Rais Kikwete aenda Marekani

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,082
Rais Kikwete aenda Marekani
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,August 26, 2008 @00:02

Raisi Jakaya Kikwete aliondoka nchini jana mchana kwenda Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais George W. Bush. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, ziara hiyo inalenga kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa karibu zaidi kati ya Tanzania na Marekani, na shughuli zote za Rais Kikwete wakati wa ziara hiyo zinalenga kufanikisha jambo hilo.

Ilisema malengo makuu ya ziara hiyo yatakuwa ni kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili hasa katika nyanja za elimu, afya na uchumi. Katika siku ya kwanza ya ziara yake keshokutwa, Rais Kikwete atahudhuria hafla ya mfuko wa kwanza katika Marekani kujishughulisha na masuala ya elimu miongoni mwa Wamarekani wenye asili ya Afrika na Waafrika wa The Phleps Stokes Fund, ilisema taarifa ya Ikulu.

Ilisema kwenye hafla hiyo, Rais atazungumzia hali ya elimu ya Tanzania, mafanikio yake na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili sekta hiyo. Baada ya hapo, Rais Kikwete atahudhuria mkutano kuhusu sekta ya afya na hasa jinsi ya kupambana na kuifuta malaria nchini kwenye Kituo cha Maendeleo cha Center for Global Development.

Wakati wa mkutano huo, pia zitatangazwa juhudi mpya na misaada mingine ya Marekani katika kupambana na malaria katika Tanzania. Baadaye siku hiyo hiyo, Rais atakwenda kwenye Bunge la Marekani, ambako itatangazwa rasmi kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Wanyamapori cha International Conservation College kitajengwa Arusha.

Kwenye siku yake ya pili ya ziara hiyo, Rais Kikwete atakwenda Makao Makuu ya Shirika la Misaada la Marekani la USAID ambako itatangazwa rasmi kuwa Marekani itatoa msaada wa dola za Marekani milioni 20 (zaidi ya Sh bilioni 30) kusaidia maendeleo ya kilimo na usalama wa chakula nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe atatia saini makubaliano ambako Marekani itasaidia usimamizi katika sekta za maji na nishati kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati Tanzania (EWURA). Rais pia atashiriki katika majadiliano kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya elimu, na baadaye kushuhudia tangazo ambako Marekani itaipa Tanzania msaada katika sekta hiyo ya elimu.

Msaada huo utakuwa wa vitabu vya kufundishia masomo ya sayansi wa kiasi cha dola za Marekani milioni 1.5, na kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya kufundishia walimu na ujenzi wa maabara tatu za kufundishia lugha ya Kiingereza, iliongeza taarifa ya Ikulu. Rais anatarajiwa kukutana na wawezekaji maarufu katika Marekani.

Kwenye siku ya tatu ya ziara yake, Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais George W. Bush katika Ikulu ya nchi hiyo. Baadaye Rais atakwenda kwenye kituo maarufu cha waandishi wa habari katika Marekani cha National Press Center ambako

Marekani itatangaza misaada zaidi kwa Tanzania katika nyanja ya afya, na hasa katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi na magonjwa ya mlipuko. Chini ya msaada huo wa kupambana na Ukimwi, Marekani itasaidia ujenzi wa vituo viwili vya kisasa kabisa vya watoto, na pia itasaidia kuongeza uwezo wa Tanzania katika kupambana na magonjwa ya mlipuko.

Jioni ya siku hiyo ya tatu ya ziara hiyo, Rais Kikwete atahudhuria mchezo wa mpira wa kikapu wa WNBA kati ya timu za Washington Mystics na Chicago Sky kwenye Uwanja wa Veriton Center. Wakati wa mechi hiyo, itatangazwa rasmi kuanzishwa kwa “Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” ambayo itaanza kufanya kazi rasmi mwezi ujao wakati ujumbe wa wachezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani utakapotembelea Tanzania.
 
Wakati wa mkutano huo, pia zitatangazwa juhudi mpya na misaada mingine ya Marekani katika kupambana na malaria katika Tanzania. Baadaye siku hiyo hiyo, Rais atakwenda kwenye Bunge la Marekani, ambako itatangazwa rasmi kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Wanyamapori cha International Conservation College kitajengwa Arusha.

Hakuna mtu hukoo wako likizo woote, anakwenda kukutana na jengo au?
 
