Rais Kikwete na ujenzi wa Chuo kikuu cha Bagamoyo

Landala

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
997
473
Watanzania wenzangu najua mnafahamu kuwa tuna chuo kikuu kipya kilichopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani lakini kulikuwa na ulazima gani kwa rais wetu JK kulazimisha hiki chuo kujengwa kwao,mie kwa maoni yangu hiki chuo kingejengwa mikoa ya kusini ya Lindi,Mtwara na Ruvuma au mikoa ya kanda ya ziwa ya Shinyanga,Mwanza,Mara,Kagera,Kigoma ambapo maeneo hayo hayana vyuo vikuu vya serikali.Uamuzi huu wa rais Kikwete kuamua kujenga chuo kikuu kwao unaonyesha upendeleo wa wazi wa eneo hilo alilotoka.Mie nampongeza JK Kwa kuamua kuendeleza elimu kwa kuhamasisha ujenzi wa chuo kikuu cha Nelson Mandela kilichopo Arusha.Nasikia pia Bagamoyo kunataka kujengwa uwanja wa ndege wa kimataifa na pia kujengwa tawi la chuo cha usimamizi wa fedha IFM.Napenda kumshauri JK alete maendeleo kwa watanzania wote bila kuwa na upendeleo wa baadhi ya maeneo.
 
Anaona ndugu zake wakwere na wadoe wako nyuma sana anafikiri kwa kujenga hivyo vyuo huko kwao ndio watafunguka!! Vyuo vinaweza kujengwa huko wakwere wakaambulia kazi ya kufagia while wakuja ndio wako kwenye lecture rooms!
 
mi naona poa tu kwani hilo eneo inabd liendelezwa uwe mji...dar yenyewe imeshajaa
 
JK ni mbinafsi sana, mikoa km mtwara na lindi iko nyuma sana kimaendeleo, Ben alijitahidi kujenga daraja na barabara ya lami lakini kwa makusudi JK alivyoingia madarakani akatoa hela za ujenzi wa barabara ya ndundu-somanga kwenda kujenga barabara ya bagamoyo-msata, na si hivyo tu hata hivyo vyuo vikuu ni kudhihirisha kuwa anataka upendeleo wa wazi wa kwao, anabahati mbya kuwa hao wakwere hawapendi shule ila ngono na ngoma tu, kwa hio tutasoma sisi wa mikoa ya kaskazini na kwingineko kwenye kuamko wa shule.
 
ben naye mmakonde alijenga daraja kwao naye alipendelea kwao, kwann asingejenga kule kigoma au Tanga kwenda mombasa
 
Ni ufinyu wa fikra na ubinafsi maana haimani kuwajengea vyuo vi gi na shule ndio watasoma au kuendelea. Kwani hajui kuwa "Penye miti hakuna wajenzi" mbona Watannzania tuu maskini pamoja na rasilimali zote tulizonazo?
Anaona ndugu zake wakwere na wadoe wako nyuma sana anafikiri kwa kujenga hivyo vyuo huko kwao ndio watafunguka!! Vyuo vinaweza kujengwa huko wakwere wakaambulia kazi ya kufagia while wakuja ndio wako kwenye lecture rooms!
 
Mimi wa Katavi ndo sisemi kabisa kwenye kuwa mbele au nyuma kimaendeleo, Mungu mwenyewe aingilie kati.Cha kunisikitisha ni kwamba waziri wangu mkuu Mbunge wa Mpanda Mashariki zamani (sasa Katavi) anadhani kuwa maendeleo yanaletwa na viwanja vya ndege ndo maana ameirinovate uwanja wa Mpanda lakini hajui kuwa watu wa Mpanda wenye uwezo wa kupanda ndege hakunaga
 
Moderator ukiamini thread ni umbea potezea mbali.Chuo kikuu Bagamoyo siyo cha serikali wala hakipo Bagamoyo .Jukwaa ili linaheshimika kwa kuonyesha tangible things na siyo umbeya.Bagamoyo University ipo chini ya ubia wa Human rights centre na akina Mvungi.HAPA LEO NAMTETEA JANGA LA TAIFA.
 
Tuambie basi kiko wapi kama sio Bagamoyo?.
 
mi namuunga mkono sababu wahadhiri wengi wapo dar sa bagamoyo itakuwa karibu tofauti na huko mtwara au lindi na hili litapunguza mambo ya padiem na gharama za usafiri, lakini nafikiri wakati wakuwa na sera za majimbo umefika vinginevyo tutakuja dundana
 
Ben alikuta mradi unaendelea, ulianza wakati wa mzee mwinyi

JK ni mbinafsi sana, mikoa km mtwara na lindi iko nyuma sana kimaendeleo, Ben alijitahidi kujenga daraja na barabara ya lami lakini kwa makusudi JK alivyoingia madarakani akatoa hela za ujenzi wa barabara ya ndundu-somanga kwenda kujenga barabara ya bagamoyo-msata, na si hivyo tu hata hivyo vyuo vikuu ni kudhihirisha kuwa anataka upendeleo wa wazi wa kwao, anabahati mbya kuwa hao wakwere hawapendi shule ila ngono na ngoma tu, kwa hio tutasoma sisi wa mikoa ya kaskazini na kwingineko kwenye kuamko wa shule.
 
..acheni mawazo mgando, hakuna alichokosea ht kama yy alipendelea kwao, lakn hicho chuo kitatumika na watanzania wote bila kujali eneo watokalo, watu tumesoma vyuo vkuu ktk mikoa tusiyotoka, ni uvivu wa kufikiri na ninaouita uchademalism kwamba kila kifanyachwo na serikali hii sio sahihi...ht kama wameshndwa kuendeleza nchi hii waacheni ht hiko kidogo wanachokifanya wakifanye kwa uhuru kwani mwisho wao umekaribia tu.....
 
Mie ninavyojua University of Bagamoyo mkuu wa chuo ni Prof Costa Mahalu na VC wake ni Prof Sengodo Mvungi. Kwani hiki ni chuo cha serikali ama kuna mkono wa JK katika uanzishwaji wake? Mbona wakuu hawa ni maadui namba 2 wa JK baada ya Lowasa? na hii University of Bagamoyo wanataka kudili zaidi na Utalii na mengineyo yatafuata. sina hakika kama kuna uwepo wa JK katika hili hebu tupeane taarifa sahihi, sio kwasababu iko Bagamoyo basi Mk.were anahusika, NO!
 
Back
Top Bottom