Rais kuwa mkali hii nchi uhalifu ulipungua wakati

Rais wangu mpendwa,SHS,ni napenda kukushauri uwe na moyo mkuu,ukawe jasiri na hodari,mkono wako usilegee,kuwa mkali sana dhidi ya uhalifu wa aina yoyote nchini.Utaokoa wengi na kuendeleza amani kwa watu wote wenye mapenzi mema.

Nimekuomba Rais wangu mpendwa mheshimiwa mama yetu SHS,kwa sababu ya dalili mbaya kuanza kuonekana kwa haraka sana baada ya kifo cha JPM.

Jambo moja tu nitaomba uniwie radhi ni kwamba sijui kuandika kwa mpangilio wa kisomi.Nimesubiri wanaojua kuandika waandike lakini sijaona wakiandika kuhusu haya.

Taarifa za wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi kuanza kusikika,mfano mtoto aliyeuwawa Tabora,zimeniumiza sana.Hatukusikia mambo haya wakati wa JPM.

Kuanza kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu kama vibaka,na sio muda mrefu tutasikia tena watekaji wa mabasi usiku,na mambo kama hayo yanarudi kwa kasi.

Ninakushauri,iwapo makamanda wakionekana kuruhusu mambo haya,wachukulie hatua kali ili wasikudharau.Ninashukuru IGP wa sasa ni mchapa kazi sana na hakuruhusu ujinga kama huo wa kuwaacha wahalifu watawale usiku.

Nisikuchoshe Rais wangu,Mungu mwenyezi akuongoze Rais wangu mpendwa ili watu waendelee kulala usingizi bila hofu.
Uhalifu haukupungua bali kilichokuwa kimepungua/hakipo ni kutolewa kwa taarifa za uhalifu. Ilikuwa ni marufuku kwa vyombo vya habari kutangaza taarifa kama hizo na zingine za majanga kama njaa na mapigano ya wakulima na wafanyakazi (Ref. karipio la Magufuli kwa ITV baada ya kutangaza taarifa za mapigano ya wafugaji na wakulima kule morogoro)
 
Back
Top Bottom