Nadhani hiyo ni Ratiba iliyotolewa na Ikulu. Hawajui sasa hivi vyama vyote viwili viko kwenye conventions zao za kuwapitisha wagombea wao.
 
...anakuja kuchukua msaada dola million 20 huku EPA na Richmondul peke yao wametuingiza mjini zaidi dola milion 400? kweli ujinga mzigo!
 
Hivi siku hizi kuna usimamizi mzuri wa fedha za msaada? Je zitafanya yaliyokusudiwa kweli kulingana na ripoti hii au sehemu yake kubwa itamegukameguka tu na kuishia kusikoeleweka.
 
jamani after a harusi ya mwanae he needs to get a holiday somewhere to rest n enjoy maisha kwa kutumia kodi zetuuuu...nmempenda aliyeask abt kufuata dola milioni 20 wakati epa wamekula dola milioni 400 kwanini asingekaa home kufuatilia zaidi hizo?
 
I think this is p**s taking...

Rais Kikwete aenda Marekani
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,August 26, 2008 @00:02

Raisi Jakaya Kikwete aliondoka nchini jana mchana kwenda Marekani kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais George W. Bush. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, ziara hiyo inalenga kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa karibu zaidi kati ya Tanzania na Marekani, na shughuli zote za Rais Kikwete wakati wa ziara hiyo zinalenga kufanikisha jambo hilo.
Hivi ni mara ngapi huu ukurasa wa mahusiano unafunguliwa?... ina maana safari zote alizoenda kule na hata Bush mwenyewe kufanya ziara Tanzania, ukurasa huu kama kweli una-exist bado haujafunguliwa tu?! Can't we just learn that such a chapter is non existant?!

Hivi tunaielewa kweli Marekani siye? Marekani inauhusiano wa karibu na nchi moja tu hapa duniani, nayo ni Uingereza. Rhetorics nyinginezo za mahusiano ni sawa na nonsense kusikika. Jambo hilo halitafanikishwa hata baada ya miaka miaka 700x7!! For simple reason kwamba, Marekani is after its own agenda and you might not know this for another generations. Tumeyaona ya Georgia hivi karibuni...

Nimesema uhusiano huo hautawezekana kwa sababu moja iliyo indirect, nayo ni kwamba Rais wetu hata ajipendekeze vipi sasa hivi na kuonekana machoni pa Waafrika wenzake yuko karibu na Amerika; kamwe hatakuwa Rais huyo huyo wa milele katika Taifa letu. Hivyo akitokea mwingineyo yeyote atakaye onesha kujali maslahi ya Tanzania zaidi tu, ndipo hapo uhusiano huo utakapo sitishwa. Uhusiano na Marekani unawezekana tu pale unapokubali kugandamizwa nao na si vinginevyo.

Ilisema malengo makuu ya ziara hiyo yatakuwa ni kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili hasa katika nyanja za elimu, afya na uchumi. Katika siku ya kwanza ya ziara yake keshokutwa, Rais Kikwete atahudhuria hafla ya mfuko wa kwanza katika Marekani kujishughulisha na masuala ya elimu miongoni mwa Wamarekani wenye asili ya Afrika na Waafrika wa The Phleps Stokes Fund, ilisema taarifa ya Ikulu.
This time around the primitive propaganda machine ya Ikulu imeamua kufyatuka na kutoa sababu zote zinazompelekea Rais wetu kwenda huko....in my opinion, all this is out of guilty conscious. Matter of fact they have overdone maelezo na kuanza kuonekana wanaremba ziara hii ili kuihalalisha.

Mithili ya mtu aliyekatazwa kunywa pombe lakini kwa ubishi akaenda zake kunywa, kisha waliomkataza wakakutana naye wakiwa na hisia kuwa karudia yaleyale... basi kwa kutaka kuonesha kuwa hajanywa pombe, mtu huyo atatembea au kusimama kwa ukakamavu alimradi tu aonekane yuko stable.. kumbe ndiyo kabisaa kukakamaa huko ndiko kunakoonesha hali isiyo ilivyo.

