Rais Kikwete 'hakuwa na jinsi'

Rais Kikwete 'hakuwa na jinsi'

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,006
Jana ilimpasa kuhudhuria,kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa na kuhutubu vile. Mh. Rais,kwa sauti na namna wananchi walivyokuwa kimya muda mwingi,hakuridhishwa na mchakato na mambo fulani kutokuwepo kwenye Katiba inayopendekezwa.

Rais alionesha dhahiri kutoufurahia mchakato kwa kumwaga misemo na rai za mara kwa mara juu ya kila jambo kuwa na muda wake na kadhalika. Akadokeza na mkutano wake na TCD bila ya kupunguza kilichoripotiwa.

Rais akagusa akidi. Takwimu ikatolewa. Akaithibitisha akidi. Hakuwa na jinsi. Rais amepokea kilicho tayari. Kisingeweza kubadilishwa Jamhuri Dodoma.

Pamoja na kauli mbalimbali za jana,waelewa wamejua kuwa Rais hakufurahia mchakato. Hata kura ya maoni amesita kuitamka moja kwa moja. Mh. Rais alikuwa pale kupokea tu. Hakuwa na nafasi ya kusema au kufanya vinginevyo. Hakuwa na jinsi.

Wananchi wanauliza,mbona wawakilishi wote wa jana ni 'wetu' kama chama tawala?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Hivi maraisi wastaafu walihudhuria sherehe zile?
 
Raisi wa nchi "Hakuwa na jinsi"...? Lol udhaifu gani huu
 
Mimi Si mwana CCM lakini dharau wanazomfanyia Kikwete Viongozi wenzie si sawa. Yeye kawapa heshima ya madaraka waliyo nayo, pia kawapa uhuru wa kutekeleza majukumu katika madaraka aliyowapa wao wanaona ni udhaifu na kumdharau.

Kwa makusudi wakamnyang'anya madaraka ya kuwa na usemi wowote kwenye bunge la katiba zaidi ya kuipokea tu. Hii ni dharau kubwa kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Kikwete bado ni Raisi kwahiyo ana uwezo wa kuchukua hatua kali. Baba akidharauliwa watoto wanafedheheka.
 
Kikwe.te ni dhaifu sana hana uwezo wa kumwajibisha LAU katibu tarafa, udhaifu wake mkubwa sana
 
Hapa inathibitisha kwamba misemo yote ya wahenga ilibeba maana nzito kuliko inavyoweza kuonekana kwa nje. Nyerere alimkataa kikwete na lowasa mchana kweupe kwamba hawafai kuwa maraisi. Kwa ujinga watanzania hasa wasukuma wa pumbavu na waatu wa kanda ya ziwa, wakajazana kwenye treni kwenda dodoma wakiwa na misimamo ya kumpa kikwete.

Kikwete ambaye hata report ya kamati ya nidhamu haikuwekwa hadharani, akapewa Tanzania, pamoja na Mwalimu kuwa amemkataa!. Sasa mnayaona haya? Raisi eti hana jinsi.. Si wehu huu? "Mdharau mwiba humchoma", na "asiyesikia la mkuu huvunjika guu"... Tanzania sasa mnaiona ilipo????

Lakini bado dawa iko mikononi mwa Watanzania. Katiba hii haijapitishwa bado. . Tuungane na Askofu Ngalalekumtwa, na waislam wa Shura ya maimamu, Ukawa na Wananci wote wasio maccm, tupige kura ya hapana kwa kili katiba nyang'au na kuiondoa ccm madarakani bila mizaha.

Ujinga huu wa akina chenge, sita, na unafiki wa jk, huku watanzania tukiteketea, hauwezi kuachwa ili taifa liangamie.

Katiba ikipigiwa kura itapita utake usitake. CCM utawazidi kwa hoja lakini huwezi kuwazidi katika mbinu za wizi wa Kura.

hivyo Raisi aendelee na msimamo wake kuwa Katiba iwe mwaka 2016. Na Raisi ahakikishe ana usemi wa nani atamridhi kiti chake. hawa wanaomdharau wasiwe wamemshamyang'anya hata maradara ya kumuandaa mrithi
 
Back
Top Bottom