Toka Rais Magufuli ameingia madarakani amekuwa na desturi ya kurudi nyumbani kwao Chato kila kipindi cha likizo yake kinapowadia.
Ni jambo zuri sana, ukilinganisha na wale waliokuwa kila kukicha wanasafiri kwenda nje.
Lakini swali kubwa lipo hapa, Ikulu ipo Dodoma, wafanyakazi wote wa ofisi ya Rais kwa sasa wanamakazi Dodoma, je anapoenda Chato gharama za malazi, chakula na fedha ya kujikimu nani analipia?
Gharama za kusafirisha polisi, wanajeshi na wafanyakazi wote wanao ambatana nae kwenda Chato nani analipia?
Tuna kazana sana kulipa kodi kizalendo basi matumizi ya kodi zetu nayo yawe ya kizalendo. La sivyo tutatafutana ubaya.