NAAM, tunatambua kwamba hivi sasa kwa matakwa ya Bwamkubwa mwenyewe Tanzania imeanza kujiandaa kuwa koloni la Marekani -kwa heri na shari!
Ninachokijua mimi ni kwamba misaada ya Marekani kwa Tanzania ni kitu kidunchu sana ukifananisha na misaada toka Sweden, Norway, Denmark lakini angalia hotuba ya Bwamkubwa imejaa Marekani, mariakani, Marekani tena na tena lakini wafadhili wa kweli hawapo.
Bila shaka huu ni mtego wa Marekani kujipromoti mbele ya mabaya yake iliyoifanya kwenye nchi za Kiislamu na kwingineko ili Waislamu waliopotea njia na ambao wameanza kukubali sasa misaada ya Marekani wawafanyie Mabwana zao Kazi ikiwa ni pamoja na kuihujumu elimu ya Kiislamu, Kurani na Uislamu wenyewe! Astaghafirulillahi- na someni Kuul audhu biraki falaki mara elfu kumuondoa dhalimu huyu!
Kila mtu anajua sasa kwamba nchi za Kushikana nazo ni China, Russia, India, Brazili, Venezuela, nchi mbalimbali za Kiarabu na hasa UAE lakini tunawashangaa CCM kutuchimbia Watanzania kaburi kwa kutuweka kwenye makwapa ya Marekani ili tuwe kama Vietnam, Iraq, Lebanon na shemu nyingine kama hizo.... ee Mola tuepushe na ujinga wetu!
Baba wa Taifa alishatuambia tuwaogope Marekani kuliko ukoma maana hicho ni kisima cha kufanya mabaya na dhuluma sehemu kubwa duniani-Iraq, Kongo, Ulaya ya Mashariki, Marekani ya Kati na kUsini na kisha kujaribu kukosha madhambi yao kwa kusaidia nchi pumbavu kama Tanzania ya sasa!
Hivi kweli dhahabu makampuni ya Marekani yanayoiba Tanzania haiwezi kutuingizia mabilioni mara 10 ya kile tunachodanganywa na Marekani kama misaada? Wewe unapewa shangaa unatoa almasi saizi ya chungwa -yaleyale ya mababu zetu.....hatutafika, tutafikwa ama kwa hakika na ukweli wa TBC!
Ujanja katika miaka hii ya GLOBALAIZESHENI sio kujiweka mzegamzega kwenye mikono ya mbabe mmoja tu duniani bali kuwachanganya wote kwa kula na huyu na yule bila kumuamini mtu yeyote katika dunia hii ya mtu kula mtu eti!
This is really terrible.
Hivi jamani hatuwezi kuandamana kupinga hizi ziara zisizokuwa na mbele wala nyuma?
Huyu jamaa naona yeye alichofuata ikulu ni kutanua tu hana jingine.
Huwezi kufuata bil 20 wakati kuna bilion 133 na nyinginezo zinaachwa kupotea.
Kwanza gharama ya kusafiri na kukaa huko is more than atakazoahidiwa na sio kupewa
Wandugu ndio uongozi huo......juzi tu alikuwa anapiga misele mikoani kwenye vumbi ili wadanganyika muache kidomodomo; sasa anaenda kupata 'bubble bath' na mai waifu wake mamtoni. Sisi tutaendelea kumshikia nchi yake tu pindi awapo safarini. Akirudi libeneke kama kawa....kwikwikwi!!
Aliesema kuwa ni Vasco da Gama hakukosea. Anaendelea kuvumbua kwa ujinga wake. Hovyoooooo.
Usikute hata Ridhiwani yumo katika msafara kwa kisingizio cha kwenda honeymoon! Jamaa haeleweki huyu!
Kazi tunayo watz,kwani kama Rais anaenda kuanzisha diplomasia ya mchezo wa kikapu na timu mbili zikiwa uwanjani haya ni mauzauza.....
Mbona haionyeshi kama ataweza kukutana na viongozi wa mpira huo?ama wote lazima wanakuwepo hapo uwanjani?