Lindi: Zaidi ya wananchi 22,000 wa Nyangao, Mtama kupata maji safi na salama

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
ZAIDI YA WANANCHI 22,000 WA NYANGAO - MTAMA KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA

Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameshuhudia utiaji saini wa mkataba baina ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wa Mkoa wa Lindi na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Limited kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi na salama wa mradi wa Nnyangao - Mtama

Ujenzi wa mradi huo utanufainisha na kuwawezesha wananchi zaidi ya 22,000 kupata maji safi na salama ambao utagharimu zaidi ya shilingi 4,577,244,446

Mradi huo utatekelezwa jimboni humo kwenye kata tatu za Majengo, Mtama na Nyangao zenye jumla ya vijiji 13 vya Nyangao A, Nyangao B, Mtakuja II, Nangaka, Masasi, Majengo A, Majengo B, Mvuleni, Mihogoni, Mbalala, Makonde, Mnamba (Chluwe) na Mkwajuni

Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Nape ni Mhe. Shaibu Issa Ndemanga, Mkuu wa Wilaya Lindi; Mhe. Yusuph Abdalah Tipu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama; Waheshimiwa madiwani wa maeneo husika, watendaji wa Ruwasa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti comred Athumani Seif Hongonyoko.

Waziri Nape amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

IMG-20220329-WA0121.jpg
IMG-20220329-WA0123.jpg
 
Baada ya kuwatesa miaka zaidi ya uhuru leo mnakuja kujisifia kwa porojo za siasa..sawasawa na baba kuleta chakula kwenye familia na anaaza kujisifia...wakati ndio jukumu lake.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa miaka Ccm iliyo tawala sio sifa kuwaambia watu 22,000 wata pata maji safi. Tulitegemea iwe nchi nzima huduma zote za kijamii ziwe jistoria na sio mapambio tena.
 
Back
Top Bottom