Rais Kikwete na mkewe safarini nchini Kenya

Wakuu

Ni jambo la kusikitisha na kuuzunisha kwa baba au mkuu wa nchi kusafiri na kuacha nchi yake katika dimbwi la matatizo.

Kwa habari nilizo zipata mkuu wa nchi yupo Kenya na mkewe amelakiwa na Kibaki, ni jambo la kushangaza sana embu tujadili hili swala bila kuweka itikadi zetu hapa.

Source: Channel ten
Yataje hayo matatizo mkuu
 
Sasa mlitaka aende wapi kakamkubwa Malya kwa Kabadi,haya ndio maisha tuliyachagua kumuweka yeye madarakani na chama chake
 
I am very sure huyu jamaa atakapo staafu hatakaa hapa Tanzania. Anajiandalia makazi nchi za nje huyu. Hizo ziara anajifunza nini amabcho hawezi ku google kama sie wenzake au kutuma mtu. Ila tuliambiwa huyu sio kiongozi ni mtu wa kunywa nae chai na kuzogoa. Watu aaaa handsome, haya sasa si ndio anauza sura sasa!
Walahi akistaafu aondoke mpaka na wajukuu zake!!!
 



n2.jpg

n1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
n3.jpg

Rais jakaya kikwete akiweka shada la maua kwenye kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
n4.jpg

Mama Salma Kikwete akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
n8.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika nje kidogo ya jiji la Nairobi. Kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho
n7.jpg

Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
n6.jpg

Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho
n5.jpg

Rais Kikwete akiangalia ng'ombe wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n6- Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n7- Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
ag11.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
n9.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi,
n10.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja n ujumbe wake na wanachuo na viongozi wa chuo hicho baada ya kukitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi. Picha na IKULU





 
Back
Top Bottom