Rais Kikwete Aagiza Kidato Cha 5&6 Kila Kata

Roho mbaya wa chama fulani bado anaendelea kumeng'enya ubongo wa wafuasi wake. Huwezi kuwa unapinga kila kitu hata kilicho na manufaa.

Kama ameona kuna tatizo sasa hivi linahitaji kuanza kufanyiwa ufumbuzi aache kutoa maamuzi kisa anakaribia mwisho wa madaraka?

Tatizo mnataka matamko yenye manufaa kwa wananchi yatoke kwa viongozi wa upande wenu tuu. Yakitoka upande mwingine tofauti na ninyi mnapinga.

Asante kaka afu mi cwapend watu wenye akil finyu km hawa wanaoegamia vyama vyao.
 
Agizo lije na fedha siyo michango kutoka watumishi, wakati fedha zipo mfukoni mwa chengea na wenzake (am talking about billions)!
 
Wakati akiwa amebakiza muda wa takribani miezi minne na nusu tu muda wake wa kukaa madarakani kwa mujibu wa katiba uishe,Kikwete ameagiza kila shule ya kata iwe na kidato cha tano na sita.Agizo hilo alilitoa jana mjini Dodoma.

My take;
Tununue vifaa vya maabara kwa maabara zilizojengwa hivi karibuni au tuanze ujenzi mpya wa madarasa/majengo ya kidato cha tano na sita kwa kila kata?

Kipi kiwe kipaumbele kwa sasa?

Maabara zilijengwa wapi na wapi? Acha utani aisee
 
Agizo la kujenga maabara lilichukua miezi mitatu tu kukamilika. Sasa kwanini hilo la kidato cha 5 na 6 uone maajabu wakati walimu wapo wa kutosha kwa sasa?

Zilijengwa wapi hizo maabara wee hawala?
 
...kweli maajabu!!
Bora angetuachia maktaba kila secondary, hzo form 5 na 6 zlzopo tu wanafunz wanaochaguliwa hawazjaz
 
Binafsi sikubaliani naye,angetoa agizo kila kanda ikajenga VETA bora kabisa mbili mbili kwa kila kanda kidogo ningemwelewa maana shule zimekuwa ziki"manufacture in JK voice"jobless......bado hajanishawishi kabisa kwa hili,wananch wamechoka na michango isiyo na tija,wamechanga maabara lakini hazifanyi kazi kabisa yamebakia ni mahall ya sherehe za shule.
 
Bila shaka wewe ni mbinafsi!! Kwavile ulipata elimu hupendi wala hutaki kuona wadogo zako na wanao wakipata elimu kwa "urahisi".

Unataman kwa vile ulisomea chini ya mwembe na wadogo zako wasomee hapo hapo! Unatamani kwa vile kijijini kwenu ulisoma peke yako, hutaki mwingine asome

Fikiri kwanza kabla haujashabikia. Katika kila kata kuna shule moja ya sekondari kwa watani. Kila shule unaweza kuta wanafunzi hawazidi 120 kidato. hebu fikiri sasa tujenge shule ya idato cha tano na sita kila kata kwa maana kuwa hata atakaepata division five anatakiwa aende kidato cha tano. Hivi mh rais anawafahamu wanafunzi wetu wanaotakiwa waende kidato cha tano? Hisia yangu ni kuwa hata waziri wa elimu na uongozi wake hautambui chakufanya kuboresha elimu yetu.

Lakini pia, wakati wadau wamekuwa wakipiga kelele kuwa shule zetu zimekuwa mno local wakimaanisha kuwa watoto wakimasai hapo walipozaliwa watasomea hapo awali hadi kidato cha sita. Hapa tunachochea ukabila na yawezekana kabisa ka-udini nako kataweza kukuzwa na mitazamo ya aina hii ya maendeleo
 
Elimu yetu inahitaji umakini sana iboreshwe issue hapa si quantity kama ambavyo nchi yetu muda mwingi imekuwa ikishabikia. Jukwaa hili kwa hoja hii tulipaswa kuishauri vema serikali ya Kikwete kuliko tunavyoshabikia. Hurumieni watoto wa taifa hili
 
UDOM ni bomu litakalilipuka muda ukifika wala siyo mafanikio ya kujivunia

Bomu lipi mkuu wakati vijana wanasoma wanagraduate katika fani mbalimbali na wengine tayari wanalitumikia taifa,hata hao wanasiasa wanaokukalilisha baadhi yao wanasoma palepale postgraduate degree zao, by the way kule kuwepo tu kwa yale majengo ni sehemu ya mafanikio hata hilo hulioni mkuu? wake up.
 
kabla ya kujenga advanced level angeamrisha viwango vya kujiunga kidato cha tano tofauti na vilivyo sasa ili tupate wanafunzi kwenye shule zetu angalau mtu akipata E mbili achaguliwe. Kinyume na hapo anachekesha walevi
 
Wakati akiwa amebakiza muda wa takribani miezi minne na nusu tu muda wake wa kukaa madarakani kwa mujibu wa katiba uishe,Kikwete ameagiza kila shule ya kata iwe na kidato cha tano na sita.Agizo hilo alilitoa jana mjini Dodoma.

My take;
Tununue vifaa vya maabara kwa maabara zilizojengwa hivi karibuni au tuanze ujenzi mpya wa madarasa/majengo ya kidato cha tano na sita kwa kila kata?

Kipi kiwe kipaumbele kwa sasa?

Kwa hiyo anamaanisha elimu ya k6 itakuwa nayo ya lazima? Kwani zilizopo zinajaa? Hapa tuwe waangalifu, kuna hatari ya kuchukua mpaka div 4 kwenda high school ni bora akaacha huu mpango kama alikuwa na nia ya dhati angeagiza kila tarafa ndo iwe na k5 na 6! Akili yake fupi amqachie rais anayekuja labda yeye atakuwa na akili bwana!!
 
Wakati akiwa amebakiza muda wa takribani miezi minne na nusu tu muda wake wa kukaa madarakani kwa mujibu wa katiba uishe,Kikwete ameagiza kila shule ya kata iwe na kidato cha tano na sita.Agizo hilo alilitoa jana mjini Dodoma.

My take;
Tununue vifaa vya maabara kwa maabara zilizojengwa hivi karibuni au tuanze ujenzi mpya wa madarasa/majengo ya kidato cha tano na sita kwa kila kata?

Kipi kiwe kipaumbele kwa sasa?
pole sana kijana , hii ndio ile tunaita BRN .
 
Back
Top Bottom