Rais Kikwete mgeni rasmi Mei Mosi 2011; fuatilia hotuba

Mwaka jana Akili zako changanya na za mbayuwayu,Mwaka huu Akili zajo changanya na za Kunguru.
 
Mgaya kweli leo umesaliti kambi yetu sie ambao kura zetu zilikuwa hazitakiwi?
Au leo umeenda front line kurusha makombora?
Jihadhari unaweza ukawa umeenda na makombora yako halafu ukajikuta Kikwete anakupa bunda la maua ridi na wewe unampa silaha yako kwa amani bila madhara. Baadae akaitumia silaha yako mwenyewe kukuangamiza.
 
Mkuu Balantanda, tafadhari fafanua ustaarabu naopaswa kuwa nao! Hoja hapo ni Je rais atasema nin? Kumbuka mwaka jana hakualikwa!

Oooooh......Hapana mkuu wangu,sijakulenga wewe.....Angalia vizuri,kuna mtu nimemquote hapo,Ng'wanangwa aliuliza 'umemuona wapi? tujulishe na sisi tufuatilie' akimaanisha Nicholous Mgaya nami nikamjibu 'TBC wanaonesha moja kwa moja toka Moro,mji kasoro bahari' sasa akatokea member akaniquote kwa kusema kwamba 'TBC = Tanzania Broadcasting CCM' ndipo nami nikamquote kwa kumwambia 'Kuwa mstaarabu mkuu...........Kukaa kimya ni busara pia'.....

Tuko pamoja sana mkuu wangu Gagurito,shaka ondoa...

Btw.....Nimeipenda sana Risala ya wafanyakazi iliyosomwa na Mgaya,hajaumauma maneno......

Naangalia na kumsikiliza mgeni rasmi akihutubia sasa......
 
Mgaya kweli leo umesaliti kambi yetu sie ambao kura zetu zilikuwa hazitakiwi?
Au leo umeenda front line kurusha makombora?
Jihadhari unaweza ukawa umeenda na makombora yako halafu ukajikuta Kikwete anakupa bunda la maua ridi na wewe unampa silaha yako kwa amani bila madhara. Baadae akaitumia silaha yako mwenyewe kukuangamiza.

Wamepatana, Rais wa TUCTA amesema ukiona ndugu wanagombana wewe chukua jembe ukalime, na wakipatana chukua kapu ukavune.

Amsema hivyo tu alipotakiwa kumkaribisha Raisi, kwa maana hiyo TUCTA (Mgaya) na Serikali sasa ni kitu moja.
Nasubiri nisikie kama Rais atatuongezea mishahara.
 
Mgaya kweli leo umesaliti kambi yetu sie ambao kura zetu zilikuwa hazitakiwi?
Au leo umeenda front line kurusha makombora?
Jihadhari unaweza ukawa umeenda na makombora yako halafu ukajikuta Kikwete anakupa bunda la maua ridi na wewe unampa silaha yako kwa amani bila madhara. Baadae akaitumia silaha yako mwenyewe kukuangamiza.

Mgaya ni jasiri,si mnafiki....

Kaisoma risala yake vizuri sana......Hajajiumauma wala kupindisha maneno,kaongea yanayotakiwa ayaongee hasa...
 
JK anatoa data za kuongezeka kwa ajira. Mimi bado nasubiri tu tangazo la kuongezeka kwa mishahara na kuwapunguzia kodi wafanyakazi! Wafanyakazi tunalipa kodi kwenye gross income wakati makampuni (wafanyabiashara) wanalipa kwenye net profit!
 
Wakuu naangalia live through TBC real Mgaya kaongea maneno mazito bila kuyapindisha........mimi nasubiri ishu ya salary na kodi tu...hapo ndio ishu..
 
Hiii TBC vipi mbona inasinzia tena!! JK anatoa data za mikopo ya mamilioni ya bwana fulani! Sijui kama haya mamilioni ya bwana fulani yameleta tija yoyote kwenye uchumi wa nchi hii
 
ili kupanua wigo wa ajira, mbona jk anazungumzia kufungua biashara tu, mfano alioutoa ni kufungua biashara ya kuuza vinywaji (bia na soda) na anahimiza BRELA kupunguza muda wa kupata leseni kwa waombaji wanaotaka kufungua biashara.Je ni kweli nchi hii itasonga mbele kwa wananchi wake wote kuwa wafanyabiashara?
 
JK ni mchumi, amenikuna kwa hotuba yake yenye takwimu za uhakika na matumaini kwa watz
 
Nami nimemsikia. Amekamua vizuri tu mbele ya kikwete, si mnamjua Mgaya? Suala la ukubwa wa kodi ameliongelea. Nasubiri nisikie kikwete atasemaje pamoja na ongezeko la mishahara.
 
Nami nimemsikia. Amekamua vizuri tu mbele ya kikwete, si mnamjua Mgaya? Suala la ukubwa wa kodi ameliongelea. Nasubiri nisikie kikwete atasemaje pamoja na ongezeko la mishahara.

Mkuu mimi katika madai ya TUCTA, hili la kodi ni muhimu sana kwa kuwa Wafanyakazi wanakamuliwa bila kupata msamaha wowote ili hali wafanyabiashara wanapewa misamaha!!
 
Jamani Rais anasema VAT imeshuka kutoka asilimia 20% hadi 8!!! Au ni kosa tu kwa kuwa mimi najua ni asilimia 18%
 
Jamani naona anaelekea kutotoa tamko zaidi ya kusema kuwa kuna mchakato wa kuongeza mishahara na kuangalia uwezekano wa kuwapunguzia wafanyakazi makali.
 
Back
Top Bottom