Rais Kikwete mgeni rasmi Mei Mosi 2011; fuatilia hotuba

The same blablah from my Honourable pesident.Nothing new.The same quantitative statistics from 2005.
 
JK amesema serikali inaanzisha mfuko kwa ajili ya Mikopo yenye masharti nafuu kwa watumishi wa uma kama ilivyo kwa wabunge. Ila hajaongelea kupunuza kodi jamani
 
JK anawaomba wafanyakazi kuwakemea wanotaka kuhodhi mchakato wa katiba mpya ili kila Mtanzania aseme bila kuzomeana.
 
Amemaliza hotuba yake bila kunikata kiu yangu ya mshahara na kupunguza kodi. Kwa kifupi sijapata jipya na hajakidhi matarajio yangu mimi binafsi!! Wafanyakazi bado tuna kilio. Naona hata pale uwanjani watu wamenyong'onyea
 
Wafanyakazi hodari toka idara mbalimbali ni kama ifuatavyo

  • TANESCO - Luninga (2,000,000.00) na TZS 3,000,000.00
  • TTCL - TZS 1,500,000.00
  • Tanznia Piplines - USD 800
  • Halmashauri ya Moshi (Zawadi imeenda kwa mkurugenzi wa manispaa ndg. Kinabo Benadeta) - TZS 1,000,000.00
  • Manispaa Morogoro - TZS 600,000.00
  • Bodi ya Korosho - TZS 1,000,000.00
  • TBC - TZS 1,000,000.00
  • TRL - TZS 1,000,000.00
  • TANAPA - TZS 3,000,000.00
  • Bandari - TZS 1,200,000.00
  • Hydom Lutheran Hospital - 1,500,000.00
  • TPC - TZS 1,270,000.00
 
Wafanyakazi hodari toka idara mbalimbali ni kama ifuatavyo

  • TANESCO - Luninga (2,000,000.00) na TZS 3,000,000.00
  • TTCL - TZS 1,500,000.00
  • Tanznia Piplines - USD 800
  • Halmashauri ya Moshi (Zawadi imeenda kwa mkurugenzi wa manispaa ndg. Kinabo Benadeta) - TZS 1,000,000.00
  • Manispaa Morogoro - TZS 600,000.00
  • Bodi ya Korosho - TZS 1,000,000.00
  • TBC - TZS 1,000,000.00
  • TRL - TZS 1,000,000.00
  • TANAPA - TZS 3,000,000.00
  • Bandari - TZS 1,200,000.00
  • Hydom Lutheran Hospital - 1,500,000.00
  • TPC - TZS 1,270,000.00

jamani nilikuwa nimelala. sauti ya jk ilinifanya nilale kwenye kochi.

hivi inakuwaje, amesema nini kuhusu mishahara ya wafanyakazi. maana nimemsikia hapa mwishoni akisema hajataja mambo yote. Asijekuwa ameruka ishu ya inkrimenti.
 
jamani nilikuwa nimelala. sauti ya jk ilinifanya nilale kwenye kochi.

hivi inakuwaje, amesema nini kuhusu mishahara ya wafanyakazi. maana nimemsikia hapa mwishoni akisema hajataja mambo yote. Asijekuwa ameruka ishu ya inkrimenti.

Amesema ameyasikia maombi/madai ya wafanyakazi kuhusu mishahara na kupunguza P.A.YE,yatafanyiwa kazi kwa wakati...

Kimsingi hotuba ya Rais imetokana na Risala iliyosomwa na Mgaya,i.e alikuwa akijibu maombi na mapendekezo ya Risala ya wafanyakazi iliyosomwa na Mgaya
 
jamani nilikuwa nimelala. sauti ya jk ilinifanya nilale kwenye kochi.

hivi inakuwaje, amesema nini kuhusu mishahara ya wafanyakazi. maana nimemsikia hapa mwishoni akisema hajataja mambo yote. Asijekuwa ameruka ishu ya inkrimenti.

Mkuu hajagusa inkriment!! Amesema kuna mchakato wa kufanya increment na umekuwa ukiendelea tangia waingie madarakani. Kwa kifupi kama una hotuba ya Diamond Jubilee isome tu au isikilize ni hiyohiyo tu. Tofauti moja ni kwamba leo kamtaja Mgaya mara mbili tu, hajakataa kura za wafanyakazi na wala kuwatishia kama watagoma!
 
