Rais Kikwete anavunja Baraza la Mawaziri lini?

Nimekuwa nikiellewa kuwa raisi huvunja baraza la mawaziri kabla ya kampeni naomba kupata jibu kwa mwenye uelewa kwanini baraza la mwaziri safari hii limechelewa kuvunjwa??
 
Emma hulijui hata gazeti la serikali?

Mm nazani anajua ndomana kauliza coz ili uwe waziri nilazima uwe mbunge ss kamabunge lilishavunjwa wazili anatokawapi tena nitarajia makayibu wakuu ndo wangefanya kazi za wizara ss
 
Hapa ndio ile maana ya Waziri anaweza kutokuwa mbunge. Sasa bunge kama limevunjwa maana yake ni kwamba na uwaziri una-dissolve kwa kuwa huwezi kuwa waziri pasina ubunge. Hii nchi imekorogwa sana. Tubadilishe kila kitu. CCM ni madikteta na mabwanyenye.
na mimi nilikuwa najiuliza hii ishu. kikatiba hawa jamaa siyo mawaziri.
 
Wakuu nashindwa kuelewa nini mantiki ya rais wangu kuto kulivunja baraza la mawaziri, tunamaliza wiki sasa tangu kampen ianze mawaziri wanatumia nafasi za uwaziri wao kuomba ubunge na wengine wanatumia uwaziri wao kuombea u rais. Na bunge halijavunjwa mpaka sasa licha ya ahadi Kuwa litavunjwa tarehe 20/8/2015 lakin mpaka sasa wabunge wanautumia ubunge wao kuusaka ubunge hivi nchi hii ninani katurogaaa

Usilie lie. Katiba inasemaje kuhusu hilo?
 
wakuu nashindwa kuelewa nini mantiki ya rais wangu kuto kulivunja baraza la mawaziri, tunamaliza wiki sasa tangu kampen ianze mawaziri wanatumia nafasi za uwaziri wao kuomba ubunge na wengine wanatumia uwaziri wao kuombea u rais. Na bunge halijavunjwa mpaka sasa licha ya ahadi kuwa litavunjwa tarehe 20/8/2015 lakin mpaka sasa wabunge wanautumia ubunge wao kuusaka ubunge hivi nchi hii ninani katurogaaa
kweli ukawa mna mambo. Wewe ndio mfano wa mashabiki bogus ukawa waliokuwanao. Nani kakwambia bunge bado lipo? Kama lipo tueleze linakutana tena lini? Nyie ndio mazombie mnapiga kelele mtashinda uchaguzi...hata facts ndogo tu hauna. Hopeless my brother.
 
jamani muwe mnajaribu kusoma, bunge lilishavunjwa kwa mujibuwa tangazo la serikali katika gazeti la serikali.

Mkuu magufuli anakagua barabara akiwa kwenye kampeni! We huna habari.

Kusoma hujui hata kutazama picha inakushinde??
 
jamani hakuna tena mwenye sifa ya kuwa waziri lakini mbona wanaendelea kukaa ktk ofisi za umma?..tindu lissu uko wapi.magufuli anazunguka kama waziri wa ujenzi uko mikoani...ukawa mnafanya nini kwanini hamkeemei hili suala.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ibara ya 57(2)

(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-

(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo;
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 57(2)

(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-

(b) Ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;

(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo;
 
Ilisemwa kuwa litavunjwa tarehe 28 August lakini mpaka sasa bado.
Mawaziri wanagombea ubunge!
Ni lini hasa baraza la mawaziri linapaswa kuvunjwa?
Na ni sababu zipi zinazoweza kusababisha rais kuchelewa kulivunja baraza la mawaziri?
Naomba msaada.

Mkiitwa wapumbavu mnasema mmetukanwa, ni lini umesikia nchi inaweza kukaa bila kuwa na serikali?ni nchi gani inayofanya hayo?

Baraza la Mawaziri litavunjwa siku utawala wa Kikwete utakapoisha, yaan Rais Mpya anapoapishwa
 
Mawaziri au manaibu waziri wataacha kuwa mawaziri pale ambapo Rais Mteule atakapokuwa ametangazwa na kabla ya kuapishwa kwake.

Hiyo ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 57(2).

(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki dunia;
(b) ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;
(c) ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini mwenye madaraka hayo;
(d) iwapo atachaguliwa kuwa Spika;
(e) iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;
(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo;
(g) iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha kwamba amevunja sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 
baharia Ar

Nakwambia hili la baraza la mawaziri kutokuvunjwa nahisi ni kwamba kuna kitu kinachoendelea..........haikubaliki hata kidogo kodi ya Wananchi iendelee kutumiwa kuwalipa mishahara watu ambao inajulikana kabisa muda wao umeshakatika

Ila Mi naweza kusema ya kwamba kuna janja anaeleza mkwe......re lakini safari hii WATAISOMA NAMBA•••••••••••••••!

Hii inaitwa hawajui na hawajui kuwa hawajui, soma katiba inasemaje kabla ya kuleta maneno mengi ambayo kumbe ni sababu tu hujui.
 
Last edited by a moderator:
bunge likivunjwa automatically kunapaswa baraza la mawaziri kuvunjwa maana kunakuwa hakuna mwenye sifa ya kuwa waziri, tunashuhudia mwendelezo wa dharau za watawala.

Soma katiba yako uelimike
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom