Rais Kikwete Aagiza Kidato Cha 5&6 Kila Kata

tatizo siyo roho mbaya mkuu,hebu hata na wewe jiongeze basi na kiakili chako hicho kinachokusaidia kusaka tonge kwa shida,kipi bora kuboresha olevel katika shule hizo au kuongeza alevel wakati olevel ni hovyo kabisa?au kwa kuwa wanenu wako international schools na abroad?

sikiliza kijana , mkubwa akisema hiyo ni sawa na amri , kinachofuatia ni utekelezaji tu , jengeni hata ya makuti kama vipi tutaboresha taratibu huko mbele .
 
Ungesema agizo la kujenga UDOM lilitolewa na Mkapa, JK akajenga, vivyo hivyo agizo likitolewa na JK, utekelezaji utafanywa na Prof. Mwandosya ningekubaliana na wewe
Kama kweli katoa agizo basi ni Jambo jema, Kikwete anaipenda Nchi yake sana, Alipotoa Agizo kujenga Udom waliobeza wameaibika baada ya Mafanikio makubwa kuonekana, Udom pekee ni kama jiji.

Agizo la JK litekelezwe haraka.
 
Sidhani kama ni agizo linalotakiwa kuanza kutekelezwa kesho ama kesho kutwa.

Kasema tuanze kufikiria kujenga au ku-epand baadhi ya shule za kata ili absorption ya 25% ya wanafunzi wenye sifa ambao kwa nafasi na idadi ya shule za High Secondary Education za sasa hazitoshi.

Mimi ni mdau wa elimu na kwa hili sina budi kuona kuwa serikali imejitahidi na nifahamuvyo ni kuwa mpaka sasa karibu kila wilaya ina shule zisizooungua mbili za kidato cha 5 & 6. Na mpango ulishaanza siku nyingi wa kuwa na High Secondary School ingalau moja kwa kila tarafa, jambo ambalo ni zuri kwa kweli.

Pia pamoja na kuipongeza serikali ktk hili ni lazima ikubali kuwa kuna changamoto nyingi na kubwa zinazoikabili sekta ya elimu kwa ujumla ktk Taifa letu.

Na kiukweli changamoto zinatokana na mipango mibovu na mibaya inayofanywa na serikali ya CCM ambayo mwisho wa siku wananchi ndiyo wanayobeba mizigo ya gharama ya miradi hiyo isiyopangwa vyema.

Mfano ni ujenzi wa shule za sekondari za kata ulioanza mwaka 2005 na wananchi kutoa ushirikiano mzuri tu. All the way watu wakapiga hela sana (ufisadi) na matokeo yake mengi ya majengo yakashindwa kukamilika mfano maabara za masomo ya sayansi, madarasa na nyumba za mwalimu ambazo hadi leo yamebaki kuwa ni magofu na sasa kwa kuwa serikali ya awamu ya nne inamaliza muda wake miezi minne tu ijayo inakurupusha wananchi kutoa fedha kwenye mifuko yao kumalizia majengo hayo ambayo kiukweli na tunafahamu fedha zilitengwa ktk bajeti za nyuma na kufisadiwa.

Very funny kuwa wananchi hata wa vijijini wanajua hili na watendaji wa serikali wanapata taabu sana kuwashawishi wananchi kuchangia miradi kama hii ambayo fedha zake zilishaliwa na mafisadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kashfa/ufisadi wa Richmond, EPA, Escrow nk

Na kwa sbb hii tu ni lazima hawa CCM wawe punished katika namna nyingi na kubwa ni kupitia sanduku la kura katika uchaguzi wa mwaka huu 2015 kwa kuwanyima kura!!
 
bila shaka hii my take ni ya mtu aliyevuta bangi.

RAIS Jakaya Kikwete ameagiza Wakuu wa Mikoa na Maofisa Elimu wote nchini, kuanza ujenzi wa shule maalumu za kidato cha tano na sita kwa kila kata na wakishindwa, katika shule za sekondari za kata, wachague baadhi na kujenga madarasa ya vidato hivyo.

Alitoa agizo hilo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu, yaliyoadhimishwa kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na kuwakumbusha kuwa kati ya wanafunzi waliofaulu kwenda kidato cha tano mwaka huu, ni asilimia 75 tu walioendelea na masomo hayo.

“Wakuu wa mikoa na maofisa elimu mliopo hapa naagiza na hili ni kwa nchi nzima, tuanze utaratibu wa kuwa na shule za kidato cha tano na sita za kata. Mnaweza kujenga shule mpya, au mchague baadhi ya sekondari za kata ziwe na kidato cha tano na sita,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kusema si vyema kuwaacha mtaani asilimia 25 wenye sifa ya kuingia kidato cha tano.

Alisema bila kuchukua hatua hiyo, Tanzania inaweza kurudi katika hali ya elimu aliyoikuta ambapo wanafunzi wenye sifa ya kuendelea na masomo, waliachwa kutokana na ufinyu wa nafasi za kuendelea na elimu.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wakati alipokuwa akiingia madarakani, alikuta asilimia sita tu ya wanafunzi waliokuwa wamefanya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba, ndio waliokuwa wakichaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari.

“Leo kila anayefaulu darasa la saba, anakwenda sekondari… tukisema leo mwanafunzi amefeli darasa la saba amefeli kweli tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichaguliwa,” alisema Rais Kikwete.

Tanzania ilipotoka Rais Kikwete alielezea sababu ya Serikali inayomaliza muda wake kuwekeza zaidi katika elimu, kiasi kwamba bajeti ya elimu katika Mwaka wa Fedha unaoisha kuwa kubwa kuliko ya sekta zingine, inayofikia Sh trilioni 3.4 kutoka Sh bilioni 600 iliyokuwepo mwaka 2005.

