Rais kuwa mkali hii nchi uhalifu ulipungua wakati

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,636
7,005
Rais wangu mpendwa,SHS,ni napenda kukushauri uwe na moyo mkuu,ukawe jasiri na hodari,mkono wako usilegee,kuwa mkali sana dhidi ya uhalifu wa aina yoyote nchini.Utaokoa wengi na kuendeleza amani kwa watu wote wenye mapenzi mema.

Nimekuomba Rais wangu mpendwa mheshimiwa mama yetu SHS,kwa sababu ya dalili mbaya kuanza kuonekana kwa haraka sana baada ya kifo cha JPM.

Jambo moja tu nitaomba uniwie radhi ni kwamba sijui kuandika kwa mpangilio wa kisomi.Nimesubiri wanaojua kuandika waandike lakini sijaona wakiandika kuhusu haya.

Taarifa za wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi kuanza kusikika,mfano mtoto aliyeuwawa Tabora,zimeniumiza sana.Hatukusikia mambo haya wakati wa JPM.

Kuanza kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu kama vibaka,na sio muda mrefu tutasikia tena watekaji wa mabasi usiku,na mambo kama hayo yanarudi kwa kasi.

Ninakushauri,iwapo makamanda wakionekana kuruhusu mambo haya,wachukulie hatua kali ili wasikudharau.Ninashukuru IGP wa sasa ni mchapa kazi sana na hakuruhusu ujinga kama huo wa kuwaacha wahalifu watawale usiku.

Nisikuchoshe Rais wangu,Mungu mwenyezi akuongoze Rais wangu mpendwa ili watu waendelee kulala usingizi bila hofu.
 
Kwani huyo anaesemekana kakutwa na mabilioni aliiba wakati gani? ila alikingiwa kifua.
Nahisi hata hao wengine walikuwepo ila walikingiwa kifua
Over"
 
Miaka mitano iliyopita nchi nzima hakuna aliyewahi kuchaniwa nyavu.
Uwekezaji hautawezekana nchini iwapo uhalifu wa wizi,ujambazi, rushwa nk utaachwa ushamiri. Mama chonde chonde IGP aliweza kwa nini hali inaanza kurudi. Chukua hatua na kwa kiasi kidogo cha haki za binadamu kwenye eneo hili.
 
Huku vijijini imebidi tujiongeze, tumeanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi wakati tulikuwa tumeishasahau huu ujinga! Tunaibiwa hadi simu za vitochi, kuku, nk!
Watu tunajiuliza JPM aliwezaje wajameni!?? Hiii bhagosha!
 
Uhalifu ulikuwepo sana tu watendaji wa Serikali ndiyo waliongoza kwa uhalifu mfano hai ni jambazi Sabaya
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom