Bashungwa aweka jiwe la msingi shule ya sekondari Jakaya Kikwete - Chalinze

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
757
932
BASHUNGWA AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA SEKONDARI JAKAYA KIKWETE - CHALINZE

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Dira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuongeza idadi ya Shule za Msingi na Sekondari ili kuondoa adha kwa wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu na kupunguza msongamano wa Wanafunzi madarasani.

Bashungwa ameeleza hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Shule ya Sekondari Jakaya Kikwete inayojengwa na Serikali kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika kijiji cha Msolwa, Halmashauri ya Wilayani Chalinze Mkoani Pwani kwa gharama ya Shilingi Milioni 470.

“Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameondoa changamoto ya watoto wetu kutembea umbali mrefu na msongamano wa wanafunzi madarasani kupitia mkakati wa kujenga Sekondari kila Kata na hata kama ipo na kuna umbali mrefu anaongeza shule ya pili kama alivyofanya hapa”, amesisitiza Bashungwa.

Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Jakaya Kikwete umesaidia kuondoa usumbufu kwa wanafunzi kutembea umbali wa kilometa 10 kufuata Shule Mama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ameeleza kuwa Shule ya Sekondari Jakaya Mrisho Kikwete ni moja kati ya Shule mpya za Msingi 48 na Shule mpya za Sekondari 42 na hivyo kufanya Mkoa Pwani kuwa na jumla ya Shule za Msingi 795 na Shule za Sekondari 264.

Naye, Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Godwin Mukaruka ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha miundombinu iliyobakia kupitia makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
IMG-20241012-WA0983.jpg
IMG-20241012-WA0995.jpg
IMG-20241012-WA0993.jpg
IMG-20241012-WA0991.jpg
IMG-20241012-WA0989.jpg
 
Back
Top Bottom