Amesema ameyasikia maombi/madai ya wafanyakazi kuhusu mishahara na kupunguza P.A.YE,yatafanyiwa kazi kwa wakati...

Kimsingi hotuba ya Rais imetokana na Risala iliyosomwa na Mgaya,i.e alikuwa akijibu maombi na mapendekezo ya Risala ya wafanyakazi iliyosomwa na Mgaya

hapo red.....

'kwa wakati' maana yake nini?

how long is 'kwa wakati'?

sekunde ngapi? dakika ngapi? masaa mangapi? siku ngapi? majuma mangapi? miezi mingapi? miaka mingapi? miongo mingapi? karne ngapi?
 
hapo red.....

'kwa wakati' maana yake nini?

how long is 'kwa wakati'?

sekunde ngapi? dakika ngapi? masaa mangapi? siku ngapi? majuma mangapi? miezi mingapi? miaka mingapi? miongo mingapi? karne ngap
i?

Hata sijui nikujibu nini Mungu wangu, umeuliza kuhusu alichozungumza Rais kuhusu mishahara nimekujibu.

Btw , siku hizi utaratibu umebadilika nyongeza ya mshahara hutajwa/hutangazwa wakati wa bajeti na si wakati wa sherehe za wafanyakazi (May Day) kama ilivyokuwa zamani, so labda wakati wa bajeti (June) ndio itajulikana huo 'wakati' unaoulizia.
 
hapo red.....

'kwa wakati' maana yake nini?

how long is 'kwa wakati'?

sekunde ngapi? dakika ngapi? masaa mangapi? siku ngapi? majuma mangapi? miezi mingapi? miaka mingapi? miongo mingapi? karne ngapi?

Mkuu nilivyosikiliza naona kwa wakati ni kuanzia 2005 walipoingia madarakani wakakuta mshahara ni Tshs. 86,000.00 wakaupndisha na wanaendelea na mchakato!!! kwa maana nyingine hakuna wakati hapa!!
 
Ndugu Rais wa TUCTA na Ndugu Wafanyakazi;
Haya ni mapinduzi makubwa katika kulinda haki na kuendeleza maslahi ya wafanyakazi nchini.Wafanyakazi wameongezewa fursa ya kutoa maoni yao na kauli yao kusikika katika kujadiliviwango vya ujira wao na waajiri wao. Inawezekana si kila wanachotaka wafanyakazikikatekelezwa au wakakipata kwa kiwango kile walichotaka, lakini hawatoki mikono mitupu. Pia,hoja zao zinakuwa zikisikika na wao wamewasikia waajiri wanachosema. Hakika hatua tuliyofikiasi ndogo hata kidogo. Kwa upande wa LESCO, naambiwa kuwa katika Bara la Afrika pengine nisisi na Afrika ya Kusini tu ndiyo wenye chombo cha namna hiyo.
Wajibu wa Waajiri na Serikali
Ndugu Wafanyakazi;
Katika kulinda na kuendeleza haki za wafanyakazi, waajiri nao wana wajibu wa kuhakikishakwamba wanafuata matakwa ya sheria za kazi za nchi. Aidha, wanao wajibu wa kudumishamahusiano mema kazini kwa manufaa yao wenyewe na wafanyakazi wao. Nimesikia kilio chawafanyakazi kwamba pamoja na kuwepo sheria na mifumo ya kulinda haki za wafanyakazi, wapobaadhi ya waajiri wanapuuza yote hayo. Wapo ambao hawaheshimu sheria zihusuzo ajira walamishahara na maslahi ya wafanyakazi wao. Wapo pia wanaokataza wafanyakazi wao kujiunga navyama vya wafanyakazi na hawaruhusu matawi ya vyama hivyo kufunguliwa katika maeneo yaoya kazi.Ni vyema waajiri wote wakatambua kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai na wanastahili adhabukali. Nakuomba Mheshimiwa Waziri, Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Kamishna waKazi msimamie sheria kwa ukamilifu. Wabaneni kisawasawa waajiri wote ili waheshimu sheria zakazi za nchi. Wasiotii wachukuliwe hatua na kuwajibishwa ipasavyo. Mamlaka mnayo,yatumieni. Asiwatishe mtu ye yote kwani sheria zinawalinda. Aidha, wabaneni Maafisa wa Kazina Wakaguzi wa Kazi watimize ipasavyo wajibu wao. Baadhi yao wanalalamikiwa kuwa hawatendihaki na wanaonekana kuegemea sana upande wa waajiri wanaowakandamiza wafanyakazi.
Mheshimiwa Waziri;
Sisemi kuwa maafisa hao wasiwe wakweli kama wafanyakazi hawana haki. Ninachosema ni kuwalazima hisia hizi hasi za kuwa wanawapendelea waajiri zifutike kwa wao kutenda haki nawaonekane wanafanya hivyo. Msichelee kuwawajibisha wanaopindisha sheria. Si vibayamkafanya uhamisho wa maofisa wenu waliokaa kituo kimoja kwa muda mrefu. Wahengawanasema: “mazoea yana taabu”
Wajibu wa Wafanyakazi
Ndugu Rais wa TUCTA na Ndugu Wafanyakazi;
Kwa upande wenu, yaani vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wenyewe, nanyi mnao wajibumuhimu katika juhudi za kulinda na kuendeleza haki za wafanyakazi. Wajibu wenu wa msingi niule wa kudai haki zenu bila woga huku mkizingatia sheria na kununi za kufanya hivyo. Ndiyomaana vyama vya wafanyakazi vipo. Timizeni ipasavyo wajibu wenu huo. Kila kilio kinawenyewe.Ili malengo yenu yafanikiwe kwa urahisi ni muhimu sana kwenu kuhakikisha kuwa wanachamawenu wanazifahamu vyema sheria na kanuni za kazi zinazowahusu. Mfanyakazi anayejua sheriaatafahamu vyema nini cha kudai na akidai vipi ili apate mafanikio. Atafanya hivyo kwa kujiaminina hatimaye atafanikiwa. Kamwe mfanyakazi huyo hatokuwa mtumwa.
Ndugu Wafanyakazi;
Pamoja na hayo lazima vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kutambua kuwa ulinzi wa haki zawafanyakazi huanzia kwa wafanyakazi kutekeleza vyema wajibu wao na majukumu yao katikakazi zao. Kwa kawaida waajiri huwapenda na kuwaenzi wafanyakazi hodari wa kazi na waaminifuna huchukia wavivu, wezi, wasiokuwa waadilifu na watovu wa nidhamu.Wafanyakazi wenyewe na Vyama vya wafanyakazi viwakumbushe wafanyakazi kujiepusha navitendo vya uvivu, utoro, wizi, ubadhirifu na utovu wa nidhamu. Wasipojiepusha na hayo

wanaifanya kazi ya kutetea na kulinda haki zao kuwa ngumu kwao na wadau wengine kama sisi.Lazima wakati wote tukumbuke kuwa kila haki ina wajibu.
Ajira na Utandawazi
Ndugu Rais wa TUCTA;
Katika risala yenu mmelizungumzia tatizo la ajira na kukumbusha umuhimu wa kulitafutiaufumbuzi. Nakubaliana nanyi kwamba lipo tatizo kubwa la ukosefu wa ajira hasa miongoni mwavijana na ni tatizo linalozidi kukua mwaka hadi mwaka. Tunalitambua tatizo hili na tunayo mikakati ya kukabiliana nalo. Tulifanikiwa katika lengo letu lakuongeza ajira milioni moja katika miaka mitano iliyopita. Na ukweli ni kwamba tulivuka lengokwa zaidi ya ajira
330,000
. Hata hivyo, tatizo ni kubwa sana kiasi kwamba mafanikio tuliyopatayamekuwa kama vile kuweka tone la maji baharini. Tunautambua ukweli huu na tumejipangakuendelea kukabiliana na tatizo hili. Lengo letu ni kufanya maradufu ya safari iliyopita.Niruhusuni nielezee mtazamo wetu na hatua tunazokusudia kuchukua kukuza ajira nchini.
Ndugu Wafanyakazi na Ndugu Wananchi;