Ilisema kwenye hafla hiyo, Rais atazungumzia hali ya elimu ya Tanzania, mafanikio yake na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili sekta hiyo. Baada ya hapo, Rais Kikwete atahudhuria mkutano kuhusu sekta ya afya na hasa jinsi ya kupambana na kuifuta malaria nchini kwenye Kituo cha Maendeleo cha Center for Global Development.
Jamani, kazi ya kuzungumzia hali ya mafanikio ya maendeleo katika miradi wanayosaidia si hata Naibu Waziri wa wizara husika anaweza kuifanya?.... Kazi ya Waziri wa Mambo ya Nje ni nini sasa iwapo Mh. Rais anafanya kazi zote hizi za kuelezea maendeleo ya tumiradi tena nje ya nchi.... aaah, this honestly depresses me.

Wakati wa mkutano huo, pia zitatangazwa juhudi mpya na misaada mingine ya Marekani katika kupambana na malaria katika Tanzania. Baadaye siku hiyo hiyo, Rais atakwenda kwenye Bunge la Marekani, ambako itatangazwa rasmi kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Wanyamapori cha International Conservation College kitajengwa Arusha.
Yaani Ikulu wamefanya juu chini kuichachambua hii itenary to the nearest second.... kumbe ndiyo kabisa inazidi kuumbua tu. Rais kama atapewa chance ya kuhutubia Bunge la Marekani kama vile Yule wa Comorro atakavyofanya kwetu, then that's what's up. Anything short of that, ni umahoka.

Kwenye siku yake ya pili ya ziara hiyo, Rais Kikwete atakwenda Makao Makuu ya Shirika la Misaada la Marekani la USAID ambako itatangazwa rasmi kuwa Marekani itatoa msaada wa dola za Marekani milioni 20 (zaidi ya Sh bilioni 30) kusaidia maendeleo ya kilimo na usalama wa chakula nchini.
Duuh, Tujitegemee full stop. Kenya wameweza na wakaweza pia kutoa Olympic champions... sisi kila siku kujiombeleza. Sikio la mwenda wazimu...

Isitoshe, Wizara ya kilimo ina bajeti yake tayari... lets strive within it and evaluate any achievement we set before hand otherwise we'll only be trying to confuse by "sexing up" figures..... pia kuna hela za EPA kwa kiwango hicho hicho au kinachokaribia zinataka kuelekezwa huko... au ndizo hizo hizo?! :confused:
Tulipotamka mapinduzi ya kilimo kwenye bajeti mbili zilizopita, sidhani kama tulitamka hivyo kwa kutegemea hela za kuomba omba.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe atatia saini makubaliano ambako Marekani itasaidia usimamizi katika sekta za maji na nishati kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati Tanzania (EWURA). Rais pia atashiriki katika majadiliano kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya elimu, na baadaye kushuhudia tangazo ambako Marekani itaipa Tanzania msaada katika sekta hiyo ya elimu.
Mh. Membe anglitosheleza katika makubaliano haya. Mh. Rais angelibaki nyumbani kutafuta suluhisho la Muungano. Siku mbili tatu naamini zingelizaa matunda fulani... Time is a resource, let's value it ipasavyo na si kuitumia kama airmiles za ku-criss cross continents.

Msaada huo utakuwa wa vitabu vya kufundishia masomo ya sayansi wa kiasi cha dola za Marekani milioni 1.5, na kiasi cha dola 500,000 kwa ajili ya kufundishia walimu na ujenzi wa maabara tatu za kufundishia lugha ya Kiingereza, iliongeza taarifa ya Ikulu. Rais anatarajiwa kukutana na wawezekaji maarufu katika Marekani.
Haya mambo ya Umatonya are now really getting out of control. That's not a lot of money za kumpelekesha Mh. Rais wetu kwenda huko.... am sure you can acquire the same sum by enhancing ukusanyaji wa kodi tu mikoani, and it won't be months before you hit the target.

Kazi ya Board of External Trade imeishia wapi mpaka Mh. Rais ndiye akakutane na wannabee wawekezaji?

Kwenye siku ya tatu ya ziara yake, Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais George W. Bush katika Ikulu ya nchi hiyo. Baadaye Rais atakwenda kwenye kituo maarufu cha waandishi wa habari katika Marekani cha National Press Center ambako

Marekani itatangaza misaada zaidi kwa Tanzania katika nyanja ya afya, na hasa katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi na magonjwa ya mlipuko. Chini ya msaada huo wa kupambana na Ukimwi, Marekani itasaidia ujenzi wa vituo viwili vya kisasa kabisa vya watoto, na pia itasaidia kuongeza uwezo wa Tanzania katika kupambana na magonjwa ya mlipuko.
Arrrgh, Tanzania ni guinea pig wa USAID na PR exercises zao?!... je umma umefahamishwa hili?

