Hebu soma vizuri mleta mada, alicho kisema amiri jeshi mkuu hapa chini.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete
amelikata Jeshi la Polisi nchini kujiandaa
kikamilifu ili kukabiliana na vurugu zozote
zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji
wapigakura, upigaji Kura ya Maoni ya
kupitisha Katiba Inayopendekezwa na
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Akifunga mafunzo ya maofisa warakibu
wasaidizi katika Chuo cha Taaluma ya
Polisi, Dar es Salaam jana, Rais Kikwete
alisema dalili zinaonyesha kwamba kuna
watu wenye nia ya kuhatarisha amani
katika matukio hayo.
Tunayoyasikia na tunayoyaona
yanaashiria kuwapo kwa dalili za wenzetu
kukwamisha shughuli hizi za kitaifa kwa
kufanya vurugu, Jeshi la Polisi jiandaeni na
vitendo vyote vitakavyofanywa kwa lengo la
kuhatarisha amani, alisema akijibu
maombi ya kupatiwa vifaa
yaliyowasilishwa kwake na Mkuu wa Jeshi
la Polisi, IGP Ernest Mangu.
Alisema Serikali itahakikisha kazi ya
uandikishaji katika daftari la wapigakura,
upigaji wa kura ya maoni na uchaguzi
mkuu vinafanyika kwa amani na utulivu
kwa gharama zozote.
Alisema ili kufanikisha kazi hiyo, Serikali
italiwezesha Jeshi la Polisi ili litekeleze
kikamilifu majukumu yake ya kulinda
amani na utulivu.
Tutawawezesha kwa kuwapa vifaa ili
kuhakikisha mnafanya kazi yenu ya
kutunza amani kwa umakini zaidi, alisema
Rais Kikwete anayemaliza muda wake wa
mihula miwili ya urais baada ya uchaguzi
mwaka huu.
Iwapo mambo yote yatakwenda kama
yalivyopangwa, Kura ya Maoni ya Katiba
Inayopendekezwa itapigwa Aprili 30 wakati
Uchaguzi Mkuu utafanyika Oktoba.
Profesa Lipumba apinga
Akizungumzia kauli hiyo ya Rais Kikwete,
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba alisema, Rais Kikwete yeye ndiye
mtu wa kwanza kuivuruga amani kwa
kutangaza tarehe ya kufanyika kwa kura ya
maoni wakati siyo jukumu lake na jukumu
hilo ni la NEC, Serikali yake kushindwa
kuratibu vyema mchakato wa uandikishaji.
Kama uandikishaji hauendi vizuri mpaka
sasa, anavunja sheria za nchi halafu yeye
mwenyewe tena anakwenda kwa vyombo
vya dola na kuvieleza vijiandae wakati yeye
huyohuyo ndiye ameanzisha uvunjifu wa
amani tunashindwa tumweleweje, alisema.
Profesa Lipumba alisema kinachotakiwa
kufanyika kwa sasa ni NEC kutangaza
tarehe kamili ya uchaguzi na uandikishaji
uende kwa utaratibu tofauti na ilivyo sasa
kwa mkoa mmoja wa Njombe kusuasua
mambo ambayo yanaashiria uvunjifu wa
amani.
www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/2663670/-/s3m51ez/-/index.html