Rais kukaa Chato ni gharama kwa Taifa

Rais kukaa Chato ni gharama kwa Taifa

Hivi Magu anatumia gharama zaidi ya zile za Kikwete kwenda nje ya nchi kila mwezi?

Yani Magufuli kuwa chato ni gharama sana wakati ameokoa mabilioni kwakutosafiri nje karibu miaka 5?
 
kweli watanzania hata ukioga baharini watasema unawatimulia vumbi.hehehe
 
Kaka mimi nipo huku kwa Malikia, nimesikia Tanzania kuna kaeneo kamejitenga na kuwa nchi inayojitegenea kanaitwa CHATO, hiz tarifa n za kwel ????
Wewe endelea kuosha vibibi huko mambo ya tz hayakuhusu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi Magu anatumia gharama zaidi ya zile za Kikwete kwenda nje ya nchi kila mwezi?

Yani Magufuli kuwa chato ni gharama sana wakati ameokoa mabilioni kwakutosafiri nje karibu miaka 5?

Kikwete alitumia vibaya hii haimfanyi na yeye atumie vibaya hata kama amepunguza
 
Route zake zimekuwa nyingi huo utimamu gani anaoutaka kila siku unamaanisha hayupo fit kila siku anataka repair?
Rudia vizuri kusoma utanielewa.
Umewahi kujibu kabla hauja digest vizuri maelezo yangu.

Si lazima yeye ndiyo anaye hitaji 'repair'.
 
Rudia vizuri kusoma utanielewa.
Umewahi kujibu kabla hauja digest vizuri maelezo yangu.

Nimekuelewa vizuri sana tu lakini mtu anayefit kuwa rais hawezi kuwa anasaka utimamu kila baada ya miezi miwili hata kama ni muajiriwa hapo ungetimuliwa
 
Mmezidi wivu, hamtaki mtu ajipumzikie nyumbani kwake ? Hasafiri hovyo kwenda ulaya na ameokoa mapesa mengi bado anafanya maendeleo makubwa anastahili kukaa likizo popote pale duniani ila kuokoa gharama kaenda kukaa kijijini kwake. Magufuli is very humble na mzalendo.
 
Nimekuelewa vizuri sana tu lakini mtu anayefit kuwa rais hawezi kuwa anasaka utimamu kila baada ya miezi miwili hata kama ni muajiriwa hapo ungetimuliwa
Kwa hivyo ukiwa raisi kipindi chako chote ukiwa madarakani wewe mwenyewe 'familia yako, ndugu jamaa na marafiki' mnakuwa na kinga flani dhidi ya matatizo ya kidunia kama ya kiafya n.k?

Ukiwa na ndugu mwenye tatizo lolote inabidi uitishwe uchaguzi tena?
Ukipata shida yoyote ya kifamilia uitishwe tena uchaguzi kumbadili raisi?

Wakosoaji wa kibongo wanawaza kiajabu ajabu sana kulinganisha na umri wao!!!!!
 
Kwa upande wa gharama sidhan Kama ni issue, Kama ni polisi hata chato wapo. Jamaa hajawahi kusafiri hivyo ameokoa billions. It's a minor issue guys
Si kila polisi wa police post anaweza kumlinda rais kuna special unit guards.
 
Kwahiyo asiende likizo kwao kama mkataba wa kazi unavyotoa siku 30 za likizo kwa mwaka!?
Rais ni kiongozi siyo mfanyakazi ingawa analipwa mshahara kwa hiyo hana likizo ya siku kadhaa kwa mwaka kama wafanyakazi ila akichoka kuteua na kutengua anaweza kwenda kokote kupumzika kwa muda anaoona unafaa.
 
Kama anatekeleza majukumu yake ya Urais hiyo haiwezi kuwa likizo kwa kuwa alichokifanya hata makamu wa Rais angeweza kukifanya, hapo amekwenda Chato kusalimia na wakati huo huo anatekeleza majukumu yake ili mambo yaendelee kama kawaida vinginevyo angemwachia makamu wa Rais na Waziri mkuu kama kweli ni likizo kwa mujibu wa kazi.
Rais wetu ni mchapakazi mzuri mwacheni aende chato kila mara hamchoki kuzungumza kuhusu chato hayo ni mapenzi yake lazima aende kwao kusalimia ila tu asisahau majukumu aliokabiziwa na wanyonge wa hali ya chini watanzania kuleta maendeleo kwa kila mtanzania.
Ruksa nenda Chato huu ni uzalendo, kwenu ni kwenu tu hata kama ni polini.
 
Vizuri ni gharama ndg. Acha alindwe kwa gharama yoyote.

Huyo nimkombozi wa watanzania zaidi ya ml.50
 
Tunasahau Rais kama binadamu naye anafamilia na ndugu zake, kingine naye pia kama mtumishi wa umma ana stahiki zake ikiwemo likizo zilizopo kisheria.

Mzee Kikwete alikuwa akienda msoga kwa likizo, Nyerere naambiwa alikuwa anaenda Butiama. Kingine Rais hawezi safiri yeye na familia yake tu lazima ataambatana na walinzi, wasaidizi na wengineo wengi tu iko hivyo duniani kote Watanzania tu tunagubu hawakuwahi kulalamikia likizo za jk msoga.

Regards tumpongeze rais wetu kufanya kazi akiwa likizo
 
Korona imerudi baba sada afanyeje??
Toka Rais Magufuli ameingia madarakani amekuwa na desturi ya kurudi nyumbani kwao Chato kila kipindi cha likizo yake kinapowadia.

Ni jambo zuri sana, ukilinganisha na wale waliokuwa kila kukicha wanasafiri kwenda nje.

Lakini swali kubwa lipo hapa, Ikulu ipo Dodoma, wafanyakazi wote wa ofisi ya Rais kwa sasa wanamakazi Dodoma, je anapoenda Chato gharama za malazi, chakula na fedha ya kujikimu nani analipia?

Gharama za kusafirisha polisi, wanajeshi na wafanyakazi wote wanaoambatana nae kwenda Chato nani analipia?

Tunakazana sana kulipa kodi kizalendo basi matumizi ya kodi zetu nayo yawe ya kizalendo. La sivyo tutatafutana ubaya.
 
Misafara imegeuka Dsm kwenda Dom sasa Dom kwenda Chato maendeleo hayana chama
 
Ni jambo zuri sana, ukilinganisha na wale waliokuwa kila kukicha wanasafiri kwenda nje.
Uko shihi kabisa. Nasikia walishaliona hilo siku nyingi na hivyo wana mpango wa kufanya utaratibu ili asiwe anaenda kabisa likizo mapumzikoni, bora awe anaenda nje kuepuka gharama. Kawaida hawa watu huwa hawaruhusiwi kurudi kwao mapumzikoni mpaka pale muda wao utakapokuwa umefikia ukomo
 
Back
Top Bottom