Rais tajiri na chama tajiri hawezi kung'ania ikulu, kwani wana cha kufanya lakini masikini wanafikiria njaa wataipeleka wapi? Matajiri wanataka kuandika historia ya kuifanya nchi yao tajiri na inayoheshimika duniani, na wabaki kwenye kumbukumbu za dunia, jiulize wapi kuna kumbukumbu ya masikini mwa mwisho duniani alikufa lini? au raisi aliyeingia madarakani na kuifanya nchi yake masikini utamsoma ktk kitabu gani duniani? Hata nyerere hana umaarufu kama Mandela kwa sababu ya umasikini, aliiacha nchi ikiwa masikini, alikua na nafasi ya kuifanya nchi iwe tajiri, ndio maana alifia uingereza kwa maadui zake, Mandela alifia nchini mwake kwa wananchi wake, ukiwa na akili ya kutosha utafikiria nikwanini? Ukiwa na rafiki masikini utakua masikini! Rafiki wa nyerere ni mchina,kiuba na mrusi na atikadi za kijamaa, wao wakazikimbia mapema yeye akaendele kuzikumbatia, sijaona mahali popote akiliongelea kosa hilo,kiuba ndio wanastuka sasa, Tunahitaji chama chenye itikadi nyingine na viongozi wenye itikadi ya utajiri, na wanotaka nchi na wanachi waheshimike kimataifa na sio kuomba kama wakoma kila siku.
Zuma walimshangaa kuongea na sim wakati Obama anakuja kumsalimia, alikua na uthubutu huo kwani nchi yake sio masikini, kama angekua raisi wa nchi masikini angeitupa mbali haraka, hayo ndio maisha ya tajiri,
kama wewe ni masikini au kipato kidogo, jitahidi umvishe mtoto wako vizuri siku moja na mpeleka mtoto wako sehemu ya kuchezea watoto wenye pesa za juu kidogo kukushinda na kaa pembeni ndio utajua umasikini ni maisha mabaya, unatakiwa upigane kufa na kupona usiwe masikini na famila yako isiwe masikini na kama kuna mtu anafanya chochote kukusabishia umasikini utapigana naye kwa nguvu zako zote.