Ajira zinaongezeka iwapo uchumi unakua. Yaani shughuli za uzalishaji mali na utoaji wa hudumazinapoongezeka ndipo watu zaidi wa kufanya kazi huhitajika na hivyo ndivyo ajira zinavyokuzwa.Ni muhimu tutambue pia kwamba kuongezeka kwa uzalishaji mali na utoaji wa hudumakunategemea kuongezeka kwa uwekezaji. Bila ya uwekezaji kuongezeka hakuna uzalishaji maliwala utoaji huduma utakaoongezeka na hivyo hakutakuwepo na ongezeko la ajira.
Ndugu Rais wa TUCTA na Ndugu Wafanyakazi;
Ndiyo maana Serikali yetu imekuwa inatoa msukumo maalum wa kuhamasisha na kuvutiauwekezaji nchini. Tunafanya hivyo kwa upande wa Serikali na ule wa sekta binafsi. Serikaliikiwekeza katika ujenzi wa shule, zahanati, barabara na miradi mingineyo, ajira huzalishwa wakatiwa ujenzi na baada ya ujenzi. Kwa mfano, ujenzi wa sekondari za kata na upanuzi wa shule zamsingi, licha ya kuajiri watu wengi wakati wa ujenzi, umewezesha walimu wapya
83,075
kuajiriwakatika miaka mitano iliyopita. Hivi sasa kuna nafasi wazi za walimu
74,996
zinazohitaji kujazwa.
Ndugu Rais wa TUCTA na Ndugu Wafanyakazi;
Kwa upande wa sekta binafsi, mikakati yetu inahusu kutengeneza mazingira mazuri kwawawekezaji wa ndani na nje kuwekeza vitega uchumi vyao nchini. Katika miaka mitano iliyopitamiradi ipatayo
3,881
yenye thamani ya kiasi cha dola za Marekani
milioni 27,330
ilisajiliwa katikaKituo cha Uwekezaji (TIC). Miradi hiyo ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezajiinategemewa kuzalisha ajira
444,343
. Bado uwekezaji kutoka nje ni mdogo ukilinganisha na fursaza uwekezaji zilizopo nchini. Ni dhamira yetu kuongeza juhudi ya kuvutia wawekezaji zaidi kujanchini na kuzalisha ajira. Madamu msukosuko wa uchumi wa mwaka 2009 na 2010 ulisababishakasi ya uwekezaji kupungua duniani na nchini umekwisha, matumaini ya kufanikiwa yapo.Lazima tuchemke kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
Ajira ya Wageni
Ndugu Rais wa TUCTA;
Katika risala yenu pia, mmelalamikia wageni kupata ajira zinazostahili kuwa za wananchi. Hayo nimakosa yanayosababishwa na watendaji katika mamlaka za utoaji wa vibali. NakuombaMheshimiwa Waziri Gaudencia Kabaka na namuomba Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha, Waziriwa Mambo ya Ndani kuhakikisha kuwa maofisa wahusika katika Wizara zenu wanatimiza ipasavyowajibu wao kuhusu suala hili. Ni dhambi kuacha Watanzania hawana ajira na kuwapendeleawageni pale isipostahili. Nawaomba wafanyakazi msichoke kutoa taarifa ili makosa hayoyarekebishwe.
Wawakezaji Wazawa
Ndugu Wafanyakazi;
Kwa wawekezaji wa ndani, mikakati yetu inalenga kutengeneza mazingira mazuri kwawajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa kuvutika na kuwekeza nchini kwao. Miongoni mwa

