Rais Kikwete azindua Uchimbaji wa Madini ya Urani

Rais Kikwete azindua Uchimbaji wa Madini ya Urani

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,061
Reaction score
64,209
Rais JAKAYA KIKWETE ameweka jiwe la msingi na kuzindua rasmi mradi wa uchimbaji wa madini ya Urani katika Mto Mkuju Mkoani Ruvuma.

Anategemewa pia kuzungumza na wananchi wa Ruvuma katika uwanja wa michezo wa Majimaji Songea, ambako pia atapata fursa ya kuwaaga wananchi wa Ruvuma baada ya kumaliza muda wake wa miaka 10 kama mkuu wa nchi.
 
huyu jamaa kweli ameanza kutapa tapa,cha kwanza alitakiwa kuwa kwenye kampeni za kumnadi JPM,huku kila siku anajidai anzindua miradi,mara kiwanja cha ndege,mara daraja,mara flyover mara gesi,mara uranium yaai ndani ya wiki mbili amzindua miradi yenye mikataba feki kibao,anafanya yote haya kwa faida ya nani?nilidhani alitakiwa asubiri serikali itakayokuja ili iweze kufanya hayo mambo maana yeye ameshachemsha alikuwa muda mwingi yuko nje ya nchi sasa imekula kwake,na aende tu kwa kweli we are fed up with him
 
Huyu jamaa anafanya yote haya ili Lowassa akiingia aanze kusema OOH ikikuwa plan ya serikali ya awamu ya nne! Ni aibu kwa taifa serikali haiwekezi popote!
 
Rais JAKAYA KIKWETE ameweka jiwe la msingi na kuzindua rasmi mradi wa uchimbaji wa madini ya Urani katika Mto Mkuju Mkoani Ruvuma.

anategemewa pia kuzungumza na wananchi wa Ruvuma katika uwanja wa michezo wa Majimaji , ambako pia atapata fursa ya kuwaaga wananchi wa Ruvuma baada ya kumaliza muda wake wa miaka 10 kama mkuu wa nchi.

Uko Tanzania gani?kashazindua na juzi kashindwa kuongea nawakazi ruvuma hakutokea Jana ndio amekuja nakuelekea namtumbo tu
 
Huyu jamaa nahisi hadi jumapili ya kesho kutwa siku ya uchaguzi atafungua mradi mwingine mpya... We mzee kubali tu matokea muda ushakutupa mkono
 
Lowassa akiingia tu... TUNAVUNJA VUNJA MIKATABA FEKI YOOOOTE... we do REVISION ya hiyo mikataba...kama ina profits kwa TAIFA au la... but 100% we are confident HAINA FAIDA KWA TAIFA..!! After Lowassa, UKAWA wakishinda tu, wataifanyia REVIEW ya haraka sana kuona jinsi ya KUIVUNJA NA KUIANZA UPYA...!!!

Kila kitu kinamalizwa nchi hii...!!!
 
Ilifata taratibu zote?
Kwanini wamepelekesha kwa kasi sana miradi mingi?
UDA hadi leo haijaanza
 
Ilifata taratibu zote?
Kwanini wamepelekesha kwa kasi sana miradi mingi?
UDA hadi leo haijaanza

Pengine nauli yaweza ku-affect uchaguzi. Kulikuwa na tetesi za viwango vya nauli ambavyo kama ni kweli wananchi wanaweza kulalamika na kuona mradi haufai.
 
Anazindua mradi wa uchimbaji je usalama wa wananchi umeishazingatiwa? kwani hayo madini ni hatari sana sasa isije ikawa yeye anacho angalia ni manufaa yake na familia yake wamepata nini na sio watanzania.
 
Taarifa za kisayansi zinaonyesha kuwa uchimbaji wa madini ya urani una madhara makubwa ya kiafya ikiwa ni pamoja na saratani ya ini, mapafu, ubongo pamoja na mfumo wa uzazi. Angalia hapa

 
Habakizi kitu Huyu ms..n..ge.Ni kama vile ana aleji na madini ya TZ.Akisikia sehemu yoyote TZ kuna madini yeye anaita wazungu fasta.CCM lazima waondoke tu madarakani watuachie nchi yetu.Imewashinda wallah.
 
huyu jamaa kweli ameanza kutapa tapa,cha kwanza alitakiwa kuwa kwenye kampeni za kumnadi JPM,huku kila siku anajidai anzindua miradi,mara kiwanja cha ndege,mara daraja,mara flyover mara gesi,mara uranium yaai ndani ya wiki mbili amzindua miradi yenye mikataba feki kibao,anafanya yote haya kwa faida ya nani?nilidhani alitakiwa asubiri serikali itakayokuja ili iweze kufanya hayo mambo maana yeye ameshachemsha alikuwa muda mwingi yuko nje ya nchi sasa imekula kwake,na aende tu kwa kweli we are fed up with him




mfa maji haachi....
 
Huyu jamaa nahisi hadi jumapili ya kesho kutwa siku ya uchaguzi atafungua mradi mwingine mpya... We mzee kubali tu matokea muda ushakutupa mkono
Jk mzee wa kuzinduaa
dr bilal mzee wa kukata utepe tu
 
Hivi kuna uharaka gani wa kuzindua miradi hiyo sasa?
Kwani the coming prezdaa hawezi kuifungua hyo miradi? Nina mashaka na mikataba yao
 
Lowassa akiingia tu... TUNAVUNJA VUNJA MIKATABA FEKI YOOOOTE... we do REVISION ya hiyo mikataba...kama ina profits kwa TAIFA au la... but 100% we are confident HAINA FAIDA KWA TAIFA..!! After Lowassa, UKAWA wakishinda tu, wataifanyia REVIEW ya haraka sana kuona jinsi ya KUIVUNJA NA KUIANZA UPYA...!!!

Kila kitu kinamalizwa nchi hii...!!!

Hii inaitwa nyanganya rafiki zake, wape rafiki zangu
 
Back
Top Bottom