Rais kuhutubia Bomang'ombe haitamsaidia lolote

Na Professor Issa Shivji

Kwani uchifu ni utamaduni wetu? Makabila mengi hawakuwa na wachifu. Waliwekwa na wakoloni kwa maslahi yao (km Wazanaki). Uchifu ulipigwa marufuku na sheria mnamo 1962. Machifu waliyokuwepo (km Adam Sapi, Fundikira, Kunambi nk) waliingizwa Serikalini katika nyadhifa mbalimbali.

Ufutaji wa uchifu ulitusaidia sana kujenga umoja wa kitaifa.Nchi zingine Za Afrika (kmNigeria, Ghana nk) wamepata shida kujenga umoja wa kitaifa. Sababu mojawapo ni machifu kulinda himaya zao kwa kukuuza ukabila badala ya utaifa. Tunachotakiwa kusisitiza ni utamaduni wa kitaifa.
Sio kweli kwamba hatukuwa na utamaduni wa kichifu na kwamba wakoloni walieta uchifu.

Machifu walikuwepo kabla ya kuja ukoloni na huo ndio ulikuwa utamaduni wetu halisi.

Wakati wa ukoloni walijitahidi sana kuwapandikiza machifu wanaokubaliana na ideologies zao.

Baada ya uhuru nyerere aliwajumuisha kwenye serikali ili kupunguza nguvu zao na kuondoa aina yeyote ya upinzani kwa serikali.
 
IMG-20220122-WA0108.jpg
 
Achangie huo utamaduni wa taifa ni upi?!!!
 
Rubber stamps leaders in the making for emerging low-low MICs in Africa
 
Mbowe ana tuhuma za uhalifu kama Sabaya tu hawana tofauti. Mbowe sio mfalme wa Hai kama alivyo Kwa wajinga MaCHADEMA.

Samia hahitji watu wa wilaya fulani tu bali watanzania wote Na tunampenda sana Na ataendelea mpaka 2030 Mungu amlinde na husuda kama za MaCHADEMA.

Umeandika nyongo tu uliyonayo Kwa Rais Na kupenda kushabikia wahalifu. Igeni ACT wenye hoja za maana maCHADEMA hopelessly kazi kukaa mahakamani kila siku badala ya kushughulika na shida za wananchi.

#MBOWE NI MTUHUMIWA KAMA SABAYA#
Unapambana na CHADEMA wakati humo kwenye inzi wa kijani kuna sukumagang wanamlia Mazaa timing?!
 
Sio kweli kwamba hatukuwa na utamaduni wa kichifu na kwamba wakoloni walieta uchifu.

Machifu walikuwepo kabla ya kuja ukoloni na huo ndio ulikuwa utamaduni wetu halisi.

Wakati wa ukoloni walijitahidi sana kuwapandikiza machifu wanaokubaliana na ideologies zao.

Baada ya uhuru nyerere aliwajumuisha kwenye serikali ili kupunguza nguvu zao na kuondoa aina yeyote ya upinzani kwa serikali.

Wafalme wetu waliokuwepo kabla ya Ukoloni siyo hawa, machief ni 100% mzao wa Ukoloni na baada ya Ukoloni, tulikuwa na Wafalme kabla ya Ukoloni, hawa machief waliwekwa na Ukoloni na ilikuwa ni mtindo wa Uingereza kufanya hivyo na walifanya Afrika yote hata India walikotawala, iliitwa indirect rule.
 
Mkwawa alikuwa zao la wakoloni??

Wewe naona unazungumzia title ila mifumo ya kiutawala ilikuwepo kabla ya ukoloni majina ya title ndio yalitofautiana kwa baadhi ya maeneo.
 
Kushabikia uchifu sawa na kushabikia ukabila, wa nini, unakazi gani hasa karne hii, mnataka kutambika? Ndio umuhimu wake uliobaki, sio vinginevyo!
 
Mkwawa alikuwa zao la wakoloni??

Wewe naona unazungumzia title ila mifumo ya kiutawala ilikuwepo kabla ya ukoloni majina ya title ndio yalitofautiana kwa baadhi ya maeneo.

Mkwawa aliuliwa na Wafalme wengi waliokuwepo kabla ya Ukoloni wa Uingereza, kumbuka uchief ulianza baada ya Uingereza kuja, ni mfumo wa Kikoloni wa Uingereza, hawa machief wengi wa leo hii hawakuwa machief kabla ya Uingereza kuja.
Iko documented kila mahali na shuleni tulifundishwa kuhusu indirect rule ya machief.

Usichanganye na Wafalme waliokuwepo kabla ni mambo mawili tofauti, Wafalme wetu walipinga Ukoloni na walipigana Vita ila Machief wote kama akina Mariale & Co. walisapoti Ukoloni na walikuwa ni sehemu ya Ukoloni, walitumiwa kama kiungo na Uingereza kutawala na ndicho Serikali za Kiafrika kama Kenya wanachofanya mpaka leo, Vita yote ya Kikabila Kenya inaanzishwa na hawa machief kwa kutumiwa na Wanasiasa na hata sasa hivi huyu anachokifanya ni hicho kama Ukoloni ulivyofanya anachukuwa machief wanapewa fedha halafu machief wanakwenda kufanya Kampeni kwa niaba ya Raisi/Mkoloni kwa wananchi na kwa kuwa wananchi wanakuwa wanawaheshimu hawa machief wanawasikiliza na ndio maana inaitwa indirect rule.
 
Wachaga sio wajinga mumuibie kura na bado mnataka kumfunga malizeni mliyopanga kumfanyia msisahau hata Ben Saanane hayupo wachaga wanamlilia sana. Msiende uchagani mnajichumia laana.
Kwahiyo kumbe ishu ni UCHAGA?? Tunakubaliana kuwa CHADEMA ni CHAMA CHA KICHAGA?????
 
Sio kweli kwamba hatukuwa na utamaduni wa kichifu na kwamba wakoloni walieta uchifu.

Machifu walikuwepo kabla ya kuja ukoloni na huo ndio ulikuwa utamaduni wetu halisi.

Wakati wa ukoloni walijitahidi sana kuwapandikiza machifu wanaokubaliana na ideologies zao.

Baada ya uhuru nyerere aliwajumuisha kwenye serikali ili kupunguza nguvu zao na kuondoa aina yeyote ya upinzani kwa serikali.
Sasa kuna tofauti gani na alichoandika Mshana ? Hoja hapa ni Hangaya kuleta mambo ya uchifu ili apenye , hata hivyo ameshitukiwa mapema sana
 
Back
Top Bottom