Rais Magufuli aagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini kuwa Halmashauri ya Mtama na Ofisi zake kuhamia Mtama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,877
Mbunge wa Mtama mh Nape amesema Rais Magufuli haangalii itikadi ya vyama ndio maana makao makuu ya halmashauri ya Lindi vijijini ameyapeleka Mtama inayoongozwa na diwani wa Chadema.

Hivyo Nape amewataka wanachadema wa Mtama kuiunga mkono CCM ambayo imewajali.

Chanzo:TBC

----
Rais Magufuli ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini kuitwa Halmashauri ya Mtama na Makao Mkuu ya Halmashauri hiyo ihamishiwe Mtama kutoka Mjini

Amesema ndani ya siku 15, Viongozi wa Halmashauri hiyo watoke Mjini na kuhamia Mtama na hiyo ndio italeta maendeleo kwani kama ni giza ndio watashughulikia umeme haraka

Aidha, amesema “Najua kulikuwa na mabishano, wapo wanaotaka Makao Makuu yaende Subi, wapo waliotaka yaende Mchinga, wapo waliotaka yaende Rondo, kila mmoja alitaka”

Amefafanua, “Kwa kuwa mimi ndio Rais, na mimi huwa napasua katikati kwa kufuata haki nimetoa maagizo, Manispaa ya Lindi itachukua eneo lake iliyokuwa nalo mpaka Mnazi Mmoja au Mingoyo na kuongezewa eneo la Mchinga.”
 
wapinzani wanaonekana kama wakimbizi ndani ya nchi,huyu no 1 siku anaapishwa aliapa kulinda na kutetea katiba ya nchi,kuwalinda watanzania wote bila kujali imani zao,itikadi zao,jinsi zao,now inaonekana aliapa kulinda wana ccm pekee,ndio maana ukimdhuru mtu aliyevaa nguo ya kijani elewa utakuwa kwenye tabu kubwa,kilichobaki kwa nchi yetu ni TIME tu ndio mwokozi na atakuja kuokoa huu ukandamizaji kisa kutofautiana kiitikadi!!.
 
Rais Magufuli ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini kuitwa Halmashauri ya Mtama na Makao Mkuu ya Halmashauri hiyo ihamishiwe Mtama kutoka Mjini

Amesema ndani ya siku 15, Viongozi wa Halmashauri hiyo watoke Mjini na kuhamia Mtama na hiyo ndio italeta maendeleo kwani kama ni giza ndio watashughulikia umeme haraka

Aidha, amesema “Najua kulikuwa na mabishano, wapo wanaotaka Makao Makuu yaende Subi, wapo waliotaka yaende Mchinga, wapo waliotaka yaende Rondo, kila mmoja alitaka”

Amefafanua, “Kwa kuwa mimi ndio Rais, na mimi huwa napasua katikati kwa kufuata haki nimetoa maagizo, Manispaa ya Lindi itachukua eneo lake iliyokuwa nalo mpaka Mnazi Mmoja au Mingoyo na kuongezewa eneo la Mchinga.”
 
Kwani hiyo halmashauri wamepelekewa CHADEMA au amewapelekea wananchi?!

Kwanza Lindi Vijijini yenyewe, haina miji na Mtama ndipo panaonekana afadhali kidogo ukitoa Lindi Mjini yenyewe ambayo ndo ilikuwa HQ ya Halmashauri kama zilivyo wilaya nyingi Tanzania!

Kwa maana nyingine, serikali hawakuwa na better option ya kuizidi Mtama ingawaje na yenyewe ni sehemu ya hovyo hovyo tu!!!
 
Kwa kuwa mlinichagua mimi kuwa Rais, na mimi ndiyo Rais sasa naagiza kuwa makao makuu ya halmashauri yatakuwa mtama
 
Kwani hiyo halmashauri wamepelekewa CHADEMA au amewapelekea wananchi?!

Kwanza Lindi Vijijini yenyewe, haina miji na Mtama ndipo panaonekana afadhali kidogo ukitoa Lindi Mjini yenyewe ambayo ndo ilikuwa HQ ya Halmashauri kama zilivyo wilaya nyingi Tanzania!

Kwa maana nyingine, serikali hawakuwa na better option ya kuizidi Mtama ingawaje na yenyewe ni sehemu ya hovyo hovyo tu!!!
Mchinga unapajua?!
 
“Najua hili nimelimaliza Halmashauri ya Lindi Vijijini itaitwa Mtama,Nape shughulikia hili najua Wananchi wako wanakupenda na mimi nakupenda, ulifanya dhambi zako nikakusamehe, Nape nimeshamsamehe sio mtuhumiwa hana dhambi yoyote naomba mshirikiane nae ktk kujenga Mtama mpya“-JPM
 
Naona mungu jpm ameongea Kwamba nape hana dhambi tena
 
Back
Top Bottom