hatua ambazo tumekuwa tunachukua ni pamoja na kupunguza urasimu na kurahisisha taratibu zakupata leseni, kuanzisha miradi na kupata mikopo kutoka asasi za fedha.Kwa upande wa wajasiriamali wadogo, kwa sababu ya mazingira mazuri tuliyoyatengenezayamekuwapo mashirika kadhaa yanayotoa mikopo midogo midogo (
micro finance schemes
). Wengiwamenufaika. Na sisi Serikalini tumeendelea kuimarisha mifuko inayotoa mikopo yenye mashartinafuu kama vile Mfuko wa Vijana na Mfuko wa Wanawake na tumeanzisha Mfuko wa Uwezeshajiwa Wananchi Kiuchumi.
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi;
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mifuko hii imekopesha fedha nyingi kwa Watanzaniawengi ambao wamewekeza katika shughuli mbalimbali zilizozalisha ajira kwa watu wengi pamojana wao wenyewe kujiajiri.Kwa upande wa Mfuko wa Vijana, kwa mfano, SACCOS mbili katika kila Halmashauri na Manispaazote za Tanzania Bara ziliainishwa na kukopeshwa. Kwa ajili hiyo, jumla ya SACCOS
238
zilikopeshwa
shilingi bilioni 1.19
hadi Desemba, 2010. Mfuko wa Dhamana wa Mradi wa Usawa wa Jinsia na Ajira Bora kwa Wanawake ulitoa jumla ya mikopo yenye thamani ya
shilingi bilioni 1.23
kwa wajasiriamali
3,800
kupitia SACCOS za wanawake. Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchuminao uliweza kutoa mikopo yenye thamani ya
shilingi bilioni 45.44
ambapo wajasiriamali
72,113
walifaidika na SACCOS zipatazo
192
na vikundi vya uzalishaji mali na kiuchumi vipatavyo
86
vilifaidika na fedha hizo. Fursa nyingi za ajira zimezalishwa na mifuko hii, ndiyo maana ni sera yaSerikali kuiendeleza na kuongeza uwekezaji.
Ndugu Wananchi;
Tutaongeza fedha katika mifuko ya Serikali ili watu wengi zaidi wanufaike miaka ijayo. Aidha,tutaendelea kuboresha mazingira ili asasi za kutoa mikopo midogo ziongezeke, ziimarike nakunufaisha wengi. Hata hivyo, riba zinazotozwa na nyingi ya asasi hizi zinalalamikiwa kuwakubwa mno kiasi cha kuwakwaza wakopaji. Badala ya juhudi zao kuwa za kujinasua na umaskiniwanajikuta wanatumia muda wao mwingi na mapato yao mengi kuhangaikia kulipa riba yamikopo. Nawaomba wenye asasi zinazokopesha wasikilize kilio hiki kwa moyo wa huruma.Waangalie viwango vya riba na taratibu za malipo. Mkopaji kulipa kila wiki hakumpi nafasi yakujijenga na hivyo kushindwa kujikomboa na umaskini.
Wajasiriamali wa Kati na Wakubwa
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi na Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa wajasiriamali wa kati na wakubwa wa Kitanzania, tulielekeza nguvu zetu katikakuwajengea fursa na uwezo wa kukua. Tuliendeleza mifuko miwili maalum kwa ajili hiyo yaani
Small and Medium Enterprises Credit Scheme na Export Guarantee Scheme
. Aidha, kuanzia mwaka wa jana tulianza kuchukua hatua thabiti za kuijenga upya Benki ya Rasilimali ili irejee kufanya kazi yabenki ya uwekezaji kama ilivyokusudiwa ilipoanzishwa. Tuliipa mtaji wa
shilingi bilioni 50
natutafanya hivyo mwaka huu mpaka 2015. Dhamira yetu ni kuwapatia wawekezaji wazawa taasisiya fedha itakayowawezesha kupata mikopo ya muda wa kati na mrefu. Kwa ajili hiyo watawezakuwekeza katika shughuli za uzalishaji mali na huduma kama vile viwanda, mahoteli, kilimo,utalii, uchukuzi n.k.
Ndugu Wafanyakazi na Ndugu Wananchi;
Tayari watu wameanza kunufaika na mikopo hiyo na uwekezaji unaendelea na ajira zinazidikuzalishwa. Dhamira yangu ni kuona sekta nyingi na wajasiriamali wengi zaidi wananufaika namikopo kutoka Benki ya Rasilimali. Naamini juhudi hizi na zile ambazo tunazozielekeza kukuzakilimo zitaongeza sana ajira nchini katika miaka michache ijayo. Kwa upande wa kilimo, pamojana mikopo inayotolewa sasa kupitia TIB, tunategemea kukamilisha uanzishaji wa Benki ya Kilimokatika mwaka ujao wa fedha.Kuanzishwa kwa Benki hiyo itakuwa kichocheo kikubwa cha kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.Kilimo ndiyo sekta inayowaajiri Watanzania wengi kuliko zote nchini ingawa watu hawaoni kama

kujishughulisha na kilimo ni ajira. Hizi ni fikra potofu. Bahati mbaya sana vijana wengihawapendi kujishughulisha na kilimo kwa sababu ya mazingira magumu ya kazi hiyo nakuwaachia wazee wao. Naamini mageuzi tunayoendelea kufanya chini ya mkakati wa KilimoKwanza yakisaidiwa na Benki ya Kilimo itakayoanzishwa yataibadili hali hiyo na kuvutia watuwengi pamoja na vijana kujishughulisha nayo.
Ajira Katika Soko la Pamoja
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi,
Jumuiya ya Afrika Mashariki nayo inatoa fursa mpya za ajira kwa Watanzania. Utekelezaji waUmoja wa Forodha umekuza mauzo ya Tanzania katika nchi wanachama na hivyo kuchocheauzalishaji na ajira kuongezeka nchini. Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki iliyoanzakutumika tarehe 1 Julai, 2010 inafungua milango kwa bidhaa, mitaji, ajira na huduma kutoka nchiwanachama wa Jumuiya kutowekewa vikwazo vya kuvuka mipaka kwenda nchi nyingine.Hatua hii inatoa fursa kwa Watanzania kuweza kupata ajira katika nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Burundi. Hivyo hivyo na watu wa nchi hizo nao watapata fursa ya kuajiriwa katikanchi yetu. Tulichokubaliana kwa upande wa ajira ni kuwa kila nchi itaainisha ajira inazofunguakwa watu wa nchi wanachama kuweza kuajiriwa. Zoezi hili limeanza na linaendelea hivi sasa.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Hii ni fursa nzuri kwa Watanzania kupata ajira, tunachotakiwa kufanya ni kujipanga vizuri ilitunufaike na soko pana zaidi la ajira katika nchi hizo. Tunatakiwa kuangalia mitaala ya shule zetuna vyuo vyetu ili wahitimu wetu waweze kuwa na sifa za kupata ajira katika nchi za AfrikaMashariki. Kadhalika tuzingatie sifa nyingine muhimu za kufanya kazi kwa bidii, nidhamu nauaminifu. Naamini tunaweza kabisa kuwa hivyo na kufanya hivyo. Watanzania tunayo sifa yakumudu magumu mengi hata changamoto hii nayo tutaikabili na kushinda.
Maslahi ya Wafanyakazi
Ndugu wafanyakazi,
Kilio chenu cha kuboreshewa mishahara na kupunguziwa kiwango cha kodi tumekipokea kwauzito unaostahili. Jambo hili mlishalileta siku za nyuma na tumechukua hatua, tunaendelea natuaendelea kuchukua hatua. Tangu tuingie madarakani, Serikali yetu imekuwa inachukua hatuaza makusudi za kuboresha mishahara ya watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi. Kwamfano, kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kimeongezeka kutoka
shilingi65,000
kwa mwezi mwaka 2006 hadi kufikia
shilingi 135,000
kwa mwezi mwaka 2010. Hii ni sawana ongezeko la
asilimia 107
.Aidha, tumekuwa tunaboresha mishahara ya kada mbalimbali za utumishi wa umma kwamakundi yao. Hatua hizi zimepunguza kasi ya watumishi wa umma katika baadhi ya kadakuhamia sekta binafsi na hata wale waliohama kurudi. Mkakati huo tutauendeleza kwa kadaambazo hatujazifikia bila kusahau wale tuliokwishawafikia kuwaboresha zaidi.
Ndugu Rais wa TUCTA na Ndugu Wafanyakazi;
Kwa upande wa sekta binafsi, hatua yetu ya kuhakikisha kuwa Bodi za Mishahara za Kisektazinaundwa na kufanya kazi imeanza kuzaa matunda. Kima cha chini kimepanda kutoka
shilingi48,000/=
kwa mwezi hadi
shilingi 80,000/=
mpaka
shilingi 300,000/=
kutegemea na aina ya shughuliafanyayo mwajiri.Vile vile, katika miaka mitano hii, kodi ya mapato imepunguzwa kutoka
asilimia 18.5
hadi
asilimia14
na VAT imeshuka kutoka
asilimia 20
hadi
asilimia 18
. Hatua zote hizo zimeleta nafuu ya kiasifulani.

Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi;
Pamoja na hatua hizo bado mishahara ya wafanyakazi nchini ni midogo ukilinganisha na gharamaza maisha. Tunatambua hoja na haja ya kuendelea kuongeza mishahara mwaka hadi mwakampaka tufikie pale tunapotaka sote tufike, yaani mshahara wa kumudu gharama za maisha.Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna upungufu wa dhamira wala utashi wa kisiasa wa kufanyahivyo, kwa upande wangu binafsi au wa wenzangu Serikalini. Yale tuliyoyafanya katika miakamitano iliyopita ni uthibitisho tosha wa ukweli huo. Ahadi ninayopenda kurudia tena leo ni kuwatutaiendeleza kazi tuliyoianza mwaka hadi mwaka. Hata hivi sasa katika mchakato unaoendeleawa kutayarisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha, wahusika wanaangalia namna ya kupandishakima cha chini cha mashahara na nafuu nyinginezo.
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi;
Uwezo wa kimapato wa Serikali ndiyo kikwazo kinachotupunguzia kasi ya kuboresha mishaharaya watumishi wa umma. Wakati wote tumekuwa tunajikuta tupo katika mtihani kuhusu kuwekauwiano mzuri baina ya matumizi ya mishahara na matumizi kwa ajili ya shughuli nyinginezo zaSerikali. Busara inaelekeza kuwa kiasi cha fedha zinazotumika kulipa mishahara kisiwe kikubwamno na kubakiza kiasi kidogo kwa ajili ya Serikali kutekeleza majukumu yake mengine yautawala, ulinzi na usalama, maendeleo na utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi wake.Changamoto kubwa tuliyonayo ni jinsi ya kuongeza zaidi mapato ya Serikali ili tuwe na fedha zakutosha kuwalipa wafanyakazi mishahara inayokidhi gharama za maisha na kubaki na pesa nyingizaidi kwa Serikali kuendesha shughuli zake na kuhudumia wananchi wake. Katika miaka mitanoiliyopita tumefanya juhudi kubwa ya kuongeza mapato ya Serikali na tumepata mafanikioyanayotia moyo. Mapato yameongezeka kutoka wastani wa
shilingi bilioni 177.1
kwa mwezimwaka 2005 hadi
shilingi bilioni 390.7
kwa mwezi mwaka 2010.
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi;
Mafanikio hayo ndiyo yaliyotuwezesha kuongeza mishahara kwa kiasi tulichofikia sasa. Hivyobasi, jawabu la tatizo lipo katika kuongeza zaidi mapato ya Serikali. Hiyo ndiyo dhamira yetu natumejipanga kimkakati kufanya hivyo. Ndiyo maelekezo yangu ya msingi niliyoyatoa kwawenzetu wa Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato nilipowatembelea mwezi Februari, 2011.Kinachotakiwa ni wafanyakazi wenzetu katika asasi hizo kufanya kazi kwa bidii na uaminifu nawalipa kodi kuwapa ushirikiano.
Ndugu Rais wa TUCTA;
Nafurahi kwamba katika risala yenu mmetoa mawazo mengi mazuri kuhusu namna ya kuongezamapato ya Serikali, kubana matumizi na kuboresha mishahara ya wafanyakazi. Mawazo yenuyanashabihiana sana na mawazo yetu na baadhi ya mambo tunayofanya na tunayoyafikiriakuyafanya katika kuboresha mapato ya Serikali na maslahi ya watumishi wa umma. Tupeninafasi tukayafanyie kazi.
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi;
Nimeagiza pia kuwa Serikali yetu ianze kufikiria mambo mbalimbali yatakayowanufaishawafanyakazi na kuinua hali zao za maisha. Hususan nimeagiza tuangalie uwezekano wawafanyakazi kupata mikopo ya gharama nafuu watakayoitumia kununua au kujenga nyumba aukununua vyombo vya usafiri au vyombo vya nyumbani. Tumekuwa tunatoa mikopo kwaWaheshimiwa Wabunge, sasa tufanye hivyo kwa watumishi wa Serikali nao. Nafurahi kuwaAzimio la kuanzisha mfuko wa mikopo ya watumishi wa umma lilipitishwa na Bunge katika kikaokilichopita.Vile vile, nimeagiza tutoe kipaumbele kwa ujenzi wa nyumba za kuishi watumishi wa umma hasawale wa vijijini na vyombo vya ulinzi na usalama ili tuboreshe mazingira yao ya kazi. Ni kaziambayo tunaifanya hivi sasa ila tunataka tuipe msukumo mkubwa zaidi.

Wafanyakazi wa Sekta Binafsi
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi;
Kwa upande wa wafanyakazi katika sekta binafsi, tutaendelea kusimamia Mabaraza ya Mishaharaya Kisekta ili yafanye kazi zake ipasavyo na kuhakikisha kwamba maslahi ya watumishi katikasekta hiyo yanaboreshwa. Kwa hatua tulizokwishazichukua tangu yaundwe, mafanikio yakeyameanza kuonekana. Hata hivyo, wafanyakazi wangeweza kunufaika zaidi. Naambiwa kwambawafanyakazi wengi katika sekta binafsi wapo katika mazingira magumu. Wapo wengi ambao nivibarua wa kutwa na wengine wako hivyo kwa maisha yao yote. Aidha, wanapata ujira mdogo.Waajiri wanakwepa wajibu wao stahiki kwa wafanyakazi wao ambao ndiyo wanaofanyawatajirike. Kuwasaidia wafanyakazi kudai na kupata haki zao ni moja ya agenda muhimu zaSerikali yetu. Naomba vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi tusaidiane na kushirikiana katika jambo hili. Haya ni mapambano yetu sote. Tukishirikiana na kusaidiana tutashinda.
Kuboresha Pensheni/Malipo ya Uzeeni
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Wafanyakazi,
Nawashukuru sana kwa maneno yenu ya pongezi kuhusu hatua tulizochukua juu ya kurekebishana kuboresha mafao ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Nami nafurahi kwamba, liletatizo la mafao ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaaam waliokuwa katika mfumo waSSSS tumelipatia ufumbuzi. Wafanyakazi hao sasa wameingizwa katika mfumo wa PPF kamawenzao wengine. Kwa ajili hiyo Serikali italipa shilingi
bilioni 9.46
kufidia michango ambayohaikuwahi kulipwa ili ndugu zetu hawa waweze kulipwa mafao yao chini ya mfumo wa PPF. Jambo la pili ni kuwa nafurahi Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamiiimekwishaundwa na imekwishaanza kazi. Tena wameanza vizuri. Kupitia mamlaka hii sasamasuala yahusuyo afya ya mifuko, uwianishaji wa mafao baina ya mifuko na uboreshaji wa mafaoyatapatiwa ufumbuzi wa uhakika na kwa wakati. Chombo hiki ni kipya, lazima tukiunge mkono.Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu wa kukilea. Naomba vyama vyawafanyakazi na mifuko ya hifadhi kukipa ushirikiano unaostahili ili kiweze kufanikisha majukumuyake ipasavyo.Kuhusu mchakato wa Katiba, napenda kuwahakikishia kuwa hakuna atakayebaguliwa. Tunatakawatu wote wapate fursa ya kushiriki. Jipangeni kushiriki kwa ukamilifu. Tusiruhusu watuwachache wanaotaka kuhodhi mjadala huu kwa kutaka maoni yao tu ndiyo yasikilizwe nakuwazuia wengine wasitoe maoni yao. Tukiruhusu tabia hiyo huenda tusipate Katiba ambayoitawakilisha maoni ya wengi bali kikundi fualni kilicho hodari kupiga kelele bila hoja.
Hitimisho
Ndugu Rais wa TUCTA, Ndugu Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi na Ndugu Wafanyakazi;
Nimezungumza kwa muda mrefu. Nimejitahidi katika hotuba yangu kutoa maelezo ya ufafanuzikwa takriban kila jambo lililotajwa katika risala yenu. Yapo baadhi ambayo sikuyazungumzialakini siyo kwamba nimeyapuuza. Kila jambo mlilolitaja tutalifanyia kazi. Nia yetu ni kujenga nchiyetu na katika kufanya hivyo natambua kuwa wafanyakazi ni mhimili muhimu sana. Ni wajibuwetu kuwasikiliza, ni wajibu wetu kushirikiana nanyi na ni muhimu kushughulikia musuala yenuipasavyo. Kila mmoja wetu anamuhitaji mwenzake. Narudia tena kuwahakikishia ushirikianowangu binafsi na ule wa wenzangu wote Serikalini wakati wote.Naomba nimalize kwa kusema kuwa kwa ushirikiano na mshikamano baina ya utatu wetu, yaani
Wafanyakazi, Waajiri na Serikali
hakuna litakalotushinda na hakuna mfanyakazi wa Tanzaniaatakayekuwa mtumwa katika nchi yake.
 
kweli jambo usilolijua niusiku wa giza. hakunajipya ni story to tena ni uhuni ambao hata mtoto wa primary anaweza gundua hatuna mtu hapo. nitarudi baadaye:israel:
 
Back
Top Bottom