Rais Magufuli: 5,000/= wanazoomba trafiki barabarani hazina shida, ni hela ya kubrashia viatu

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,156
2,000
Amani iwe kwenu wakuu,nimemsikia Rais Magufuli akisema pesa wanazochukua trafiki barabarani hazina shida ni za kung`arishia viatu.

Hii imekaaje kauli hii sio kwamba anahalalisha rushwa? nawaza tu!

Je, uelewa wa Rais kuhusu rushwa ni mdogo au alipitia tu maana kwa maelezo yake Rais anaamini rushwa ni ile labda inayohusisha kiwango kikubwa cha fedha?

Rais Magufuli omba radhi na ufute kauli yako hii tata ambayo inachochea rushwa kuongezeka zaidi.Kwa kauli hii ni wazi wazi Rais Magufuli amewapa vichwa trafiki barabara kuendelea kuomba rushwa! Rais Magu uongozi unahitaji hekima sio kila ni cha kuzungumza!
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,596
2,000
amani iwe kwenu wakuu,nimemsikia rais Magufuli akisema pesa wanazochukua trafiki barabarani hazina shida ni za kung`arishia viatu,hii imekaaje kauli hii sio kwamba anahalalisha rushwa nawaza tu! je uelewa wa rais kuhusu rushwa ni mdogo au alipitia tu maana kwa maelezo yake rais anaamini rushwa ni ile kabda inayohusisha kiwango kikubwa cha fedha? rais wangu magufuli omba radhi na ufute kauli yako hii tata ambayo inachochea rushwa kuongezeka zaidi..kwa kauli hii ni waziwazi rais magufuli amewapa vichwa trafiki barabara kuendelea kuomba rushwa! rais wangu magu uongoz unahitaji hekma sio kila ni cha kuzungumza!

Akuombe radhi wewe?!
Mbona Tanzania nzima wewe peke yako ndiyo umelishupalia hilo? Hilo halitoshi kukushawishi kwamba una matatizo labda ya uelewa? Kwa maana ktk yoote yanayojadiliwa hapa khs Hotuba ya raisi hilo halijaongelewa ila wewe tu ndiyo umelisikia!
 
Chifu Nsyepa

Senior Member
Jul 9, 2016
106
225
Akuombe radhi wewe?!
Mbona Tanzania nzima wewe peke yako ndiyo umelishupalia hilo? Hilo halitoshi kukushawishi kwamba una matatizo labda ya uelewa? Kwa maana ktk yoote yanayojadiliwa hapa khs Hotuba ya raisi hilo halijaongelewa ila wewe tu ndiyo umelisikia!
Duh Barbarosa unatetea mpaka rais kusherehesha rushwa? Ama kweli ukipenda, chongo utaita kengeza!
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,077
2,000
amani iwe kwenu wakuu,nimemsikia rais Magufuli akisema pesa wanazochukua trafiki barabarani hazina shida ni za kung`arishia viatu,hii imekaaje kauli hii sio kwamba anahalalisha rushwa nawaza tu! je uelewa wa rais kuhusu rushwa ni mdogo au alipitia tu maana kwa maelezo yake rais anaamini rushwa ni ile kabda inayohusisha kiwango kikubwa cha fedha? rais wangu magufuli omba radhi na ufute kauli yako hii tata ambayo inachochea rushwa kuongezeka zaidi..kwa kauli hii ni waziwazi rais magufuli amewapa vichwa trafiki barabara kuendelea kuomba rushwa! rais wangu magu uongoz unahitaji hekma sio kila ni cha kuzungumza!
Kwani hiyo ndio main topic au ilikuwa kipande cha story tu kuelezea jambo kubwa?!!
 
myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,624
2,000
Sitaki kuamini kama kweli Rais ameongea hayo! Na kama kweli amesema basi amepotoka; tena kupita kiasi kwa maana anachukulia kana kwamba wote wanaopita barabarani ni wenye ma VX na hivyo, ni kama inaonekana ndogo! Mtu mwenye VX yake hawezi kuombwa 5,000 hata siku moja! Atakayeombwa 5,000 ni wale wenzangu na mimi; hususani Bajaj na Bodaboda!

Kwa mtu wa Bajaj na Bodaboda; Sh.5000 kwake ni nyingi sana; sawa na kama ambavyo wenye nazo wanavyoweza kuombwa mamilioni!

Narudia, siamini ikiwa kweli ametamka hayo na kama ametamka basi amepotoka!
 
endesha

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
974
1,000
Nilichokisema ni kwamba wewe una matatizo labda ya euelewa, jiulize kwa nini wewe peke yako ndiyo umelisikia hilo? Kwa nini halijajadiliwa hilo hapa JF tangu Hotuba itolewe? Kwa nini wewe ndiyo ulilete?
Acha basi nawewe kutetea kila kitu..Mtu yeyote ana Uhuru wa kuleta taarifa/hoja yoyote jukwaani ilimradi ni ya kweli,labda umshambulie mleta mada kama aliloliwasilisha halina ukweli.Tatizo lako hupendi kusikia usilolipenda.JIKITE KWENYE MADA.
 
simba45 mkali

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,981
2,000
Acha basi nawewe kutetea kila kitu..Mtu yeyote ana Uhuru wa kuleta taarifa/hoja yoyote jukwaani ilimradi ni ya kweli,labda umshambulie mleta mada kama aliloliwasilisha halina ukweli.Tatizo lako hupendi kusikia usilolipenda.JIKITE KWENYE MADA.
Mkuu tatizo ni njaa na kuchangia kwa sifa ata kama ni uozo ni basi tu ili kufurahisha mabwana zao.
 
mbeziboy

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
1,502
2,000
Sitaki kuamini kama kweli Rais ameongea hayo! Na kama kweli amesema basi amepotoka; tena kupita kiasi kwa maana anachukulia kana kwamba wote wanaopita barabarani ni wenye ma VX na hivyo, ni kama inaonekana ndogo! Mtu mwenye VX yake hawezi kuombwa 5,000 hata siku moja! Atakayeombwa 5,000 ni wale wenzangu na mimi; hususani Bajaj na Bodaboda!

Kwa mtu wa Bajaj na Bodaboda; Sh.5000 kwake ni nyingi sana; sawa na kama ambavyo wenye nazo wanavyoweza kuombwa mamilioni!

Narudia, siamini ikiwa kweli ametamka hayo na kama ametamka basi amepotoka!

mkuu ni kweli kabisa JPM kayatamka hayo. Hata mimi nilishtuka sana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom