Sekta ya biashara na masoko katika pato la taifa. Pia Kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha biashara ya mtandao (e-commerce) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Kwa kweli nitakua mchoyo wa fadhila nisipo ishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari Dkt. Joseph Pombe Magufuli kwa kutambua umuhimu wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara, uchukuzi na mawasiliano kwa lengo la kuwezesha ujenzi wa uchumi imara unaojitegemea. Manufaa elekezi ni pamoja na kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na kuongezeka kwa matumizi ya fursa za kijiografia na mapato ya nchi kwa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi na wananchi kwa ujumla.