Ofisi ya Rais ina mawaziri na manaibu kibao, kuna makamu wa Rais ambaye na ofisi yake ina mawaziri na manaibu na wakurugenzi. Kuna Ofisi ya waziri mkuu ambayo pia ina mawaziri na manaibu na wakurugenzi kibao, kuna wizara za kisekta ambazo pia zina mawaziri manaibu wakurugenzi, maafisa wakuu, maafisa waandamizi, maafisa daraja la I na la II kibao. Wote hao wako kwa ajili ya kumsaidia Rais. Kuna vikao vya mawaziri na vikao vya makatibu wakuu ambayo humshauri Rais na kutekeleza mambo mbalimbali. Duuu kweli utumishi wa umma umevamiwa.