Rais kufia madarakani na kumpata Rais Mwanamke kwa mara ya kwanza, hii inaashiria nini?

Kwamba wanaume tumeshindwa kulisaidia taifa, kwamba mabadiliko makubwa yanakuja, kwamba Mungu ametoa fursa ya kutengeneza mifumo yenye nguvu badala ya watu wenyenguvu.
 
Salaam,

Ramadhan Maqbul.

Wanajamvi naomba kuongea haya na labda kuibua hoja. Kama nilivyoanza kwenye kichwa cha Habari hivi Katika historia ya nchi hii ni mara ya kwanza Rais anafariki akiwa Madarakani na Kwa Mara ya kwanza tunapata Rais ambaye ni Mwanamke; hii inaashiria nini?

Kwanza kwetu limekuwa jambo geni sana, ndiyo maana uliona kunakuwa na sintofahamu nyingi! Pia kuona tunafanya transition kwa amani haikutegemewa ndiyo maana wale walioishi kwa kumtegemea mtu na siyo uwezo wao kwa sasa wametahayuri.

Pia Makamu wa Rais kuwa Rais na kujiamini ni kukomaa kwa siasa ninaona mbeleni kuna mabadiliko mengi katika medani ya siasa.

Mwisho.

Naomba utupe mawazo yako hapa.

Kazi iendelee.
Kupita kipindi hiki mkuu salama inawezekana ni kwa sababu Watanzania ni waoga/hawapendi vurugu.

Kwa upande mwingine kuwa na Rais mwanamke kuna ashiria nini,huu ni mkakati mpana wa wanaoitawala dunia ambao ni Luciferian.Mkakati wao siku zote ni kufanya mambo kinyume na mpango wa Mungu.As to what will happen,ni yale yale yanoyoweza kuikumba nchi iliyomuasi Mungu na kufanya mambo kivyake.Biblia imeizungumzia sana Israel kuhusiana na athari ya kudharau maagizo ya Mungu.
 
Na uzuri amekuwa tofauti na mtangulizi wake na nchi inaonekana inacheka na kuna matumaini mapya! Ukiangalia kwa undani kuna mambo mengi yanaenda kubadilika na chuki zitaisha japo kuna watu ndani ya watendaji wake kuendelea na misimamo ya mwendazake.
 
Back
Top Bottom