Sababu ya kwanza Rais Kikwete alisema, waliona kuwa kuwekeza katika elimu ndio kuwekeza katika taifa na Serikali isingechukua uamuzi huo, Watanzania hawataweza kutawala mazingira yao na kutumia vizuri rasilimali zao.

Pili alisema alipoingia madarakani, alikuta Tanzania yenye watu wengi zaidi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, iko nyuma ikilinganishwa na Kenya na Uganda, kwa idadi ya wanafunzi waliokuwa wakisoma shule za sekondari na vyuo.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, mwaka 2005 wanafunzi waliokuwa wakisoma sekondari ni zaidi ya 500,000, wakati nchini Uganda waliokuwa wakisoma sekondari walikuwa zaidi ya 700,000 na Kenya zaidi ya 900,000.

Kwa upande wa vyuo vikuu, Tanzania ilikuwa na wanafunzi 40,000 tu wakati Uganda ilikuwa na wanafunzi 124,000 na Kenya 180,000.

“Kuwa nyuma katika kutoa fursa ya elimu ikilinganishwa na wenzetu ilikuwa inaweka nchi yetu katika mazingira mabaya katika ushindani wa soko la ajira la Afrika Mashariki,” alisema Rais Kikwete.

Mbali na mazingira mabaya katika ushindani wa soko la Afrika Mashariki, Rais Kikwete alisema Watanzania nao walifikia hatua ya kuamua kupeleka watoto wao kwenda kusoma Kenya na Uganda.

Hatua zilizochukuliwa, Rais Kikwete alisema Serikali kwa kushirikiana na wananchi, waliamua kujenga shule za sekondari za kata, ambapo wananchi walihamasishwa, wakahamasika wakajenga shule mpaka Mkurugenzi mmoja wa elimu, akahofia kukosa walimu wa kupeleka katika shule hizo.

“Tulihimiza wadau wengine wajenge vyuo vya elimu ya juu na kuamua mikopo ya elimu ya juu itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vyote,” alisema Rais Kikwete.

Alibainisha kuwa kwa sasa Tanzania ina wanafunzi 1,800,000 wanaosoma sekondari na imeshaipita Uganda yenye wanafunzi 1,700,000 wanaosoma elimu ya sekondari, lakini imezidiwa na Kenya ambayo ina wanafunzi 2,100,000.

Hata hivyo alisema ni rahisi kuipita Kenya kwa hilo pengo la wanafunzi 300,000, kwa kuwa shule za sekondari zilizopo zina nafasi ya kuongeza wanafunzi milioni mbili zaidi.

“Hapa lazima tuwafukuzie Wakenya, lazima tuwakute na kuwapita na huu ni ushindani mzuri kwa kuwa ni ushindani wa maendeleo,” alisema Rais Kikwete.

Kwa upande wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema vyuo vikuu vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2005 hadi kufikia 52 na idadi ya wanafunzi walio katika vyuo vikuu ilitoka 40,719 hadi kufikia 200,956.


Chanzo:
Habari Leo

My Take: Tunakimbilia wapi ilhali elimu inayotolewa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ubora wake hauridhishi?
 
My Take: Tunakimbilia wapi ilhali elimu inayotolewa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ubora wake hauridhishi?

Sasa wewe boresha, madarasa unayo, Waalimu unao. Ungeboresha elimu wakati ulikuwa hauna hata madarasa ya kuwaweka wanafunzi?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Kikwete kauwa kuchaguana kisayansi kabisa.

Hilo ni dongo zito sana ambalo wengi hawatopenda kulisikia.

Utawaina humuhumu, sasa hivi.
 
tatizo siyo roho mbaya mkuu,hebu hata na wewe jiongeze basi na kiakili chako hicho kinachokusaidia kusaka tonge kwa shida,kipi bora kuboresha olevel katika shule hizo au kuongeza alevel wakati olevel ni hovyo kabisa?au kwa kuwa wanenu wako international schools na abroad?

Sasa zikibireshwa zikawa tayari,hao wanaotoka o level wataenda wapi?
 
asilimia 95 wanamaliza na div o,div 5 na div 4 za mwisho ambazo hata a'level hawawezi kwenda.hata kazi zisizotumia elimu sana kama police tu huwa wana cut points.sasa kama unaandaa alevel kwa ajili ya asilimia 5 tu,na asilimia 95 imepotea hapo unasaidia au unabomoa?

Acha uongo!lete hapa idadi ya wanafunzi wa shule za kata kwa miaka 2,2013&2014, idadi ya jumla yao!waliofaulu&waliofeli ili tuthibitishe hiyo % ulioiweka hapo!
 
Watu wengine bana kwani agizo la kikwete au agizo la Rais tumia akili mkuu jk alikuwa akizungumza kama Rais siyo kikwete.
 
mkijua kuwa ni agizo la rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mtaelewa kuwa linapaswa kutekelezwa kikamilifu na si kujisemesha maneno yasiyosaidia watanzania, watanzania wanahitaji elimu na hizo ni hatua ambazo serikali inazidi kuchukua
kuboresha elimu
 
Nyingi ya hizo shule za kata ni majanga tu! Hawaoni hata haya kujisifia nazo? Angefanya vema pia kuagiza hizo shule zote ziwe na ratio ya mwalimu kwa mwanafunzi inayotakiwa kitaalamu, ziwe na maabara na vitabu vya kutosheleza idadi ya wanafunzi.a
 
Back
Top Bottom