Rais Kikwete awaambia Polisi wakae mguu sawa

Rais Kikwete awaambia Polisi wakae mguu sawa

Haki za wale raia-wananchi waliowachagua viongozi wao ipo wapi?.Nnakuuliza hivi kwa sababu wale viongozi waliosimikwa kimabavu wananchi wamewatenga na hawana ushirikiano nao kwa namna yeyote ile kiasi swali hilo lilielekezwa kwa Wizara husika kuwa maendeleo ya maeneo husika yanakujaje ikiwa ni pamoja na kutekeleza shughuli zote za kiserikali?.

CCM kwa matendo yenu na maneno yenu mnatugawa wananchi hata ule umoja wetu tena hatuna,demokrasia ya aina hii ya kulazimishiwa viongozi tusiowataka hatuitaki na haifai tena wakati huu.

Msitulazimishe kupokea katiba haramu mliyoitunga kwa maslahi yenu tena ikaandikwa na watu wachafu,hatutaki kabisa tunasema hatutaki.

Tutakapoamua kufanya fujo hakuna majeshi ya kutosha na hatutaki kufikia huko na msitulazimishe kufika huko mbona hamtuelewi lakini?

Waacha porojo wewe, wasimikwe watu kimabavu na nyie mkae kimya tu? mahakama hamzijuwi?
 
Rejea Bandiko langu Ustazant ... Nimesema Amiri Jeshi ni jukumu lake kuandaa vikosi vyake ili ziwe na uwezo wa kukabiliana na shari yoyote itakayojitokeza... Ila kwa Amiri Jeshi kuandaa Vikosi vyake kukabiliana na Udhaifu mapungufu ya Tume ya Uchaguzi, au kuandaa kubaka Demokrasia ni Udhaifu uliopitiliza!!! Sidhani kama JK anapenda kuona sifa yake inaharibiwa dakika za Mwisho!!! Unless wamemnukuu vibaya ... sikutegemea kauli kama hii kutoka kwa amiri Jeshi Mkuu!! Nani asiejua Udhaifu wa Katiba inayopendekezwa? nani asiejua kuwa BVR zimeshindwa kuwaandikisha wapiga kura? nani asiejua kuwa Muda wa kupiga kura imekaribia sana na tume kwa vyovyote vile haitaweza andikisha wapiga kura? nani asiejua kuwa CCM mwaka huu wana hali mbaya sana!! Kauli hii italeta maafa kwa Raia ambao mara zote huonewa na police ..

Hizo sasa ni porojo bila mpango.

Rais anatayarisha polisi kupambana na hali yoyote ya uvunjifu wa amani utakaojitokeza. Hayo sijuwi ya nani, nani, nani ni kubwabwaja na kuhororoja bila mpango.

Ulitaka Rais asiamuru Polisi kujiandaa kukabiliana na hali yoyote ya uvunjifu wa amani wakati wa michakato hiyo?

Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
 
embu tujuzana katika hili kwa nini tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao presha inawapanda ajabu na muda wote wapo karibu zaidi na vyombo vya dola,polisi na JWTZ. kuna siri gani hapa? au ni kuwatisha wapiga kuwa hili wasiwachague wapinzani? mfano mzuri juzi rais alipowambia polisi wajiandae andae. karibuni.
 
Ndo walewale wanaosema wapigwe tu. Na kweli naona kila kona ya tz wananchi anashugulikiwa kweli na police. But police hawatakuwa kwenye dakika ya kutumbukiza kura zetu kwenye sanduku la kura
 
Hiyo ni hali ya viongozi ambao imani zao zimekufa sasa kutokana na hofu wanatumia nguvu kubaki madarakani.
 
Huyo Amiri Jeshi wa majeshi yote ya Tanzania na Rais wa Tanzania, si wangu pekee - Kumbuka hilo.

Kwanini asilitayarishe jeshi la polisi kukabiliana na chochote kinachoweza kutokea?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga.

Kwani angemwachia Mangu aongee na jeshi lake isingeeleweka?
 
Kwani angemwachia Mangu aongee na jeshi lake isingeeleweka?

Rais anapoongea na kuwajulisha umma ina maana kubwa zaidi, anataka na sisi tuelewe kinachojiri.

Sasa kama mlipanga kufanya fujo muelewe kuwa vijana wanatayarishwa kulinda usalama wa raia kwa namna yoyote ile.

Upo hapo ulipo?
 
Hapa nilipo sipo nimetoka.
Ngoja nikale kwanza nakuja kukujibu sasa hivi njaa iko tumboni


Rais anapoongea na kuwajulisha umma ina maana kubwa zaidi, anataka na sisi tuelewe kinachojiri.

Sasa kama mlipanga kufanya fujo muelewe kuwa vijana wanatayarishwa kulinda usalama wa raia kwa namna yoyote ile.

Upo hapo ulipo?
 
Back
Top Bottom