CHARLES2016
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 376
- 435
Yaani wabongo hamna jema, mtu anaenda zake likizo nyumbani kwao kama watumishi wengine inakuwa shida, kwa hiyo akiwa Rais hatakiwi kwenda likizo? Kama angeenda likizo ughaibuni angalau mgepiga kelele, lakini yupo Chato mkoa wa Geita. Au Chato siyo Tanzania?Toka Rais Magufuli ameingia madarakani amekuwa na desturi ya kurudi nyumbani kwao Chato kila kipindi cha likizo yake kinapowadia.
Ni jambo zuri sana, ukilinganisha na wale waliokuwa kila kukicha wanasafiri kwenda nje.
Lakini swali kubwa lipo hapa, Ikulu ipo Dodoma, wafanyakazi wote wa ofisi ya Rais kwa sasa wanamakazi Dodoma, je anapoenda Chato gharama za malazi, chakula na fedha ya kujikimu nani analipia?
Gharama za kusafirisha polisi, wanajeshi na wafanyakazi wote wanaoambatana nae kwenda Chato nani analipia?
Tunakazana sana kulipa kodi kizalendo basi matumizi ya kodi zetu nayo yawe ya kizalendo. La sivyo tutatafutana ubaya.
Gharama ziko palepale awe Dodoma au mkoa mwingine kwa sababu popote alipo lazima aambatane na wasaidizi wake.