Rais Kikwete na mkewe safarini nchini Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete na mkewe safarini nchini Kenya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MATESLAA, Sep 11, 2012.

 1. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu

  Ni jambo la kusikitisha na kuuzunisha kwa baba au mkuu wa nchi kusafiri na kuacha nchi yake katika dimbwi la matatizo.

  Kwa habari nilizo zipata mkuu wa nchi yupo Kenya na mkewe amelakiwa na Kibaki, ni jambo la kushangaza sana embu tujadili hili swala bila kuweka itikadi zetu hapa.

  Source: Channel ten

  ============

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Kenya Jumanne, 11 Septemba , 2012, kuanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa ameshawahi kufanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.

  Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, Rais Kikwete ambaye amefuatana na mkewe, Mama Salma Kikwete, amepokewa na mwenyeji wake, Rais Mwai E. Kibaki na kwa mbwembwe zote za kiprotokali zinazoambatana na ziara rasmi za kiserikali.

  Baadaye mchana, Rais amekwenda Ikulu ya Kenya ambako ametia saini kitabu cha wageni, akafanya mazungumzo ya faragha na Rais Mwai Kibaki kabla ya kufanyika kwa Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili majirani na wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).

  Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete na ujumbe wake amekwenda kwenye Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako wamepokewa na Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar, Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Mstaafu Onesmus Mutungi na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Olive Mugendi.

  Kwenye chuo hicho ambacho Desemba 8, mwaka 2008, kilimtunuku Rais Kikwete Shahada ya Uzamivu ya Heshima, amefungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo hicho.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Shule hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa utalii ni sekta muhimu sana katika chumi za nchi za Afrika Mashariki na ambayo mchango wake unagusa maisha ya maelfu kwa maelfu ya wananchi wa nchi za ukanda huo.

  Rais pia amesema kuwa nchi hizo za Afrika Mashariki sasa zimekuwa ni eneo lenye mvuto mkubwa katika nyanja ya utalii ambao unaweza kuwaingizia wananchi na mataifa ya Afrika Mashariki mapato zaidi kama changamoto zinazoikabili sekta ya utalii kwa sasa zitashughulikiwa ipasavyo na kwa pamoja na nchi hizo.

  Miongoni mwa changamoto ambazo Rais Kikwete amezitaja ni ukosefu wa miundombinu ya kutosha kufanikisha kwa namna bora zaidi sekta ya utalii, ukosefu wa juhudi za pamoja kuitangaza Afrika Mashariki kama eneo muhimu la utalii, na umuhimu wa kuboresha kiwango cha usalama wa watalii.

  Aidha, Rais Kikwete amezielezea changamoto nyingine kuwa ni pamoja na umuhimu wa kuwepo na viza ya pamoja ya utalii kwa nchi zote za Afrika Mashariki, kuwepo kwa safari za ndege za kutosha kutoka kwenye mataifa makubwa yanayozalisha watalii kwa wingi kuja Afrika Mashariki na umuhimu wa kupungua kwa nauli za ndege za kuja Afrika Mashariki.

  Jioni, Rais Kikwete ametembelea Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI) ambako anatarajiwa kupokelewa na Waziri wa Kilimo wa Kenya, Mheshimiwa Dr. Sally J. Kosgei na usiku alikuwa mgeni rasmi kwenye Dhifa ya Kitaifa ambayo itaandaliwa na mwenyeji wake, Rais Mwai Kibaki.

  Leo Jumatano 11 Septemba, 2012 Rais Kikwete ataweka shada la maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta, kwenye Viwanja vya Bunge la Kenya na kutembelea Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika.

  Kwa mujibu wa ratiba ya ziara yake, Rais Kikwete atatembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi, ambako atapokelewa na Waziri wa Nchi wa Ulinzi, Mheshimiwa Yusuf Haji na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Jenerali Julius Karangi.

  Baadaye, Rais Kikwete atakwenda kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan ambako atapokelewa na Waziri wa Huduma za Matibabu, Mheshimiwa Anyang Nyong'o.

  Baadaye jioni, Rais Kikwete, ambaye anaongozana na kundi kubwa la Wafanyabiashara wa Tanzania, atashiriki chakula cha jioni ambacho ameandaliwa na Jumuiya ya Wafanya Biashara ya Kenya.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  11 Septemba, 2012

  =============


  [​IMG]
  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.

   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha kujadiki hapo.
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  aiseee babaangu we unaona ni sawa
   
 4. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Ameenda kutembelea mashamba ya maua,mwacheni !
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ameshaenda tayari. unaweza kubatilisha hiyo safari? kwa hiyo hiyo hii si habari tena bali ni taarifa. Tugange yajayo
   
 6. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,348
  Likes Received: 6,697
  Trophy Points: 280
  vipi kuna msiba kenya?
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwanche aende kuangalia MABARABARA YA MAANA KIBAKI amejenga wakati wa UTAWALA WAKE; EXPRESS WAYS MPAKA ETHIOPIA na ni TWO WAY LINE Aone hizo barabara za JUU KWA JUU; SIO YEYE NI AHADI na PESA Anaficha USWISI na UTAWALA WAKE...
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Si mara yake ya kwanza kuacha nyumba yake ikiwa imeshika moto wa petroli na yeye kuingia kwenye pipa kwenda kumtembelea jirani.

  Hivyo hata hili jambo la hatari bila spea ya kifo cha mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, kugeuzwa RUNDO LA NYAMA kwa maelekezo ya mawaziri wake; hayo yote kwake ni kama vile ni mmbu tu kafa chumbani wala hakuna tatizo lolote lile.

  Naomba nirudie; wala sijashangaa kitu kusikia kwamba katika hali tete kama hii Rais Jakaya Mrisho Kikwete bado ameweza kupata tu ujasiri wa kuacha yote chini na kwenda uwanjani kukwea kipipa kama kawaida.

  Cha msingi, wale ndugu zetu wenye ule utaratibu wa kutunza kumbukumbu za safari za rais wetu nje ya nchi ni vema mkatupa kumbukumbu hizo hivi sasa kwamba ni safari ya ngapi hiyo baada ya ile ya kwa marehemu Zenawi.
   
 9. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Yaan Roho zenu zitota sugu ya Viroo vya Korosho, hiki kibabu chenye mtoto mchanga Roho ina mkereketa hata tungekupa Urais vurugu za Ndoa na Talaka za wazazi wenzio si zingekula muda wa kutatua matatizo!
   
 10. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yaani huyu hajifunzi ya ile kichwa iko kisafari safari tu
   
 11. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Wana Jf tufikie hatua tuwaelewe viongozi dhaifu wa nchi yetu, mie sioni jipya la kujadiri hapa kwani mtalii wetu tumemzoea hawezi kutuli bila kupanda ndege au kubadirisha hali ya hewa.
  Sanasana navumilia tu amalize mda wake atuachie nchi yetu tuijenge upya.
  Hakuna la kujadiri hapa huyo tumemzoea.
   
 12. M

  Mr.Mpugusa Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli huu uhuru wa kila mtu kuongea vile atakavyo sasa inamgharim. Jamani mie nimekuwa vistor kwa kipindi kirefu sasa nimeona nijiunge nami niweze kutoa mawazo yangu ili kujenga nchi.
   
 13. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  aiseee babaangu hakuna msiba
   
 14. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu wewe unaona si sawa?
  bado haujamzoea raisi wako? Mi hata akipotelea angani sita shangaa!
   
 15. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  aiseee babaangu hakuna msiba ikuli kunachosha ameona atoke na mkewe
   
 16. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,348
  Likes Received: 6,697
  Trophy Points: 280
  una maanisha yeye weekend yake ndo ina anza leo!!!
   
 17. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Naichukia Nchi yangu Tanzania , nawachukia watawala wake, namchukia Kikwete hii ni kwa sababu ya kuanza kuua watu tena mbele ya kadamnasi. Hata mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa uwa ananyongwa kwa staha. Sasa hawa mbwa wake Kikwete walikuwa wanaua mtu hadharani kwa sababu gani ? Hakuna mtu anayetaka kushuhudia haya.

  Tena Kikwete akae kimya tu asitoe neno. Aseme " no comment " asituletee kichefuchefu cha Nchimbi, Tendwa , Nape na wanyama wengi wa polisi . Mtu anauawa mbele ya macho ya watu mchana kweupe , mtu anaibuka na kuanza kubwabwaja kama watu hatuna akili , Ingekuwa busara kwa polisi kusema tunachunguza na kutawapa taarifa, basi. Lakini kuanza kuleta matamshi yanayotia kinyaa inakera.

  Kusema ukweli kama kuna mtu yupo tayari kuanzisha jeshi la msituni nipo tayari kujiunga , Mungu leta gharika angamiza hii nchi ya baraha inayoitwa tanzania. Ni afadhari niitwe Mtanganyika , kuliko kuwa mtanzania , Nchii hii ina laana
  natamani kufa au kujitoa mhanga
   
 18. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Kanyaga twende JK umehangaika sana 2010 kuutetea urais wako,,,,niseme nini sasa??? Ambyulensi au???
   
 19. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  aiseee babaangu ilo si lakuuliza alitaka akale weekend yake dar ila ndio hivyo maandamano so ameamua kujipumzisha na mke weke mama rizi
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kagonga ya 337, still more to count!!!!
   
Loading...