Landala
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 997
- 473
Watanzania wenzangu najua mnafahamu kuwa tuna chuo kikuu kipya kilichopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani lakini kulikuwa na ulazima gani kwa rais wetu JK kulazimisha hiki chuo kujengwa kwao,mie kwa maoni yangu hiki chuo kingejengwa mikoa ya kusini ya Lindi,Mtwara na Ruvuma au mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga,Mwanza,Mara,Kagera,Kigoma ambapo maeneo hayo hayana vyuo vikuu vya serikali.Uamuzi huu wa rais Kikwete kuamua kujenga chuo kikuu kwao unaonyesha upendeleo wa wazi wa eneo hilo alilotoka.Mie nampongeza JK Kwa kuamua kuendeleza elimu kwa kuhamasisha ujenzi wa chuo kikuu cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.Nasikia pia Bagamoyo kunataka kujengwa uwanja wa ndege wa kimataifa na pia kujengwa tawi la chuo cha usimamizi wa fedha IFM.Napenda kumshauri JK alete maendeleo kwa watanzania wote bila kuwa na upendeleo wa baadhi ya maeneo.