Rais Kikwete,tafadhali chagua moja

kasitile

Member
Feb 22, 2011
32
0
Pasi na shaka hakuna tena ari mpya,kasi mpya wala nguvu mpya serikalini,semina elekezi za Ngurdoto nikazi bure na upotevu wa mali za umma.Si siri tena kuwa maisha bora kwa kila mtanzania hamna,zaidi kuna maisha bora kwa kila kigogo.Utendaji wa serikali ya Kikwete umedorora sana japo kuna mazuri ambayo serikali hii imeyatenda,lakini hatuwezi tukakaa na kunywa mvinyo kusherehekea mafanikio machache yaliyoyopatikana,wakati baada ya miaka 50 ya uhuru bado kuna watu wanakula mizizi ili kujinusuru na njaa inayowakabili.

Inawezekana Kikwete akapuza hoja za watu wenye akili timamu na kusikiliza sifa kutoka kwa watu ambao wanamtindio wa ubongo,kwa kile anachokiona kama ni wivu wa urais,maana ni kawaida kwa viongozi wetu wa kiafrika kulewa madaraka na kupuuza sauti ya umma.Hapa Kikwete atakuwa anajidanganya,Tanzania ya sasa sio ya enzi za akina Makamba,watu wameamka,wanajua ugumu wa maisha unaowakabili hautokani na kudra za Mwenyezi Mungu,bali unatokana na uongozi legelege na ufisadi wa kutisha unaofanywa na viongozi wao waliowapa dhamana ya kuongoza taifa.Inawezekana watanzania wastaarabu sana,kiasi kwamba pamoja na ugumu wao wa mwaisha,bado wanampa rais muda ili ajirekebishe pamoja na watendaji wake kama ambavyo amewahi kuwapa muda wala rushwa na wauza madawa ya kulevya vinginevyo atakwenda na maji,au hata chama chake atakiacha katika makati mgumu sana atakapoondoka ikulu mwaka 2015.

Inawezekana rais Kikwete bado anapendwa kama wapambe wake wanavyojaribu kutuaminisha hivyo, inawezekana wananchi bado wanampenda rais Kikwete kwa sababu ya ujinga walionao, ambapo hawawezi kuhusanisha maisha magumu waliyonayo,na uongozi mbovu,wanaona hali hiyo inatokana na kudra za Mwenyezi MUNGU.
Kama rais angechukulia suala la kupendwa kama njia ya kuwaletea wananchi maendeleo bila shaka sasa tungekuwa tunaongea mengine.

Sina uhakika kama bado Kikwete anayajua maisha ya huku uswahilini,maana katika ziara zake za kusaka misaada nje ya nchi,amewahi kukaririwa kuwa hata yeye hajui chanzo cha umasikini,kama ni kweli hajui umasikini wetu unatokana na nini,kwa nini aligombea urais?,au alitaka naye kusafisha nyota na kuingia kwenye vitabu vya rekodi katika nchi yetu?Sasa rais wetu yuko Magogoni kwa miaka sita kwenye jumba la kifalme akizungukwa na wapambe wanaojipendekeza pasipo kumwambia ukweli,wanafanya kila linalowezekana rais asijue maisha yanayoendelea huku uswahilini,rais asipo badilika hatakwepa laana ya wananchi ambao ndio waajiri wake japo hawaitwi waheshimiwa.

Rais anatakiwa asome alama za nyakati,akipuuza atakwenda na maji au akiona kazi zimemwelemea awe muungwana,aseme wazi hadharani wala hatutamcheka bali tutamwaona muungwana na mzalendo wa kweli,akishindwa aseme wazi yasije yakampata kama ya Hosn Mubarak.

Rais Kikwete inatosha sana,kama miaka sita ilikuwa ya majaribio,bila shaka sasa umejifunza kitu,kama unaweza kuongoza au huwezi unaweza kupima mwenyewe kama alivyopima swahiba wako Lowassa,wakati unajipima mwenyewe,pia wananchi wana vipimo vyao,yanayosemwa huku uswahilini ambako wewe au hata wapambe wako hawafiki ndio haya tunayasema.Kusema kuwa wanaokushauri japo kuwa hawalipwi,kuwa ni wehu ni uendawazimu na kama hata rais wangu unaamini kuwa wanaokukosoa wana wivu na urais wako basi miaka mitano ilikuwa ya bure kabisa.
 
Rais Kikwete unaongea mambo mengi sana,lakini sasa fanya maamuzi maana hatutakupa muda wa kujitetea.Tabia yako ya undumila kuwili au ukinyonga kamwe haitakusaidia,kama kuwa wa moto awe wa moto,kama wa baridi aonekane wa baridi,
 
Rais Kikwete unaongea mambo mengi sana,lakini sasa fanya maamuzi maana hatutakupa muda wa kujitetea.Tabia yako ya undumila kuwili au ukinyonga kamwe haitakusaidia,kama kuwa wa moto awe wa moto,kama wa baridi aonekane wa baridi,

Mimi sina hata lakusema kwa jinsi nilivyo na hasira na hiyo Serikali ya Mkwere, Vijana wote hatuna kazi, nchi imejaa utajiri lakini nafasi wamepewa wageni mzawa ukifungua kabiashara TRA hao wametia timu kuja kuua mtaji wako. Mimi wala sijui hii serikali ya Mkwere inataka tuishi vipi. Kila kukicha nashikwa na hasira mpaka mtu unafikiria kwenda kujilipua nao huko magogoni kama waraabu wanvyofanya:embarassed2:

 
Back
Top Bottom