Jioni ya siku hiyo ya tatu ya ziara hiyo, Rais Kikwete atahudhuria mchezo wa mpira wa kikapu wa WNBA kati ya timu za Washington Mystics na Chicago Sky kwenye Uwanja wa Veriton Center. Wakati wa mechi hiyo, itatangazwa rasmi kuanzishwa kwa "Diplomasia ya Mpira wa Kikapu" ambayo itaanza kufanya kazi rasmi mwezi ujao wakati ujumbe wa wachezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani utakapotembelea Tanzania
Waziri wa Michezo kakaa wiki mbili China na kashindwa kabisa kutumia muda huo kukamilisha hayo akiwa huko...anyway, najua asingeweza (sababu nyingi ati) ... lakini leo hii yahitaji Mh. Rais ili kuwekeza katika Diplomasia ya Basket Ball. I believe Super Tall Thabit angelitosha.

Daaah, ngoja nikalale tu.... i hope sitakuwa na nightmares za haya mambo.. :( :(
 
Steve D,

Ngoja nikuongezee uchungu zaidi!

Mwezi ujao atarudi tena na kwenda NY kwenye Baraka Kuu la Umoja wa Mataifa!
 
Steve D,

Ngoja nikuongezee uchungu zaidi!

Mwezi ujao atarudi tena na kwenda NY kwenye Baraka Kuu la Umoja wa Mataifa!

Na kundi kubwa la the so called wapambe watakaoandamana na wake zao au waume zao ili kufanya shopping ya nguvu kujiandaa kwa Xmas! Ooops na Idd :)
 
Kikwete ni usanii mtupu

Kuna watu bado hawalioni hilo!! Wanaona ni mchapa kazi mzuri. Ukiwauliza ni kipi alichokifanya tangu aingie madarakani kuhusiana na ahadi alizotupa Watanzania wakati wa kampeni za uchaguzi wanaanza kung'aa macho na kutoa blah blah zao.
 
Ameenda kumtengenezea mazingira mazuri ya hny moon ya bwana na bibi ridhiwani jakaya mrisho kikwete jamani hayo mengine badaae
 
Ameenda kumtengenezea mazingira mazuri ya hny moon ya bwana na bibi ridhiwani jakaya mrisho kikwete jamani hayo mengine badaae

Nafikiri hii inaweza kuwa kweli; nani anajua waliokuwamo kwenye msafara wake?
 
Kwa kweli tangu Alhamis iliyopita nimekuwa nikipata nightmares almost kila usiku juu ya utawala mbovu wa jamaa! Sijawahi kujua wanasiasa wanaweza kunipa taabu kiasi hiki!

Huyu jamaa sasa naona anaturudisha enzi za Mzee Mwinyi, maana vituko ndio vimeanza! Watu waandamane kuunga mkono hotuba! Kumbuka watu waliandamana wanafunzi chuo kikuu walipofukuzwa mwaka mzima!!! Kweli jamaa wanawekeza kwenye ujinga wa wananchi! Ndio usema wanampango wa kukuza elimu! Subutu!!!!
 
Kazi tunayo watz,kwani kama Rais anaenda kuanzisha diplomasia ya mchezo wa kikapu na timu mbili zikiwa uwanjani haya ni mauzauza.....

Mbona haionyeshi kama ataweza kukutana na viongozi wa mpira huo?ama wote lazima wanakuwepo hapo uwanjani?
 
Na kundi kubwa la the so called wapambe watakaoandamana na wake zao au waume zao ili kufanya shopping ya nguvu kujiandaa kwa Xmas! Ooops na Idd :)
Bubu! kule kwetu mtu akipata habari mbaya anapiga lwangwi,(sijui kama umenipata hapo) nami napiga kwa sauti kuu, UUWIII!
 
Muheshimiwa kaja kipindi kibaya, na cha kusikitisha siku ambayo yeye anataka kuongea na Bush ndio siku amboyo ma analyst wote wa politics wanaanlyze Obama party nomination. So, no one will even cares about Tanzania.

Vile vile wamarekani wanasuffer na hali ngumu, hivyo kusikia kwamba kuna bingwa kaja kuchota 20M nyingine itakuwa ni kuwapandisha mzuka.

Lakini mheshimiwa bado ana opportunity ya Kukutana na special people aka WATANZANIA. ooohh ukitaka ubalozi ugeuke jiwe waambie JK anaombwa akutane na watanzania waishio US.

Mswahili president... kazi tunayo
 
NAAM, tunatambua kwamba hivi sasa kwa matakwa ya Bwamkubwa mwenyewe Tanzania imeanza kujiandaa kuwa koloni la Marekani -kwa heri na shari!

Ninachokijua mimi ni kwamba misaada ya Marekani kwa Tanzania ni kitu kidunchu sana ukifananisha na misaada toka Sweden, Norway, Denmark lakini angalia hotuba ya Bwamkubwa imejaa Marekani, mariakani, Marekani tena na tena lakini wafadhili wa kweli hawapo.

Bila shaka huu ni mtego wa Marekani kujipromoti mbele ya mabaya yake iliyoifanya kwenye nchi za Kiislamu na kwingineko ili Waislamu waliopotea njia na ambao wameanza kukubali sasa misaada ya Marekani wawafanyie Mabwana zao Kazi ikiwa ni pamoja na kuihujumu elimu ya Kiislamu, Kurani na Uislamu wenyewe! Astaghafirulillahi- na someni Kuul audhu biraki falaki mara elfu kumuondoa dhalimu huyu!

Kila mtu anajua sasa kwamba nchi za Kushikana nazo ni China, Russia, India, Brazili, Venezuela, nchi mbalimbali za Kiarabu na hasa UAE lakini tunawashangaa CCM kutuchimbia Watanzania kaburi kwa kutuweka kwenye makwapa ya Marekani ili tuwe kama Vietnam, Iraq, Lebanon na shemu nyingine kama hizo.... ee Mola tuepushe na ujinga wetu!

Baba wa Taifa alishatuambia tuwaogope Marekani kuliko ukoma maana hicho ni kisima cha kufanya mabaya na dhuluma sehemu kubwa duniani-Iraq, Kongo, Ulaya ya Mashariki, Marekani ya Kati na kUsini na kisha kujaribu kukosha madhambi yao kwa kusaidia nchi pumbavu kama Tanzania ya sasa!

Hivi kweli dhahabu makampuni ya Marekani yanayoiba Tanzania haiwezi kutuingizia mabilioni mara 10 ya kile tunachodanganywa na Marekani kama misaada? Wewe unapewa shangaa unatoa almasi saizi ya chungwa -yaleyale ya mababu zetu.....hatutafika, tutafikwa ama kwa hakika na ukweli wa TBC!

Ujanja katika miaka hii ya GLOBALAIZESHENI sio kujiweka mzegamzega kwenye mikono ya mbabe mmoja tu duniani bali kuwachanganya wote kwa kula na huyu na yule bila kumuamini mtu yeyote katika dunia hii ya mtu kula mtu eti!
 
Ninaambiwa kisa ni watoto wa wenyewe kusoma Marekani na kisha hivi sasa kwa Vigogo na Vizito wa Tanzania kuwa wabia wa Marekani katika kuhakikisha wanachimba madini mbalimbali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na dhahabu, almasi, mkaa wa mawe, uranium na cobalt bila Mtanzania wa kawaida kunufaika na lolote wallahi!
 
Jamani ni lazima tuelewe kwamba ili watanzania tuheshimike duniani ni lazima sisi na nchi yetu iwe inatendea haki kwa wananchi wake na watu wote wanaoishi Tanzania.Kutenda haki kwa wananchi ni kutowaibia kodi zao na hela nyingine za mapato zinazokusanywa na serikali.Haki za binadamu ziheshimike, za wawekezaji na kadhalika.Nchin kama marekani kuwa na uhusiano mzuri na sisi inabidi viongozi wetu waonyeshe mafano mzuri. Nchi masikini kama hii kiongozi akitumia pesa za watu masikini kwenda kulala kwenye hoteli ambayo usiku mmoja unaweza kujenga darasa la shule ili watoto wasiketi chini wamarekani wanayaona hayo na wanatushangaa.Ushirikiano wetu na marekani utakuwa wa upande mmoja kwani sisi kazi zetu kuomba kwao tu na wala sisi sio masikini. Wanashindwa kutuelimisha kwani ni aibu. Wajehapa wachukue mali gafi zote alafu watutupie kidogo . Wanatuonea huruma.Hakuna uhusiano hapo ni aibu kwao.
 
Back
Top Bottom