Rais Kikwete ahutubia taifa mwisho wa mwezi Februari

Amesema hatua ya kusaini muswada ilikuwa ni kuheshimu maamuzi ya wengi na kwamba kama asingefanya hivyo wabunge wale wasingekubali na wangeona kwamba wamedhalaulika.
 
...mambo makuu anasema ni mgomo wa madaktari ambao anasema kamati ya pinda imekabidhi leo ripoti na wataanza kufanyia kazi kuanzia keso(ameogopa kutoa maamuzi), mauaji ya songea na mabadiliko ya katiba...anasema asingetia saini mswada wa sheria ya katiba angeleta mgogoro mkubwa katika nchi...ameanza hotuba kwa kamera kumuonyesha katika chumba sijui ndio ikulu na leo anatoa hotuba huku akiwa amesimama...hotuba inaendelea hivi sasa...
 
Anaongelea suala la katiba mpya, naona amechanganya zake na za mbayuwayu kama alivyowahi kusema siku zilizopita!!!!!
 
Inafurahisha tunapokuwa na rais ambae anaongelea mauaji na mgomo wa madaktari baada ya madhara kutokea ,kweli hii ni tanzania pekee inawezekanza,zaidi ya mwezi issue ya madaktari leo kiranja mkuu anataka wananchi waamini kuwa ana uchungu nao
 
Eti aliogopa wabunge wengi waliopitisha ule mswada na kwamba hiyo ndo busara yake; akili au matope!!!!
 
mgomo wa madaktari na mauaji ya songea kachelewa yalikuwa matukio ya dharura suala katiba ni sawa.
 
Eti alipitisha ili baadae ifanyiwe marekebisho, kama wale waliopitisha wanggoma!
 
Tume ya kuratibu maoni itatumia miezi 18 au wanaweza kuongeza miezi miwili....watakaohusika kupeleka maoni ya nani anafaa kuwa mjumbe wa tume.
 
Rais mwoga, mwenye wasiwasi, mwenye hofu juu uamuzi kama atauchukua ni rais wa mashaka juu ya uwezo wake!!!!!!!!!!!!!
 
Tume ya katiba mpya itakuwa na wajumbe 32 tu, pasu pasu bara na visiwani!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom