Wamarekani wameshamsoma na kumuelewa vizuri rais wetu and this time wamefanya kweli. Wamemchongea line safi ya kupata Tuzo hata kwa mambo ambayo hajawahi fanya chochote ili mradi tu wanakuza EGO yake maana ni bishoo asiyekuwa na ukomo. Kwa mfano afya ya mama na mtoto inafadhiliwa na UN kupitia shirika lake UNFPA na hata launching ya huu mpango ulichelewa for more than 6 months kwa sababu Rais alitaka awepo but guess what? siku aliyosema ifanyike hakutokeza! it was embarassing na kwenye kurido za mabosi wa UN hapa bongo hawakuamini. Na hata ile idea ya kuleta bajaj za kubeba wajawazito naomba niwataarifu kuwa ni wazo la UNFPA. Serikali hii inafikiria tu kuonekana majukwaani, hakuna la maana.
Pili, kuna vituzo vingine vinavyotambulika NASDAQ na wamerekani walimualika aende kugonga kengele ya kufunga shughuli za soko! Nilivyoona hii picha nilijiuliza hivi Mwl Nyerere angefanya mambo ya hovyo kama haya, ya kugonga kelele kwenye masoko ya wazungu wakati kwako hakuna la maana! Sijui huu umaarufu unaotafutwa marekani unafaida gani kwa watanzania?
Kila anasa anayotaka na kila sifa anayotaka Kikwete Marekani watampa kwa sasa kwa sababu wanataka uranium yetu kwa udi na uvumba. Kumbukeni hata wacheza mpira wa vikapu huko marekani wamekuwa 'regular visitors' siku hizi huko Magogoni. Bado tutaendelea kuona vituzo vya ajabu ajabu toka UN na marekani ili mradi tu bwana mkubwa anapanda kwenye majukwaa. Kwa ujumla Tanzania iko chini ya mfumo wa CHIFU MANGUNGO. Very sad!