Rais Kikwete azuia mawaziri kutoka nje ya Dar

Elisante Yona

Senior Member
Oct 6, 2009
130
24
MAWAZIRI wote wamezuiwa kusafiri kikazi nje ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kile kinachoelezwa ni maandalizi ya kukabidhi ofisi kwa mawaziri wapya ambao wanatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Taarifa hizo zimekuja siku moja tu tangu Ikulu kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salvatory Rweyemamu, kuwataka Watanzania kuwa na subira kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete wakati wowote kuanzia sasa atatoa uamuzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Profesa Muhongo na baadhi ya viongozi wengine wa Serikali, wanahusishwa na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow

Endelea kufuatilia,
 
Ondoa bangi mkuu kama umekosa la kuongea tupishe kwa sasa simbachawene yuko Tabora.
 
Kaona bunge linaanza ameamua kuleta maigizo, mbona kibaka mkuu wa escrow yuko Davos ambako ni nje ya nchi.

Ila Lema, Sugu na Nassari wangekomesha Jumanne kwa kumtoa nje kinguvu mwizi na mwongo Muhongo. Natamani asibadili baraza au amuache Mr Escrow Muhongo ili aone nguvu ya umma
 
Jaman, muheshimiwa rais hawez tena kuvunja baraza Hilo, Kwan lote linavuja, na hana vifaa wala spear mpy zote ni zilele
 
sasa hivi watakua wanapishana Bagamoyo kwa waganga wa kienyeji kupata tunguli za kulinda nafasi zao...
 
Back
Top Bottom